Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-22 18:23:56    
Bara la Afrika kuelekea Pan Afrika mpya

cri

    Kuanzia Umoja wa nchi huru za kiafrika hadi Umoja wa Afrika, maendeleo ya Bara la Afrika siku zote yanaambatana na utafutaji wa Pan Afrika. Mkutano wa 3 wa wakuu wa Umoja wa Afrika uliofungwa tarehe 8 Julai huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia umeonesha kuwa, mawazo kuhusu maendeleo ya Afrika pia yanabadilika kutokana na wakati, ambapo wazo la Pan Afrika limekuwa fikra ya uelekezaji kwa aina mpya na maana mpya kwa nchi za Afrika kutafuta mshikamano, kuhimiza muungano na kujipatia maendeleo.

    Waraka uliopitishwa kwenye mkutano kuhusu "Matarajio ya Umoja wa Afrika na majukumu ya Kamati ya Umoja wa Afrika" unaona kuwa, wazo la Pan Afrika linapaswa kulingana na mabadiliko ya hali ya mambo, lingechukua kazi ya kuhimiza maendeleo ya uchumi kuwa mwendelezo wa juhudi za ukombozi wa kisiasa, kukabiliana kimkakati na utandawazi wa uchumi wa kikanda, kufanya ushirikiano wa kikanda ili kuuwezesha uchumi wa Afrika ubadilishe aina yake, na unapoimarisha majukumu ya serikali, lazima kuhamasisha watu katika jamii nzima kushiriki kwa juhudi katika maendeleo ya uchumi.

    Wazo la Pan Afrika lilianza tangu zamani. Baada ya miaka ya 50 ya karne iliyopita, wazo hilo lilihusishwa zaidi na harakati za ukombozi zilizofanyika katika hali ya motomoto, na liliendelea haraka na kuwa wazo la pamoja kwa Bara la Afrika. Ingawa maelezo ya kila nchi kuhusu wazo hilo yanatofautiana, lakini lengo lao la msingi ni moja, yaani nchi za Afrika zinataka kuimarisha mshikamano kati ya nchi za Afrika, kuung'oa ukoloni, kulinda uhuru wa mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi za nchi za Afrika.

    Wazo la jadi kuhusu Pan Afrika pia lilisisitiza kuendeleza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi, lakini huo haukuwa mwelekeo wa uelekezaji wa Umoja wa OAU. Kwa upande mmoja OAU ilitilia mkazo kwanza juhudi za kujipatia uhuru wa kisiasa wa nchi za Afrika ambao ulikuwa wa dharura zaidi, na kwa upande mwingine, wakati huo ulikosa mpango wa kimkakati kuhusu ushirikiano wa kiuchumi, hivyo ulikosa ushirikiano halisi kivitendo.

    Kadiri utandawazi wa uchumi duniani ulivyoendelea haraka, ndivyo maendeleo ya Afrika yalivyoonekana kuwa ya nyuma zaidi, ambapo yanakabiliwa na hatari ya kuwekwa pembezoni. Nchi za Afrika zimetambua kuwa, jukumu kubwa lenye taabu zaidi limewekwa mbele ya nchi mbalimbali za Afrika. Mwezi Julai mwaka 2002, mkutano wa kwanza wa wakuu uliofanikiwa kufanyika huko Durban, Afrika ya kusini ulionesha kuwa jukumu la kihistoria la OAU lilikamilika, na watu wameanza kufikiri upya maisha na mustakbali wa bara la Afrika.

    Kutokana na wazo la jadi la Pan Afrika, Bara la Afrika limepata ukombozi, lakini kwa kukabiliwa na hali ya umaskini, na maendeleo yaliyoko nyuma, maana ya ukombozi huo bado haijakamilika. Katika miaka miwili iliyopita, Umoja wa Afrika umetambua kuwa, alama ya mshikamano na muungano wa Afrika lazima ioenekane katika maendeleo halisi ya uchumi kwenye msingi wa utandawazi wa kikanda.

    Mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika ulipitisha nyaraka tatu ambazo zimeweka majukumu ya Umoja wa Afrika katika miaka mitatu ijayo, pia kubuni mipango ya Bara la Afrika katika sekta mbalimbali kuanzia sasa hadi mwaka 2030, na kusisitiza kuondoa umaskini, kuendeleza uchumi na kuwapatia faida halisi wananchi wa nchi mbalimbali.

     Rais Joachim Chissano wa Msumbiji alipotoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika alifahamisha umuhimu wa Pan Afrika mpya akisema kuwa, maendeleo ya Bara la Afrika yanategemea siku zake za usoni.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-22