Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-15 18:50:12    
Mkondo wa uhamishaji wa miji mikuu duniani

cri

    Kutokana na sababu za kisiasa, kiuchmi, idadi ya watu, ujenzi wa miji na kadhalika, nchi nyingi duniani zimehamisha mji mkuu kutoka mji mmoja hadi mwingine, au kujenga mji mkuu mwingine kabisa.

    Tangu kumalizika kwa vita vikuu vya pili, nchi zaidi ya 20 duniani zimeshahamisha miji yao mikuu, na nchi nyingine 10 hivi zinapangia kuhamisha mji mkuu.

    Brazil: Kutoka Rio de Janeiro Hadi Brasilia    

    Brazil ni nchi kubwa kabisa katika bara la America ya Kusini, kihistoria, hali ya maendeleo ya kiuchumi ya nchi hiyo haikuwa ya uwiano, sehemu yake ya kusini ni tajiri zaidi kuliko sehemu kaskazini. Mwaka 1822, watu waliwahi kupendekeza kuhamisha mji mkuu kutoka Rio de Janeiro, uliostawi na ulioko kwenye pwani ya kusini hadi bara. Mwaka 1956, serikali ya Brazil iliamua kujenga mji mkuu mpya kwenye pori la Jimbo la Goias, lililoko kwenye sehemu ya magharibi na kati ya nchi hiyo, na kuuita Brasilia. Mwezi Aprili mwaka 1960 mji mkuu wa Brazil ulihamishwa rasmi. Baada ya kuhamishwa mji mkuu, Brazil ilitunga sera ya kustawisha kilimo kwa kutumia sayansi na teknolojia kwenye savana, sera hiyo si kama tu ilibadilisha hali ya kutokuwa na uhusiano wa maendeleo kati ya kaskazini na kusini, pia imehimiza maendeleo kasi ya uchumi nchini kote. Sasa Brasilia umekuwa mji maarufu duniani wenye idadi ya watu zaidi ya milioni mbili.

    Nigeria: Kutoka Lagos hadi Abuja

    Lagos ni mji mkuu wa zamani wa Nigeria, ni bandari kubwa ya kwanza, na kiini cha viwanda nchini Nigeria. Kwa kuwa kijiografia mji wa Lagos uko katika magharibi ya nchi hiyo, hivyo haikuwa rahisi kuwa na mawasiliano na sehemu nyingine , pamoja na idadi yake kubwa kupita kiasi ya watu na ukosefu wa nafasi ya kupanuka, mji huo ulikumbwa na matatizo mengi kama vile mawasiliano na mazingira ya kiafya. Hivyo mwezi Octoba mwaka 1979, serikali ya Nigeria iliidhinisha rasmi muswada wa mpango wa mji mkuu mpya--Abujah. Mji wa Abujah uko katikati ya Nigeria, baada ya ujenzi wa miaka mingi, sasa umekuwa mji mzuri wenye miti mingi na maua mazuri.

    Cote Di'voire: Kutoka Abidjan hadi Yamoussoukro

 

    Abidjan ni moja ya miji inayopendeza na iliyoendelea sana katika nchi za magharibi ya Afrika, mji huu huitwa Paris ya magharibi ya Afrika. Kwa kuwa Abijan ni mji unaozifungulia mlango nchi za nje, hivyo watu wengi kutoka nchi jirani wamemiminikia katika mji huo na kusababisha ukabiliwe na msukosuko wa watu kujazana. Mwezi March mwaka 1983, Cote Di'voire iliamua kuufanya mji wa Yamoussoukro kuwa mji mkuu wa kisiasa, kuhamisha vyombo vya utawala wa serikali kutoka Abidjan hadi Yamoussoukro, na kuuacha Abidjan kuwa mji mkuu wa kiuchumi. Mji wa Yamoussoukro uko umbali wa kilomita 240 kutoka kaskazini ya Abijan, ni mji mkuu wa nne katika historia ya Cote Di'voire.

    Ujerumani: Kutoka Bonn hadi Berlin

    Tarehe 20 mwezi Juni mwaka 1991, Ujerumani iliamua kuhamisha makao makuu ya bunge na serikali kutoka Bonn hadi Berlin. Tarehe 25 Agosti mwaka 1999, chansela wa Ujerumani Gerhard Schrulder alihamia katika ofisi ya muda ya waziri mkuu mjini Berlin. Kwa wajerumani wengi, baada ya kuunganishwa Berlin ni mji mkuu pekee wa kimataifa nchini Ujerumani, ni ishara ya umoja wa kitaifa wa nchi hiyo. Kuhamishwa mji mkuu hadi Berlin kumeifanya Ujerumani kuwa daraja la kuunganisha Ulaya mashariki na Ulaya magharibi. Zaidi ya hayo, kuifanya Berlin kuwa mji mkuu pia kumehimiza maendeleo ya mashariki ya Ujerumani.

    Khazakstan: Kutoka Alamtu hadi Astana

   

    Tarehe 10 Desemba mwaka 1997, rais Nazarbayev wa Khazakstan alitangaza kuufanya mji wa Akmura kuwa mji mkuu wa kudumu wa nchi hiyo badala ya Alamtu. Mwezi May mwaka 1998, mji wa Akmura ulibadilishwa jina kuwa Astana. Mji wa Astana uko kati kati ya nchi hiyo, ulianza kukua kuanzia miaka ya 50 ya karne iliyopita, umekuwa kituo muhimu cha mawasiliano ya barabara na reli katika sehemu ya kaskazini ya Khazakstan. Sababu ya kuhamisha mji mkuu ni kwamba, mji wa Alamtu hauna nafasi ya kutosha kwa mahitaji ya ujenzi wa mji mkuu; hali ya mazingira ya viumbe na uchafuzi wa hewa ni mbaya sana, uko katika mpakani mwa kusini, ni mbali kutoka sehemu za viwanda, tena mji wa Alamtu uko katika ukanda wa tetemeko la ardhi, kwa hiyo hakuna usalama.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-15