Mkutano wa 15 wa ugonjwa wa ukimwi duniani umefunguliwa leo usiku huko Bangkok, mji mkuu wa Thailend, wawakilishi wa serikali, wanasayansi, madaktari na watu wanaohusika zaidi ya elfu 20 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 160 duniani wamehudhuria mkutaho huo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amehudhuria ufunguzi wa mkutano.
Mkutano huo unatazamiwa kufanyika kwa siku 6, washiriki wa mkutano huo watajadili njia za kinga na tiba ya ukimwi duniani, serikali za nchi kutunga sera kusaidia kinga na tiba ya ukimwi, kulinda haki na maslahi ya wagonjwa wa ukimwi na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ili kudhibiti kwa pamoja maambukizi ya ukimwi. Mkutano huo utafuatilia zaidi jamii inavyowapatia nafasi za kupewa elimu wagonjwa wa ukimwi na watu walioambukizwa viruvi vya ukimwi ili wasaidiwe ipasavyo.
Idhaa ya kiswahili 2004-07-11
|