Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-09 15:47:54    
Wakulima wa mkoa wa Shanxi, China kupata faida ya Yuan za Renminbi milioni mia 9

cri

 

    Mwaka huu, mkoa wa Shanxi ulitekeleza sera mfululizo za kuwafaidisha wakulima. Wakulima wote wa mkoa huo wamepata faida ya moja kwa moja ya Yuan za Renminbi milioni mia 9, kwa kupitia kufutwa kwa kodi za mazao maalum ya kilimo, kupunguzwa kiasi cha kodi za kilimo na kupewa ruzuku ya chakula.

    Mwaka huu, mkoa wa Shanxi umefuta kodi za mazao maalum isipokuwa tumbaku na kiasi cha kodi za kilimo za mkoa huo kimepunguzwa hadi asilimia 6 kutoka asilimia 7. Kutokana na takwimu za mwanzo, kodi za kilimo na za mazao maalum zilizodaiwa kwa wakulima zilipungua kwa Yuan za Renminbi milioni 530 kuliko mwaka jana. Kuanzia mwaka huu, miji miwili ya Yenan na Yulin imeamua kufuta kodi zote za kilimo. wakulima maskini na wakulima waliokumbwa na maafa ya kimaumbile wa miji miwili ya Xian na Xianyang wanafutiwa kodi za kilimo na jumla ya thamani ya kodi za kilimo zilizofutwa katika mkoa huo ni karibu Yuan za Renminbi milioni mia 2.

    Serikali ya mkoa wa Shanxi imeamua kutenga Yuan za Renminbi milioni 150 kutoka mfuko wa ruzuku ya uzalishaji chakula ili kuwapatia ruzuku ya moja kwa moja wakulima wa wilaya 32 zinazozalisha zaidi chakula mkoani humo. Mwaka huu, serikali hiyo pia imetenga Yuan za Renminbi milioni 35 kutokana na mapato ya uuzaji wa ardhi katika kutoa ruzuku ya mifuko ya plastiki ardhini kwa kupanda mahindi katika majira ya spring. Serikali hiyo pia imeweka mfuko maalumu wenye Yuan za Renminbi milioni 8 ambazo zitatumika katika kueneza ufundi wa kupanda mazao kwa mbegu bora. Idara ya fedha ya mji wa Yenan mwaka huu imetenga fedha za Yuan za Renminbi milioni 53 katika ujenzi wa miundo mbinu vijijini.

    Shanxi ni mkoa mkubwa kwa uzalishaji wa nafaka na matunda ya miti. Kufutwa kwa kodi za mazao maalum ya kilimo kumeyawezesha mashamba ya matunda ya miti kuongeza mapato ya Yuan za Renminbi 1,451 kwa hekta na kila familia imepunguziwa kodi za Yuan za Renminbi 200 kuliko mwaka jana. Mwaka huu familia 347 mkoani humo zimefaidika kwa kupewa ruzuku ya nafaka ya moja kwa moja na kila mkulima ameongezewa mapato yenye Yuan za Renminbi 41.2 kwa wastani. Baada ya mji wa Yenan kufuta medani ya kilimo, wakulima wa mji huo wamepunguziwa kodi za Yuan za Renminbi milioni 9 na kila mkulima kupunguzwa kodi za Yuan za Renminbi 58 kwa wastani. Utekelezaji wa sera ya kutoa ruzufu nyingi na kupunguza kodi umehamasisha sana jitihada za wakulima kuzalisha mazao. Kutokana na uchunguzi uliotolewa na idara za kilimo mkoani Shanxi kwa wilaya 32 zinazozalisha matunda ya miti, katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Machi tu, wakulima waliwekeza Yuan za Renminbi 1,144 kwa kila hekta ya mashamba katika kuzalisha zaidi mazao, kiasi ambacho kilizidi sana kile cha miaka iliyopita.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-09