daraja la Longnao katika Mto Jiuqu
Daraja la Longnao katika mto Jiuqu, Wilaya ya Luxian, ambalo lipo kusini mwa Jimbo la Sichuan lilijengwa katika utawala wa Mfalme wa Hongwu, Enzi ya Ming (mwaka 1368-1398). Daraja hilo lina urefu wa mita 54 na nguzo 14 kati ya nguzo hizo, nane zilichongwa sanamu za simba, tembo, joka na unicorn wa Kichina, na kila sanamu ina uzito wa tani saba. Wachongaji walichemsha bongo na kuchonga sanamu za wanyama hao wanaoonekana kama wanyama hai. Kwa mfano, kichwa cha joka kilichongwa macho, masikio, pua, ndevu na pembe na kuchongwa magamba mwilini. Mdomoni mwa joka walichonga tufe lenye uzito wa kilo 30 ambalo linaweza kuzungushwa.
Wanakijiji wa kijiji cha Longhua wanalipenda daraja la Longnao kama Mungu wa Ulinzi wao
Daraja hilo lipo kwenye mawe yenye urefu wa mita 3.1 na upana wa mita 0.8. Na kati ya mawe hayo hawakutumia kitu chochote kuyaunganisha isipokuwa yalishikamana yenyewe kutokana na jinsi yalivyochongwa, na hayasogei wala kuteleza.
sanamu za joka kwenye daraja hilo
Nguzo za daraja la Longnao zenye sanamu za simba, tembo, joka na unicorn wa Kichina
Daraja la Longnao liliidhinishwa kuwa daraja la kale la utamaduni wa kitaifa na Baraza la Mawaziri mwaka 1996.
Idhaa ya Kiswahili 20004-07-15
|