Mradi mkubwa unaojengwa hivi sasa wa kupeleka gesi yaasili ya sehemu ya magharibi hadi sehemu ya mashariki ya China ni mradi unaogharimu fedha nyingi, na ni moja ya hatua muhimu zinachochukuliwa na serikari ya China katika ustawishaji wa uchumi wa sehemu ya magharibi. Je, mradi huo sasa uko katika hali gani tangu ulipoanza kujengwa? Mradi huo sasa umeanza kuleta ufanisi kama ilivyotarajiwa na serikali hapo awali? Hivi karibuni mwandishi wetu wa habari Bi. Xu Jian-ying alikuwa na mahojiano na baadhi ya wafanyakazi wa ujenzi wa mradi huo na upelekaji gesi na kufahamisha maendeleo ya ujenzi wake.
Mradi wa upelekeaji gesi ya asili kutoka sehemu ya magharibi hadi mashariki ya China ambao ulianza kujengwa mwezi wa Julai mwaka 2002 na kugharimu fedha za Renminbi Yuan bilioni 140, sawa na dola za kimarekani bilioni 17.1, utapeleka gesi ya asili ya sehemu ya Talimu ya mkoa wa Xinjiang Weur hadi mkoa wa Jiangsu, mji wa Shanghai na sehemu ya delta ya mto Changjiang. Mabomba ya kupeleka gesi yana urefu wa kilomita zaidi ya 4,000 na kupita kwenye mikoa na miji 10 kwa jumla ikiwemo Xinjiang, Sanxi, Jiangsu na Shanghai.
Bw. Wu ni naibu meneja mkuu wa kampuni ya mradi wa upelekaji wa gesi kwa mabomba ambayo inashughulikia ujenzi wa mradi, upelekaji na mauzo ya gesi. Alipohojiwa na mwandishi wa habari alisema kuwa tangu ujenzi wa mradi ulipoanza, kazi zote zimefanyika bila matatizo, na hivi sasa, theluji mbili ya ujenzi wa mradi imekamilika.
"Tangu ujenzi wa mradi wa upelekaji wa gesi kuzinduliwa rasmi tarehe 4 mwezi Julai mwaka uliopita, ujenzi wa mradi uliendelezwa kufuatana na mpango uliopangwa. Hivi sasa karibu watu elfu 20 wanajenga mradi huo kutwa na kucha. Tuna uhakika kwamba tutafikia lengo la kupeleka gesi Shanghai tarehe 1 Juanuari
Mradi wa upelekaji wa ges ya sehemu ya magharibi kwa sehemu ya mashariki ya China ni mradi mmojawapo miongoni mwa miradi mikubwa ya China ya kustawisha sehemu ya magharibi. Serikali ya China inatarajia kuipatia gesi ya sehemu ya magharibi soko kubwa kwa mradi huo wa upelekaji wa gesi ili kuchangia maendeleo ya uchumi wa sehemu zote za magharibi zilizoko kando ya mabomba ya upelekaji wa gesi. Wafanyakazi kadhaa wanaotandika mabomba mkoani Xinjiang walipohojiwa na mwandishi wa habari walisema kuwa katika mahali pa kazi aliona kwamba maisha ya wakazi wa huko yameanza kuboreshwa.
Wafanyakazi walimwambia mwandishi wa habari kuwa walipotandika mabomba kwenye Jangwa la Gobi mkoani Xinjiang waliona kuwa maisha ya mzee mfugaji mmoja wa kabila la Wawiur yaliboreshwa kutokana na kuuza chai kwa wafanyakazi hao; Pato la baadhi ya familia za wakazi zenye magari rahisi ya kilimo liliongezeka kutokana na kuwasafirishia vitu vya mahitaji wafanya kazi. Msimamizi mwingine wa ujenzi wa mabomba ya upelekaji gesi, aliyeko mkoani Xinjiang Bw. Shi Yu-hai alimwambia mwandishi wa habari,
"Ili kurahisishia ujenzi wa mradi wa mabomba ya kupelekea gesi, wafanyakazi wa mradi huo walioko Xinjiagn walijenga barabara moja yenye urefu zaidi ya kilomita 600 inayopita sehemu ya ndani ya mlima wa Tianshan ambayo ilipunguza urefu wa safari kwa zaidi ya kilomita 200 kuliko kutumia barabara iliyokuweko hapo awali. Barabara hiyo mpya pia imenufaisha makampuni na migodi ya huko katika usafirishaji. Aidha, sehemu yenye wakazi wachache ambapo vifaa vya ujenzi na vitu vya mahitaji vipatavyo tani makumi kadhaa vinategemea kusafirishwa na magari ya huko kutoka sehemu nyingine, jambo ambalo limeleta ufanisi wa kiuchumi kwa huko."
Habari zinasema kuwa baada ya ujenzi wa mradi huo kukamilishwa, makampuni ya gesi na mabomba ya upelekaji gesi yatatoa kodi nyingi kwa serikali ya huko; mahitaji ya vifaa vya ujenzi ya vituo vya gesi, mabomba na miradi ya uhifadhi wa mito na vitu vya kiutamaduni yatachangia maendeleo ya masoko ya vifaa vya ujenzi; hali kadhalika kwa maendeleo ya mahoteli na mikahawa.
Mtaalamu mmoja wa mambo ya uchumi alisema kuwa kutokana na kujengwa mradi wa upelekaji wa gesi, thamani ya uzalishaji mali wa viwanda vya mkoa wa Xinjiang inaongezeka kwa 25% kwa mwaka na pato la mkoa huo linaongezeka kwa kiasi cha 10%, licha ya hayo, mradi huo umeleta ufanisi wa kiuchumi kwa mikoa na miji mingine inayopitiwa na mabomba ya upelekaji gesi.
Aidha, ujenzi wa mradi wa upelekaji gesi kutoka sehemu ya magharibi hadi sehemu ya mashariki utaboresha mazingira ya asili. Kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya gesi ya asili, wakazi wa sehemu zinazopitiwa na mabomba ya upelekaji gesi, wataweza kuona siku nyingi zenye anga la bluu na mito yenye maji safi. Delta ya mto Changjiang iliyoko katika sehemu ya mwisho ya mradi huo ni sehemu mojawapo miongoni mwa sehemu zilizoendelea kiuchumi nchini China.Viwanda vyenye teknolojia ya kiwango cha juu na wakazi wa sehemu hiyo wanataka sana kutumia niashati safi. Habari zinasema kuwa Shanghai inatumia tani zaidi ya milioni 40 ya makaa ya mawe kwa mwaka, hali ambayo inaleta ongezeko la zaidi ya 10% la mvua nyingi yenye asidi kwa Shanghai na mkoa wa Jiangsu. Kutumika kwa gesi ya asili ya sehemu ya magharibi kutabadilisha mfumo wa matumizi ya nishati ya sehemu hiyo na kuboresha hewa ya sehemu hiyo. Ingawa ujenzi wa mradi huo hivi sasa uko katika hatua ya mwanzo, sehemu nyingi zimeanza kujiandaa zikitarajia ujenzi wa mradi huo wa upelekaji wa gesi ukalimishwe,mapema zaidi ili kuweza kutumia nishati safi, kuboresha mazingira na kukuza uchumi wa sehemu yao.
Kutokana na mpango wa ujenzi wa mradi huo, Shanghai itaweza kutumia gesi ya asili ya Xianjiang tarehe 1 Januari mwakani. Mfanyakazi wa ujenzi wa mradi huo anayefanya kazi katika sehemu ya Shanghai Bwa. Li Shiquan alimwambia mwandishi wa habari kuwa idara husika imesema kuwa itajitahidi kuipatia Shanghai gesi ya asili mapema iwezekanavyo. Alisema, serikali ya Shanghai ilifanya uchunguzi katikati ya mwezi Aprili juu ya kutumika kwa gesi katika siku za baridi mwaka huu. Kampuni ya mfumo wa gesi ya asili ya Shanghai imewatumia barua ikitaka kuleta gesi ya asili katika siku za baridi mwaka huu.
Habari zinasema kuwa sehemu zote zinazopitiwa na mabomba ya upelekaji gesi, ziwe za magharibi au mashariki, zote zimetokewa na mabadiliko makubwa.
Idhaa ya Kiswahili 2004-06-16
|