Jua kali, tatizo la kuzirai kutokana na joto jingi na joto kali linalosumbua watu huandamana kwa pamoja. Kujiepusha na tatizo hilo, ni suala ambalo limekuwa likifuatiliwa sana na watu katika majira ya siku za joto. wataalamu wanaona kuwa tatizo la kuzirai kutokana na joto jingi linahusiana sana na halijoto, unyevunyevu wa hewa, upepo, kupigwa na jua kali, pamoja na hali ya afya na lishe. Mbinu mwafaka wa kujiepushana suala hilo ni kama iivuatavyo:
Kwanza, usifanye shughuli kwa muda mrefu katika mazingira ya joto kali. Hususan watu wale wenye ugonjwa wa muda mrefu wa mishipa ya damu ya moyo na ubongo, maini na figo, wasiwe kwenye mazingira yenye joto kali na unyevunyevu mwingi, ili wasije wakazidisha hali ya ugonjwa.
Pili, watu wanaopaswa kufanya kazi katika mazingira ya joto kali, wanatakiwa kunywa maji yenye madini yaa potass, magnesium, maji ya matikiti maji na choroko, ambayo yanawasaidia kuondokana na tatizo hilo.
Aidha, uhai uunaimarishwa kutokana na mazoezi ya mwili. Usikae nyumbani kutwa kucha na kuangalia TV tu, kwani kukosa mazoezi ya mwili kunapunguza kinga ya mwilini dhidi ya maradhi, na kurahisha zaidi kupatwa na tatizo la kuzirai kutokana na joto jingi. Ni dhihiri kwamba usifanye mazoezi ya mwili kupita kiasi kwa ajili ya kupunguza uzito wa mwili. Baadhi ya wanawake wanaogopa kuwa wanene, hupenda kufanya mazoezi makali ya mwili na kujinyima chakula. Kufanya hivyo kunaweza kusababisha upungufu wa ujoto mwilini na kuvuruga uwiano wa lisha. Baadhi ya vitu vinavyohitajiwa sana na mwili pia vitapotea kwa wingi, kusababisha udhaifu wa mwili, kupunguza kinga ya mwili, na kupatwa na tatizo la kuzirai kutokana na joto jingi ambalo litaweza kusabisha uugue ugonjwa mwingine.
Mbali na hayo, uwe na desturi nzuri ya maisha na mazoea ya kuzingatia usafi. Katika majira ya siku za joto, vijidudu vinazaliana kwa haraka, hivyo mboga na matunda yanapaswa kusafishwa vizuri kabla kuyatumia, na usile chakula kilichoharibika. Ujue kwamba gharama utakayotumia kwa kununua madawa ni kubwa zaidi kuliko ya chakula hicho. Ufungue madirisha ya nyumbani na ofisini, usijifungie chumbani au ofisini kwa kutegemea feni na kiyoyozi tu, na wala usilale nje ya nyumba ili kujiepusha na kiharusi.
Idhaa ya Kiswahili 2004-07-14
|