Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-09 17:05:17    
Hariri ya Suzhou

cri

    Wakati vitambaa vya hariri vya China vilipoenezwa hadi Ulaya mnamo karne ya tatu K.K. viliwashangaza sana wafalme na makabaila wa nchi za Magharibi. Wakikabili vitambaa hivyo vya hariri vilivyokaa kama mawingu mazuri walivisifu kuwa vilikuwa kama ndoto moja maridadi.

    Ufunguzi wa "Njia ya Hariri" ya Enzi ya Han, miaka 2,100 iliyopita, ulivifanya vitambaa vya hariri vya China viweze kusafirishwa hadi nchi za Magharibi kwa mfululizo. Majora mengi ya vitambaa hivyo yalifumwa Suzhou na Hangzhou, miji iliyoko pwani ya Kusini Mashariki mwa China. Kutokana na mafanikio hayo Mji wa Suzhou pia huitwa "Mji wa Kale wa Hariri".

    Mpaka leo hii mtalii yeyote anayefika Suzhou, akiondoa kutembelea bustani zake nzuri, huwa na jambo jingine ambalo inambidi afanye, nalo si jingine bali ni kununua vitambaa vya hariri.

    Mji wa Suzhou ulioko kando ya Ziwa Taihu ulikuwa mji mkuu wa Dola la Wu katika Kipindi cha Chunqiu (770 K.K-476 K.K), hali ya hewa ya hapo huwa ni vuguvugu, ardhi yake ni yenye rutuba inayofaa kw kupanda miforosadi na kufuga viwavi vya hariri. Historia ya uzalishaji wake wa vitambaa vya hariri imekuwa na umri wa miaka 3000. Mji huo ulikuwa tayari kituo cha hariri cha China mnamo Enzi ya Song (960-1179) na zilipofika Enzi za Ming na Qing vilitokea vitambaa bora na vizuri vya hariri vya aina moja baada ya nyingine na kuvishinda vitambaa vyingine vingi. Kesi (aina ya ufumaji uliofanywa kwa njia ya tapestry kwa kutumia hariri bora na nyuzi za dhahabu), tarizo, mahameli, shashi na atlasi zote zilijulikana nchini China na ng'ambo. Katika mji wa Suzhou wa leo bado tunaweza kuona magofu ya majengo ya zamani kuhusu ufumaji wa vitambaa vya hariri.

    Katika miaka mingi iliyopita shughuli za ufumaji wa vitambaa vya hariri zimekuwa zikistawi siku zote. Hivi sasa vitamba vya hariri vinavyofumwa kila majuma mawili mjini Suzhou vinaweza kutandikwa kutoka mji wa Chang'an, mwanzo wa "Njia ya Hariri" ya kale hadi Constantinople, kikomo cha njia hiyo. wafanyakazi wanaoshughulikia moja kwa moja ufumaji wa vitambaa vya hariri wamepindukia 50,000. Kwa kufuatia maendeleo ya sayansi na ufundi, ustadi wa jadi umeunganishwa na teknolojia bora ya kisasa, rangi na aina za vitambaa vya hariri na atlasi vinaongezeka kila siku ichayo.

    Vitambaa vizuri vya hariri vya Suzhou vinapendwa sana na kina mama katika masoko ya kimataifa, huuzwa katika nchi 100 na zaidi. Mwanamfalme Charles wa Uingereza na Nancy Reagan waliwahi kuchagua tafeta zilizofumwa huko Suzhou ili kushonea mavazi ya sherehe. Atlasi ya Xiuhua iliyojumlisha hulka za tarizo, ufumaji wa jacquard na mabombwe ya mahameli hupendwa zaidi na wafanyabiashara wa kiarabu. Miaka ya hivi karibuni mavazi ya hariri ya Suzhou yamejulikana zaidi na zaidi na kila mwaka hushonwa 840,000, mengi miongoni mwao huuzwa nchi za nje.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-09