Kila mtu akipanda mlima wa Manjano,ataweza kupiga picha nzuri"Mwalimu wangu alisema wakati nilisoma somo la kupiga picha,miaka ya 1960.
September,1997, kwa bahati nzuri nilishamaliza kazi ya kuhoji yangu katika mji wa Tongling, jimboni Anhui, nikipanda basi kufika mlima wa Manjano baada ya safari ya saa tatu .Asubuhi mapema ya siku ya pili, nikipanda gari la utalii la kuning'inia kuelekea kilele cha kotwe Mlima wa Manjano .Mara tu nilipoacha mizigo yangu ndani ya chumba cha Hoteli ya Shilin, nilipanda kilele cha Simba ambacho kipo kaskazini ya hoteli hiyo.
Kilele cha Simba kinaonekana kama simba dume anayesimama kuelekea mashariki katika kiuno chake kumeinuka jabali lenye urefu wa mita 10 na upanda wa mita tatu, nalo linaitwa jukwaa la Baridi.
Nikisimama juu ya jabali hilo niliona vilele vingi vingine ambavyo vinapambwa na mivinje na misonobari yenye maumbo mbalimbali ,majabali yenye maumbo ya ajabu yanayosimama kote milimani na mawinguni yanayozunguka vilele .Katika upande wa kushoto wa jukwaa la baridi kuna tumbili wa jiwe anaangalia bahari ya mawingu,katika upande wa kulia kuna kilele cha Shixin,kilele cha Xiannu na kilele cha Shangsheng vyote hivyo vimekaa kama picha nzuri za kichina ,Kati ya vilele vya Shangsheng na Shixin kuna safu ya majabali ya ajabu na maumbo yao kama waumini wa dini ya Kitao,na miongoni mwao wawili wanacheza sataranji na mmoja akisimama upande wao kuangalia. Nilijongea karibu kidogo niliona daraja moja la jiwe kati ya magenge yanayosimama wima.
Nikifuata kijia kuelekea kushoto nilifika bondeni na kuona stalagmite nyingi kama michipukizi ya mianzi nayo yenye maumbo kem kem.
Nilipanda mita 1,840 juu ya usawa wa bahari kufikia kilele cha mwangaza ambacho ni cha pili kati ya vilele 72 vya Mlima wa Manjano kwa kimo chake,(kilele cha kwanza cha Mayungiyungi chenye mita 1,860 juu ya usawa wa bahari) kituo kikubwa cha kutabiri hali ya hewa katika sehemu ya kusini mashariki ya China kilijengwa hapo. Nilihisi kama kwamba nikisimama katika mawingu ya bahari na vilele vyote vipo chini ya miguu yangu . Kilele cha Mwangaza kipo kati ya sehemu ya utalii ya Mlima wa Manjano na mbele yake kipo kilele cha jade na nyuma yake ni kilele cha Simba.
Nikielekea kusini baada ya kupita bonde refu kuvuka mgongo wa samaki kujipenya ufa wa majabali na kupanda ngazi mia, jumla nilitembea kilomita tatu kwa kutumia saa mbili nikafika mbele ya jengo adhimu ya Jade na Msonobari wa kuwapokea wageni nilihisi nimeingia paradiso
Jengo la Jade liliitwa hekalu la Wen Shu, lipo kwenye mita 1,668 juu ya usawa wa bahari . Inasemekana katika mwaka 1614 mtawa mmoja alikuja hapa kutoka wilaya ya Daixian, jimboni Shanxi alijenga jengo hilo .Watu hunena kuwa usingefika jengo la Jade wakati wa utalii inamaanisha hujafika Mlima wa Manjano .
Mlima wa Manjano mzuri una eneo la kilomita 154 za mraba vilele elfu vikubwa na vidogo ,majabali ya ajabu kem kem mvinje na misonobari yenye umri wa mika elfu kadhaa,zaidi ya hayo mawingu na ukungu hutokea mwaka mzima haswa baada ya kunyesha mvua hutokeza upindi.Kweli ukifika kila maahali utaweza kupiga picha nzuri katika Mlima wa Manjano.
Idhaa ya Kiswahili 2004-07-08
|