Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-16 20:53:31    
Wimbi la wafanyabiashara wa Zhejiang kuwekeza vitega uchumi barani Afrika

cri
    Kwa Muda mrefu uliopita, ushirikiano kati ya China na Afrika umekuwa ukiongezeka siku hadi siku, na kuzidi kuendelezwa katika nyanja mbalimbali na kupata maendeleo makubwa, hasa baada ya kuanzishwa kwa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika.

    China imesaini mikataba ya biashara na nchi zaidi ya 40 barani Afrika, mikataba ya kuhimiza na kuhakikisha uwekezaji na nchi 23 za Afrika, na mikataba ya kutotozana ushuru mara mbili na nchi 8 za Afrika.

    Mpaka sasa, China imeanzisha kampuni 602 katika nchi 49 barani Afrika, na thamani ya vitega uchumi inafikia dola za kimarekani bilioni 1.2. Kampuni hizo zinashughulika na nyanja za biashara, utengenezaji, uendelezaji wa maliasili, mawasiliano na kilimo.

    Kutokana na ongezeko la mawasiliano ya kibiashara kati ya China na Afrika, wachina wengi zaidi hasa wafanyabiashara kutoka mkoa wa Zhe Jiang wanakwenda Afrika kuanzisha kampuni. Hivi sasa, wimbi jipya la kuwekeza vitega uchumi barani Afrika limetokea mkoani Zhe Jiang, China.

    Yiwu ni mji mkubwa wa mkoa wa Zhejiang unaotengeneza na kuuza bidhaa ndogondogo nchini China. Tangu Bw. Zhao Xianwen aanze kuwekeza vitega uchumi nchini Afrika ya Kusini miaka mitatu iliyopita, mamia ya wafanyabiashara kutoka Yiwu walifanya uchunguzi na kuamua kufanya biashara katika nchi mbalimbali za Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, hali hiyo imekuwa ikienea kwenye sehemu zilizoendelea nyingine za mkoa huo kama vile Ningbo na Wenzhou.

    Meneja mkuu wa kampuni ya Huafeng iliyoanzisha soko la bidhaa ndogondogo nchini Afrika ya Kusini Bw. Zhao Xianwen alisema, "Afrika ni sehemu inayovutia wafanyabiashara wengi ulimwenguni. Pia inatoa fursa nzuri ya biashara kwa kampuni za Zhejiang."

    ZheJiang ni mkoa mkubwa wa viwanda vyepesi nchini China, ambapo pia ni mkoa unaouza bidhaa ndogondogo nyingi sana.

    Baadhi ya wachambuzi wa soko wanaona kuwa, hivi sasa utaratibu wa uchumi katika nchi za Afrika unafaidisha uchumi wa Zhejiang. Bidhaa zinazotengenezwa katika mkoa wa Zhejiang zinaweza kulingana na mahitaji ya wanunuzi wa Afrika.

    Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya China imekuwa ikizingatia sana kuendeleza uhusiano wa biashara na Afrika. Ili kuhimiza na kusaidia kampuni za China kufanya biashara na kuanzisha kampuni barani Afrika, idara zinazohusika zimeanzisha vituo vya kuendeleza biashara katika nchi 10 za Afrika zikiwemo Misri, Cameroon, na Nigeria, na kutoa huduma za ushauri wa sera na vitu kwa makampuni.

    Hivi sasa, ujenzi wa kituo cha biashara cha Benin uliandaliwa na mji wa Ningbo mkoani Zhejiang unaendelea vizuri. Baada ya kukamilika kitakuwa na utakuwa kama sura ya bidhaa za Zhejiang katika Afrika Magharibi.

    Mbali na hayo, China imesaini mkataba wa mkopo na nchi 19 barani Afrika. Kutokana na makubaliano hayo, kampuni za China zitakazopata miradi inayofaa katika nchi hizo za Afrika, zitaweza kuomba mkopo huo. Ofisa wa serikali ya mkoa wa Zhejiang alieleza kuwa, idara zake zinazohusika vilevile zinajiandaa kutangaza sera mpya kadhaa, na kutoa misaada mingi zaidi kwa kampuni hizo kuanzisha shughuli katika nchi za nje katika upande wa usimamizi.

    Mkuu wa Kampuni ya Yifa ya mkoa wa Zhejiang inayotengeneza injini Bw. Fang Junming alisema, Afrika ina mazingira mazuri kwa kampuni za nchi za nje kuweka vitega uchumi, pia kunaurafiki mkubwa kati ya China na Afrika, na waafrika ni wakarimu sana kwa wachina. Hii ni sababu muhimu ya sisi kufanya biashara barani Afrika.

    Kampuni ya Yi Fa ya Zhejiang imeamua kutilia mkazo kufanya biashara nchini Nigeria, ili kujitahidi kuingia katika soko la Afrika. Sasa imepata uidhinishaji wa serikali za China na Nigeria, na kujenga kiwanda kipya huko Lagos kwa kutumia dola za kimarekani milioni 2.

    Mkoa wa Zhejiang unahimiza kampuni za huko kuweka vitega uchumi katika nchi za nje. Mkoa huo unaona kuwa, ni kazi nzuri kuendeleza kazi ya kilimo barani Afrika. Afrika ina ardhi kubwa yenye rutuba, wakati hali yake ya hewa ni mwafaka kwa kilimo. Mbali na hayo, serikali za Afrika zimetangaza sera nyingi za kuhimiza kilimo katika nchi zao.

    Tangu mtaalam wa kilimo Bw. Yu Lisheng alipokwenda Afrika mwaka jana, alipanga kuanzisha shughuli za kilimo barani Afrika. Kutokana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya China na Benin, yeye na wenzake watatu walilima shamba la majaribio lenye hekta 15. Madhumuni yao kuonesha mfano kwa wakulima wa huko na kueneza teknolojia ya uzalishaji wa kilimo ya China.

    Baada ya hapo, uzalishaji wa shamba lao ulizidi kwa theluthi kuliko wakulima wa huko. Jambo linalowafurahisha ni kuwa, wenyeji wa huko wanawasifu kutokana na kazi yao na wanawaomba wawafundishe teknolojia yao. Bw. Yu lisheng alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, anatumaini kulima shamba kubwa zaidi karibu na mji mkuu wa Benin baada ya mkataba wa shamba la majaribio kumalizika miaka miwili ijayo, ili kuzalisha mboga kwa soko la Cotonou.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-16