Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-08 14:38:40    
msanii mmoja wa China

cri

    Katika Tianjin, mji wa kaskazini mwa China, kuna mkulima aitwaye Dou Xizhen, ambaye pia ni msanii. Bw. Dou hakupata mafunzo yoyote ya uchoraji wa kitaaluma, lakini amejifundisha mwenyewe. Picha zake zimechanganya umaalumu wa uchoraji wa kichina na kimagharibi, hivyo zinapendwa na Wachina na wageni.

    Bw. Dou Xizhen amezidi umri wa miaka 50, lakini anaonekana kama kijana kutokana na kwamba, yeye ni mzima sana kama chuma cha pua na mwenye sauti kubwa. Alizaliwa vijijini na kukua hapa, tangu utotoni mwake, alikuwa anapenda aina mbalimbali za sanaa za Kichina, kama vile, picha za mwaka mpya, ambazo hubandikwa wakati wa kusherhekea mwaka mpya wa kalenda ya Kichina, vinyago vya udongo wa mfinyanzi, naksi ya ukataji wa karatasi n.k.. Wakati wa mapumziko baada ya shughuli za kilimo, wenzake walikusanya wakipiga gumzo, lakini Bw. Dou alipendelea kuchorachora, akichukua kijiti kimoja, na kuchora kwenye mashamba picha za vitu karibu naye kama vile, milima, mito, ndege na mawingu. Akikumbusha historia hiyo, Bw. Dou anasema, "Wakati ule, nilikuwa sina karatasi wala rangi, nafanyaje? Basi, nakata fimbo ndogo, kuchukulia mashamba yawe karatasi, na fimbo kama kalamu, maumbile ni rafiki yangu, nachora vitu na mandhari ya kimaumbile, nachora kila ninachotizama."

    Siku nenda siku rudi, inakuja majira ya mavuno. Mwanzoni Bw. Dou alichora ovyo ovyo tu, na baadaye alianza kuvutiwa na uchoraji na kufanya mazoezi kwa makusudi. Hatua kwa hatua, uchoraji umekuwa sehemu ya maisha yake. Picha zake zilifuata umaalumu wa picha za Kichina ambazo ni rahisi, za kiasili na zenye rangi nzito. Ingawa hakupata elimu ya uchoraji wa kimagharibi, lakini anafahamu kutumia ustadi wa picha za kimagharibi kwenye uchoraji wake. Na hivyo, akapata mtindo wake mwenyewe.

    Hivi sasa, mkulima huyo anajulikana sana kama mchoraji. Picha zake zimeshinda tuzo mbalimbali katika mashindano ya uchoraji ya nchini China na ya kimataifa. Jina lake limechapishwa kwenye orodha ya wasanii mashuhuri wa sanaa za kiraia za China na vitabu vya shairi, makala na picha za watu mashuhuri, pia alipewa heshima ya msanii hodari wa Kichina ulimwenguni. Katika miaka ya karibuni, Bw. Dou alifaulu mtihani uliandaliwa na wizara husika ya serikali, akawa mchoraji wa ngazi ya kwanza wa taifa. Si kama tu wenzake wa vijijini wanaomba picha zake mara kwa mara, bali pia wageni wamepata habari za mchoraji huyo mkulima.

    Siku moja, Bw. Dou Xizhen alikuwa amemaliza kazi za mashambani na kupumzika nyumbani, alipokea simu kutoka mwandishi wa habari wa shirika la utangazaji la Uingereza BBC, ambaye alimwambia kwamba, wageni wengi alisoma maelezo juu yake kwenye magazeti, wakaona kuwa, ni ajabu kwa mkulima mmoja wa China anaweza kuchora picha nzuri bila elimu ya kitaaluma, kwa hivyo, mwandishi huyo alikuwa na hamu kukutana na Bw. Dou, na kumwalika kwenda ubalozi wa Uingereza mjini Beijing.

    Kwenye ubalozi, maofisa wa Uingereza na mwandishi wa BBC walikutana na Bw. Dou pamoja na picha alizochukua naye, ambapo walipenda sana picha hizo na kushangaa ustadi wake aliopata kwa kujifundisha mwenyewe. Bw. Dou aliwafahamisha, "Sanaa yangu hutokana na vijiji na maisha ya watu wa huko, nikiondoka vijiji na kuacha maisha ya huko, basi sitaweza kuchora picha nzuri."

    Mwezi Octoba, mwaka jana, shule moja ilimwalika Bw. Dou Xizhen kuwa mwalimu wa uchoraji wakati wa mapumziko, vile vile shule ilijenga chumba cha uchoraji kwake, ili awe na mazingira mazuri ya kuendelea na shughuli zake za sanaa. Bw. Dou alieleza kuridhika sana, anasema (sauti 3) "Nipe chumba maalumu cha kushughulikia mambo ya sanaa, sasa nina mazingira nzuri, naweza kujishughulikia kabisa kwenye uchoraji."

    Mbali na kuwa mwalimu wa uchoraji, Bw. Dou anashikilia kuwa yeye ni mkulima. Wakati ambapo kuan shughuli nyingi za kilimo, anakwenda mashambani pamoja na jamaa zake. Mikono yake zinatumia zana za kilimo, lakini pia brashi ya kupakia rangi. Hivi sasa, picha zake zimehifadhiwa na makumbusho mengi huko Hong Kong, Taiwan, Japan, Philipines na Marekani.

    Ardhi ya China imemlea mchoraji huyo mkulima, na kumpa mawazo ya uchoraji. Kila taifa linalokumbwa na matukio muhimu, Bw. Dou anachora picha kwa kumbukumbu. Kwenye picha aliyochora wakati China iliporudisha mamlaka yake huko Macao mwaka 2000, alichora vijana wanaocheza ngoma za dragon na simba, watoto wanaovaa kofia yenye sura ya tiger, mto Changjiang ambao ni mto mkubwa wa kwanza nchini China, maandishi ya Kichina ya neno la furaha pamoja na njiwa mweupe ambao ni ishara ya amani.

    Hivi karibuni, alikamilisha picha moja kubwa yenye urefu wa mita 35, ameipa jina la "furaha ya enzi tukufu". Kwenye picha hiyo ndefu, alichora hadithi zaidi ya 30 ya Kijadi ya Kichina.

 

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-08