Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-25 21:03:09    
Picha zinazoshonwa kwa vitambaa

cri

    Bwana Feng Yunshan ni msanii wa vijiji vya jimbo la Shaanxi, ambaye anachonga picha kwenye mbao, kisha kuzichapa katika karatasi. Katika miaka ya karibuni, ameacha kuchora kwa kalamu, karatasi, rangi na kisu, bali ameanza kushughulikia aina mpya ya sanaa?kuboresha picha za vitambaa kwa sindano na gundi. Picha zake hizo zilionyeshwa katika miji ya Beijing, Shanghai, Shenzhen na Guangzhou. Baadhi ya picha zilichapishwa katika magazeti au kuhifadhiwa na majumba ya kumbukumbu na watu binafsi.

    Kusema kweli kushona picha siyo uvumbuzi wake, anaa hii imekuwa ikisanifiwa na akina mama wa vijijini kwa miaka chungu nzima. Bw. Feng mwenye bidii nyingi, alijifunza sanaa hiyo, kisha aliboresha na kuikuza katika ushoni, fani za kumithili na maudhui ya kuonyesha maisha ya wakulima. Picha za vitambaa zilivumbuliwa na akina mama, baada ya kumaliza kushona nguo wakitumia masalio ya vitambaa walishona picha. Rangi za picha za kushona zinang'ara, wahusika wanajitokeza nje, maudhui na fani vinashikamana. Wananchi wa jimboni wanipenda sanaa hiyo, kwani inamudu kuyaonyesha maisha yao vizuri.

    Picha za vitambaa zinatokana na wananchi, kwa hivyo, ujumbe wake huwa juu ya maisha ya wenyeji. Picha za Bw. Feng zinazotia for a ni zifuatazo: 'Jua Kali', 'Wakulima wa Milimani', 'Akina Mama' na 'Jamaa wa Familia Moja'.

    Bw. Feng alizaliwa na kukua vijijini. Hakupata kusoma elimu ya sanaa katika shule maalumu, lakini anacho kipaji cha uanasanaa. Kwa miaka zaidi ya 100 alipofanya kazi na kusomesha shuleni. Akitumia saa za mapumziko alichora michoro mingi ya kuonyesha maisha mazito ya vijijini. Picha zake za vitambaa pia zinadhihirisha upendo wake kwa watani aliyozaliwa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-25