Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-29 18:38:05    
Michoro ya rangi ya maji

cri

    Michoro ya rangi ya maji nchini China ilitoka Ulaya karibu miaka 100 iliyopita. Katika kipindi kirefu, michoro hiyo ambayo ni aina ndogo ya sanaa ya uchoraji haikuwa na wachoraji maarufu. Miaka ya karibuni kwa sababu ya mageuzi na mlango wazi, watu wanapanua shauku zao, na hivyo homa ya michoro ya rangi ya maji imetokea polepole. Maonyesho ya 6 ya sanaa ya taifa ya mwaka 1984 na maonyesho ya 7 ya mwaka 1989 yalikuwa na sehemu yake pekee ya michoro ya rangi ya maji. Michoro ya aina hiyo ya wasanii wa China pia imekwenda nchi za nje na kusifiwa huko Japani, Marekani na nchi za Ulaya Kaskazini. Kutokana na maoni ya wasanii mbalimbali duniani kuhusu sanaa hiyo, kulizuka mijadala ya namna ya kuchora michoro hiyo. kwa kawaida, michoro ya rangi ya maji huchorwa kwa kufuata vitu vilivyo, yaani vitu vya asili, lakini wameondoa dhana hiyo. yaani, mchoraji hajali asili ya vitu, bali anaweza kuongeza mawazo yake na hisia kwenye michoro. Ukombozi huo wa dhana umepanua uchoraji wa michoro ya rangi ya maji.

    Mwaka 1992, maonyesho ya pili ya michoro ya rangi ya maji ya taifa yalifanywa Xuzhou jimboni Jiangsu. Watu wanaona kuwa maonyesho hayo yana maendeleo mapya. 

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-29