Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-09 16:14:54    
Turpan yainua uchumi kwa mambo ya utalii.

cri

 

    Turpan ni sehemu iliyoko mkoani Xinjiang,magharibi mwa China yenye rasimali nyingi za utalii ambayo licha ya kuwa na madhari nzuri ya jagwa, maziwa, milima yenye theluji na miji ya kale, pia ina mila na desturi za kipekee za makabila ya wauygur na wakazak. Katika miaka ya hivi karibuni, Turpan imejitahidi kukuza mambo ya utalii ambayo yamechangia katika kuboresha maisha ya wakazi wa huko.

    Maiguli ni msichana mrembo wa kabila la wauygur. Alisema kuwa kila ifikapo msimu wa utalii, kuna watalii wengi wanaotembelea nyumbani kwao ambapo anawaonesha watalii ngoma za kwao. Mwandishi wa habari alimuliza,

    "Watalii waliotembelea nyumbani kwenu, mara kwa mara wanacheza ngoma pamoja na ninyi?"

    Maguli alimjibu "ndiyo" wageni wakitutembelea, huwa tunacheza ngoma pamoja nao, baba, mama, dada na kaka zangu tunacheza nao pamoja. Turpan ni sehemu inayojulikana hapa nchini kwa uzalishaji wa zabibu. Kila mwaka kuna wageni wanaotoka sehemu mbalimbali duniani kutembelea hapa kwetu, kuonja matunda ya zabibu, zabibu zilizokaushwa pamoja na mvinyo na shughuli ile ijulikanayo kwa "Furaha ya familia za wakulima" inaongeza furaha kwa wageni.

    Maguli alisema kuwa hivi sasa kila mwaka kuna wageni wengi wanaotembelea nyumbani kwao, na familia yao inapata Yuan elfu 30 hadi 40 kwa mwaka.

    Habari zinasema kuwa watalii waliokwenda Turpan kushiriki kwenye utalii wa Furaha ya familia za wakulima mbali na wale waliotoka sehemu nyingine nchini, kulikuwa na wageni kutoka Japani, Marekani, Ujerumani, ufaransa, Itali, Uholanzi na Hispania.

    Furaha ya familia za wakulima, ni njia mojawapo ya kukuza mambo ya utalii na kuongeza pato la wakazi wa sehemu ya Turpan. Turpan inazingatia sana ustawishaji na ufanisi wa matumizi ya rasimali za utalii za huko wakati inapoendeleza mambo ya utalii.

    Turpan ina sehemu nyingi zenye madhari nzuri ya kimaumbile ambazo ni pamoja na Ziwa la Aiding. Ziwa hilo ni sehemu iliyo chini kabisa kwenye ardhi nchini China ambalo liko chini usawa wa bahari kwa mita 154 na pia ni sehemu ya pili kwa kuwa chini sana ya usawa wa bahari humu duniani ikiifuatia DEAD SEA. Sehemu ya ziwa la Aiding pia ni sehemu yenye joto sana nchini China, hali ya joto yake inaweza kufikia nyuzi 47 kwa kipimo cha centigrade. Licha ya hayo huko kuna bonde la mizabibu lenye umbali wa kilomita 7 lenye madhari nzuri na mizabibu mingi. Katika majira ya mavuno ya zabibu, watalii wengi hupenda kutembelea huko na kuonja zabibu.

   Turpan iko kwenye njia ya hariri iliyojulikana sana zamani za kale na imekuwa na sehemu nyingi za kiutamaduni. Mkurugenzi wa shirika la utalii la sehemu ya Turpan Bw Wali Niyaz alisema,

   "Kwa wageni wanafika hapa Turpna, tunapenda sana kuwafahamisha mabaki ya mji wa kale wa Jiaohe ambao ni mji wa kwanza wa kale kwa kuhifadhiwa vizuri ambao ulijengwa zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita na hivi sasa hakuna wakazi. Hivi sasa tumetoa ombi la kuuorodhesha mji huo wa kale kuwa urithi wa dunia. Muda si mrefu uliopita, wataalamu kutoka shirika la elimu, sayansi na utamaduni la umoja wa mataifa UNESCO walifika hapa kufanya uchunguzi, ikaonekana kuwa ombi letu linaelekea kufanikiwa."

   Vitu vingine maarufu vya kiutamaduni vya huko ni pamoja na mnara wenye mtindo pekee wa kiislamu, mji maarufu wa kale wa Ganchang na mapango ya budha pamoja na mila na desturi za makabila madogo madogo.

   Bw Wali alisema kuwa hata katika mwaka 1989, sehemu ya Turpan ilikuwa imebuni sera za kukuza mambo ya utalii na kutunga sera nyingine bora. Baada ya kujitahidi kwa miaka zaidi ya 10, sehemu nyingi za utalii zimeendelea ipasavyo, hatua ambayo imechangia katika maendeleo ya uchumi wa huko. Alisema,

   "Baada ya kuhitaji kwa miaka hiyo iliyopita, mambo ya utalii ya Turpan yalikuwa haraka, mwaka uliopita walipokea watalii zaidi ya milion 1 na laki 5 ambao zaidi ya laki 2 ni wale waliotoka nchi za nje, na pato lao kutokana na utalii lilikuwa zaidi ya Yuan za Renminbi milioni 380, sawa na dola za kimarekani milioni 46 likichukua 5% ya jumla ya thamani ya pato la sehemu hiyo. Hivi sasa, idadi ya watalii inaongezeka kwa 20% kwa mwaka."

   Bw Wali anaona kuwa kutokana na kasi ya maendeleo ya utalii ya hivi sasa, basi itakapofika mwaka 2010 pato kutokana na utalii katika sehemu ya Turpan litaweza kuchukuwa 8% ya jumla ya thamani ya pato lake. Sehemu ya Turpan itakuwa na maendeleo makubwa katika mambo ya utalii, ilimradi iendeleze na kutumia vizuri rasimali za utalii ya huko.

   Habari zinasema kuwa katika siku za baadaye, sehemu ya Turpan itakuza uzalishaji wa bidhaa zenye umaalumu wa kikabila wa huko pamoja na vitu vya kumbukumbu vya utalii. Licha ya kuendelea kuzalisha mazao bora ya zabibu zilizokaushwa, mvinyo na matunda, itazalisha vitu vya kumbukumbu vya utalii vya kiwango cha juu ili kuongeza pato la wakazi wa huko na kuboresha maisha yao.

 

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-09