Ni hatua gani zinazofaa kuchukuliwa wakati wa kuandaa ama kumtayarisha kwa mazishi mtu aliyekufa kwa ugonjwa wa UKIMWI?
Wanaohusika kumwosha au kumvalisha maiti nguo yawapasa kutimiza baadhi ya mambo yafuatayo:
1. wasiwe wana vijeraha vyovyote mikononi mwao.
2. wajihadhari kuingiwa na damu au majimaji yatakayokuwa yanamtoka marehemu.
3. wavae mipira mikononi endapo itabidi washikeshike kitu chochote kitakachomtoka marehemu.
4. baada ya kumwosha wafunge vijeraha vitakavyokuwepo mwilini na wazibe pua, mdomo, tupu ya nyuma na ya mbele kwa kutumia pamba ama kitu kingine chochote cha kuzuia damu au majimaji yatakayoweza kuendelea kutoka baadaye kabla ya mazishi.
5. maji yaliyotumika kumwosha maiti pamoja na uchafu mwingine uliotoka?hivi vyote vifukiwe chini ardhini.
6. mahali palipotumika kumwoshea maiti pasafishwe na kama itawezekana panyunyiziwe dawa ya kuua viini vya ugonjwa.
7. waliohusika na kazi hiyo ya kumtayarisha maiti waoge na kubadili nguo zao.
8. nguo zilizotumika kufanya kazi ya kumwosha maiti zichemshwe kabla ya kufuliwa.
9. baada ya mazishi jeneza lisafishwe kwa sabuni au maji moto.
10. endapo itaonekana kwamba ni vigumu kutekeleza haya yote huko nyumbani, basi ni afadhali maiti ikabidhiwe hospitali kwa mazishi au ikabidhiwe watu wenye utaalam kwa kusudi hilo.
Hapa kwetu ugonjwa huu umeenea kiasi gani na kwa kina nani zaidi?
Kila mkoa umeshakumbwa; wagonjwa wako mijini na vijijini, lakini waliokumbwa zaidi na ugonjwa huu ni wale wenye tabia za uasherati?hasa vijana wenye umri wa miaka 15-35.
Ikiwa imeonekana kwamba damu wanazopewa watu hospitalini huweza kueneza ugonjwa wa UKIMWI, mbona jambo hilo lisipigwe marufuku?
Damu ni kitu kinachookoa maisha ya mtu. Kwa hiyo katika jambo la kufa na kupona, ni afadhali kuponyesha maisha kwanza, halafu hayo mengine yatakayotokea baadaye yachunguzwe na ikiwezekana yarekebishwe. Hata hivyo wale wenye kutoa damu ni lazima wawe watu ambao inaaminika kwamba hawana ugonjwa wa UKIMWI.
Idhaa ya Kiswahili 2004-07-29
|