Wei Dalun, msanii wa Jumba la Sinema na Michezo la Wananchi la Wilaya ya Qixian, jimboni Henan, anasifiwa kuwa ni "gwiji wa mamung'unye', kwa sababu yeye ni hodari sana wa kuchora nakshi za picha kwa uunguzaji juu ya mamung'unye.
Wei Dalun alizaliwa katika familia ya mchoraji. Aliwahi kupata elimu bora katika Shule ya Sanaa ya Kaifeng wakati alipokuwa mtoto. Miaka 10 iliyopita, wakati Wei alipokaribia umri wa miaka 50, alipata wazo jipya la uvumbuzi. Mamung'unye makubwa na madogo yenye maumbo mazuri na sura ya kung'ara yalichochea hamu yake ya kutia nakshi za picha juu yake.
Lakini, kutia nakshi za picha kwa uunguzaji juu ya mamung'unye manene ya mviringo si kazi rahisi. Wei alifanya majaribio mengi na kubadilisha vifaa mbalimbali, hatimaye, kipingo cha fedha cha nywele kilichotumiwa na mkwe wake kilimfanikishia kazi hiyo. Alivumbua kalamu ya umeme iliyotengenezwakutoka kipingo cha fedha cha nywele na kuitumia kutia nakshi za picha kwenye mamung'unye kama apendavyo.
Katika Maonyesho ya kwanza ya "Maajabu 100 ya China" yaliyofanyika huko Guangzhou, Wei Dalun alitia nakshi za picha mbalimbali kwa uunguzaji kwenye mamung'unye zaidi ya 200 hadharani. Mamung'unye hayo yalipendwa sana na watazamaji na yote yalimumuliwa.
Miaka michache ya karibuni, Wei alitengeneza papo hapo mamung'unye zaidi ya 600 yenye picha za sura za watalii kutoka nchi zaidi ya 20 zikiwemo Marekani, Japani, Uingereza na Ufaransa na ndugu zetu kutoka Hong Kong, Macao na Taiwan. Watalii walishangaa sana walipoona picha za sura zao zilivyotokea kwenye mamung'unye.
Bi. Wu Hezhen ni mchoraji wa Taiwan, ambaye alipania kutembea na kuchora duniani kote. Katika ziara yake hii, alitembelea Ulaya, Marekani na Afrika Kusini. Kwa kulinganisha tofauti kati ya taathira ya utamaduni wa China na Magharibi, alitambua umuhimu wa utamaduni wa China na kupiga moyo konde kuukuza. Mwaka 1994, alirudi China bara, alivinjari Mkoa wa Xinjiang, Tibet, Guangxi na Jimbo la Qinghai, Sichuan, Guangdong, Shananxi na Jiangsu. Kutokana na shauku yake kwa utamaduni wa jadi wa taifa na utamaduni wa kienyeji wa Beijing, mwaka 1995 Bi. He aliingia Chuo Kikuu cha Filamu cha Beijing na kusoma katika kitivo cha sanaa na uchoraji.
Baada ya miaka 3, Bi. He alipata shahada ya masta. Wakati huu, alimaizi Dhahiri kuwa jukumu la msanifu kama yeye ni kuzalisha matunda ya utamaduni wa taifa na kuwagawia wananchi wake, lakini, kwa sasa anapaswa kubeba wajibu wa kuingilianisha utamaduni kati ya China bara na Taiwan. Si siku nyingi zilizopita, alifanya maonyesho ya michoro yake ya kuhitimu katika Jumba la Sanaa la China, jijini Beijing. Michoro yote ni juu ya Taiwan, hii ni hatua ya kwanza katika mwendo wake wa kutimiza wajibu wa utamaduni. Kutoka nafasi ya pekee ya kuangalia, michoroa ya Bi. He ilionyesha ustaarabu wa kisasa wa kiutamaduni wa Taiwa, pia ilionyesha upendo wake mkubwa wa dhati kwa watani wake. Mchoro "Gari la Ng'ombe" unawavusha watazamaji kikwazo cha nyakati, wakifuata nyayo za mababu wanaingia eneo la watani wao. Katika mchoro wa "Wasichana Wanachuma Majani ya Chai", michai ya kijani inasambaa kote ardhini, wasichana wazuri wanacharaza mikono kwa ubingwa na furaha. Katika mchoro wa "Pirikapirika katika Soko la Samaki", kelele za kupigana bei zinaingiwa na masikilizano na mapenzi baina ya watu kwa watu. "Miavuli ya Karatasi", kwa rangi za kupendeza unaonyesha uchangamfu na furaha ya wenyeji wa kusini wakiwa chini ya mionzi ya jua. "Tamasha la Taa, Sikukuu ya Zhongyuan" unaonyesha hali ya nderemo na ukarimu wa Wataiwan kwa wageni.
Idhaa ya Kiswahili 2004-06-18
|