Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-21 17:39:31    
AIDS (UKIMWI) 12

cri
    Mgonjwa wa UKIMWI eti anaweza akaacha viini vya ugonjwa wake kwenye viti vya chooni (toilets) na kusababisha watu wengine waupate?

    Anaweza kuacha viini humo endapo tu atakuwa anatokwa na damu au majimaji yatakayodondokea kwenye viti hivyo. Lakini hata kama jambo hilo litatokea, si rahisi kwa viini hivyo kuweza kuambukiza watu wengine kwani itabidi mtu atakayekalia viti hivyo awe naye anavyo vidonda au majeraha katika sehemu zake za mwili zitakazogusana na viti hivyo. Isitoshe itabidi pia huyo atakayegusa viti hivyo awahi mapema kufanya hivyo viini hivyo vikiwa vingali hai. Hili nalo sio jambo ambalo ni rahisi kutokea katika ukamilifu huo na kwa hiyo uambukizaji wa UKIMWI (AIDS) kwa njia ya toilets sio jambo la kawaida.

    Nimesikia kamba michezo ya mapenzi na watu wenye UKIMWI yaweza pia kuwa ni hatari, je! Ni kweli?

    Njia za kawaida za kuonyeshana ishara ya upendo kama vile kushikana mikono, kukumbatiana, n.k. hazina madhara yoyote. Lakini zile njia za kufisadi za kuonyeshana mapenzi kama vile kunyonyana ndimi; kunyonyana chuchu za ziwa; au kunyonyana via vya uzazi n.k. zinaweza kueneza sio UKIMWI tu peke yake bali na magonjwa mengine ya siri.

    Je, kushirikiana na mtu mwenye UKIMWI kunaruhusiwa au haukuruhusiwi?

    Kunaruhusiwa sana mradi tu ushirikiano wenyewe usiruke mipaka fulanifulani. Imethibitishwa kwamba uhusiano wa kawaida hauna hatari. Kwa mfano huko Marekani watu wengi ambao wameishi kwa muda mrefu nyumbani na jamaa zao wenye UKIMWI wameonekana kamba hawakuhahi kuambukizwa ugonjwa huo; lakini pamoja na hayo wamekuwa wakichukua tahadhari zinazofaa.

    Ijapokuwa viini vya UKIMWI vimewahi kuonekana onekana kwenye mate, machozi na majimaji mengine yanayowatoka wenye UKIMWI, lakini mpaka sasa hakuna ushahidi unaothibitisha kwamba ugonjwa huu huenezwa kwa kukohoa; ama kwa kupia chafya; ama kwa kupeana mikono. Huwezi kuokota UKIMWI kwenye viti; au kwenye mikono ya milanog; au kwenye sahani za kulia; au kwenye bilauri za kunywea; au kwenye nguo za kuvaa; au kwenye vitabu na magazeti n.k.

    Ushirikianao ambao unaleta hatari ni ule wa kujuana kimwili au ule wa kujuana kimwili au ule unaoruhusu damu na majimaji yanayomtoka mgonjwa yaingie moja kwa moja mwilini mwako ama kwa njia ya sindano; ama kwa njia ya vijeraha n.k.

    Kwa vyovyote ni lazima kuchukua tahadhari fulani fulani wakati wa kudumisha ushirikiano wa kawaida wa aina yoyote na mtu mwenye UKIMWI.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-21