Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-13 18:38:02    
Mlango wa meli wa mradi wa maji wa Magenge Matatu

cri

 

    Mlango wa meli wa mradi wa maji wa Magenge Matatu, ambao umegharimu Yuan bilioni 6.2, unajulikana kwa "mlango wa meli wenye njia mbili na ngazi tano". Mlango huo wa meli ambao, ulijengwa katika mlima, upande wa kushoto wa ukingo wa bwawa kubwa la Magenge Matatu, ujenzi wake ulianzisha tarehe 17 mwezi Aprili mwaka 1994 na kukamilika baada ya miaka 9. Usafirishaji wa meli ulianza tarehe 16 Juni mwaka 2003 baada ya bwawa kumaliza kulimbikiza maji katika kipindi cha kwanza.

    Mlango wa meli wa Magenge Matatu una urefu wa kilomita 6.4, ambao meli zenye uwezo wa kubeba mizigo zaidi ya tani elfu 10 zinaweza kupita bila matatizo. Kutokana na usanifu wake, mlango huo una uwezo wa kupitisha meli na mizigo tani milioni 50 kwa mwaka. Katika sehemu kuu ya maji ya mlango wa meli, kuna njia mbili ambazo kila moja ina vyumba vitano, na kila chumba kina urefu wa mita 280 na upana wa mita 34.

    Mlango wa meli wa Magenge Matatu ambao unajulikana ni mlango wa kwanza duniani, usanifu wake ulikumbana na matatizo mengi ya kiteknolojia yasiyowahi kuonekana katika ujenzi wa milango ya meli hapo zamani, yakiwa ni pamoja na teknolojia ya udhibiti wa uchimbaji kwenye mteremko mkali, usanifu wa elimu ya nguvu za maji kwenye mlango wa meli wenye kina kirefu cha maji, upangaji wa majengo kwenye mlango wa meli wenye ngazi nyingi, lengo lake kubwa ilikuwa ni kuufanya mlango huo uwe na sura ya mfano wa herufi ya V iliyopinduka pamoja na teknolojia ya kulifungua na kulifunga. Lango hilo la meli ni kubwa sana, upande wake mmoja una upana wa mita 20.2, urefu wa kwenda juu mita 38.5 na unene wa mita 3, pande mbili za lango kwa pamoja zina ukubwa unaolingana na kiwanja cha mchezo wa mpira wa kikapu na uzito wa zaidi ya tani milioni 8.5.

    Wakati wa kujenga mlango huo, wafanyakazi walisawazisha ardhi ya vilele 18 vya mlima na kufungua njia moja kwenye vilima vilivyoko kwenye kando ya kushoto, hali ambayo ni tatizo kubwa lisilowahi kuonekana katika ujenzi wa miradi ya maji duniani. Kina chenye maji mengi zaidi kwenye mlango wa meli ni mita 113, kiasi hiki ni kirefu zaidi ya mita 45 kuliko mlango wa meli uliojengwa na Urusi ya zamani. Meli zinapopita kwenye mlango wa meli wa Magenge Matatu ni kama kupanda ngazi kupita urefu wa kwenda juu ulio kama wa jumba kubwa lenye ghorofa 40.

    Teknolojia iliyotumika katika ujenzi wa mlango wa meli wa Magenge Matatu ni ya kiwango cha juu kabisa duniani. Kina cha maji cha kila chumba cha mlango wa meli ni kiasi cha mita 45.2, na maji yanayopita kwenye chumba cha mlango wa meli ni mita za ujazo elfu 56.7 kwa sekunde, hali hiyo ni mpya kabisa duniani. Kusafiri katika mazingira ya namna hiyo, kunahitaji mlango wa meli kuwa na utulivu mkubwa.

    Kimsingi, usanifu, ujenzi, uzalishaji wa zana zake na ufungaji wa mitambo vyote vilikamilishwa na wachina. Zana zinazohitajiwa na mradi huo ni zenye teknolojia za kiwango cha juu, ambazo usanifu, uzalishaji na uungaji wake vyote vilitegemea viwanda vya nchini china. Jambo hilo limedhihirisha kuwa teknolojia za uzalishaji wa sekta zilizohusika zimefikia kiwango cha juu duniani.

 

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-13