Wataalamu wa Idara ya mipango ya pamoja ya Ukimwi ya Umoja wa Mataifa hivi karibuni walieleza kuwa, kasi ya kuenea kwa Ukimwi haipungui, lakini udhibiti wa kuenea kwa ugonjwa huo na hali ya tiba kwa wagonjwa imepata maendeleo kiasi.
Naibu mtendaji wa Idara hiyo ya Umoja wa Mataifa alieleza kuwa, tangu mkutano wa 14 wa Ukimwi duniani uliofanyika mwezi Julai, mwaka 2002, huko Bacelona, nchini Hispania, watu milioni 9 waliambukizwa virusi vya Ukimwi, Kati yao zaidi ya milioni 5 walikufa kutokana na ugonjwa huo. Takwimu mpya inaonesha kuwa, kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi, na kuimarisha tiba ya ugonjwa huo ni changamoto kubwa inayowakabili binadamu duniani.
Idara ya mipango ya pamoja ya Ukimwi ya Umoja wa Mataifa tarehe 6, Julai, ilitoa ripoti kuhusu hali ya ugonjwa wa Ukimwi duniani ya mwaka 2004 ikieleza kuwa, hivi sasa, watu milioni 38 wameambukizwa virusi vya Ukimwi duniani, na watu milioni 2.9 walikufa kutokana na Ukimwi mwaka 2003. Idara hiyo inataka serikali za nchi zote kuzingatia kudhibiti kasi ya kuenea kwa Ukimwi, na kuchukua mbaya zaidi.
Katika sehemu za Afrika zilizoko kusini mwa Sahara ambapo Ukimwi unaenea sana, ugonjwa huo si kama tu unaenea kati ya watu wanaotumia dawa za kulevya na watu wanaojamiiana kwa njia zisizo salama, bali pia unaenea kati ya watu wa kawaida. Mwaka 2003, watu milioni 3 waliambukizwa virusi vya Ukimwi, na milioni 2.2 kati yao walikufa. Idadi ya watu wa sehemu za Afrika zilizoko kusini mwa Sahara ni asilimia 10 ya watu wote duniani, lakini watu milioni 25 kwenye sehemu hiyo waliambukizwa Ukimwi. Idadi hiyo inachukua asilimia 70 kwa watu wote walioamzukiwa Ukimwi diniani. Katika sehemu hiyo, idadi ya watu wameambukizwa Ukimwi ni zaidi ya asilimia 17 katika nchi 7, na inazidi asilimia 35 katika nchi nyingine kadhaa.
Ripoti hiyo inasema kuwa, sasa ni wakati muhimu sana kwa Bara la Asia lenye idadi kubwa ya watu kudhibiti kasi ya kuenea kwa Ukimwi. Kwa upande mmoja, watu walioambukizwa Ukimwi katika nchi nyingi za Asia hawazidi asilimia 1. Kwa upande mwingine, Ukimwi unaenea kwa kasi sana barani Asia, robo ya watu wanaoambukizwa Ukmwi ni kutoka Asia. Mwaka 2003, watu milioni 1.1 waliambukizwa Ukimwi barani Asia, na zaidi ya laki 5 walikufa kutokana na ugonjwa huo. Hivi sasa, Asia ina watu walioambukizwa Ukimwi milioni 7.4.
Mbali na hayo, hakuna dalili yoyote ianyoonesha kuwa, kasi ya kuenea kwa Ukimwi inapungua katika sehemu ya mashariki ya kati, Afrika Kaskazini na Ulaya Mashariki. Katika nchi zilizoendelea za Ulaya na Marekani, vifo vya wagonjwa wa Ukimwi vinapungua kwa kiasi kikubwa kutokana na mbinu mpya za tiba. Watu wanaoambukizwa Ukimwi wanaongezeka katika nchi hizo kutokana na kutozingatia hatari ya ugonjwa huo.
Mkutano wa 15 wa Ukimwi duniani ulifanyika kufanyika kuanzia tarehe 11 hadi 16, Julai, huko Bangkok, mji mkuu wa Thailand, wajumbe wapatao elfu 17 wakiwemo maofisa wa serikali, wanasayansi na watu wanaoshughulikia kazi ya tiba na jamii kutoka nchi na sehemu 160 walihudhuria mkutano huo.
Idhaa ya kiswahili 2004-07-16
|