Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-30 19:52:20    
Kuchonga nakshi kwa kompyuta

cri

  

  

    Taasisi ya Kompyuta ya Kweupe, Mji wa Changsha, Jimbo la Hunan, ilivumbua mashine ya kuchonga nakshi kwa kompyuta kwenye nyenzo ngumu kama mawe, chuma na kadhalika. Wakati habari hiyo ilipoenea, wasanifu wengi walishindana kwenda kujionea wenyewe.

    Baadhi ya wasanifu walifanya majaribio. Waliandika maneno ya pongezi na kuyachonga kwenye mawe ya aina mbili. Ingawa maneno fulani yalikuzwa mara kadhaa, lakini sifa za awali hazikupungua hata kidogo.

    Katika chumba cha maonyesho cha taasisi hiyo kuna michongo mizuri mingi iliyochongwa kwenye mawe, chuma cha pua kisichoingiwa na kutu, mianzi, vioo na ganda la yai la mbuni. Kivutio cha michongo hiyo ni michoro maarufu "Malaika87" wa Enzi ya Song wenye urefu wa mita 8 na kimo cha mita 1. Mchoro huo ambao ulikuzwa ukubwa mara 10, ulichongwa kwenye pandikizi la jiwe jeusi kwa mistari ya dhahabu. Malaika 87 wanaokwenda machi wote wanaonekana kama wa hai, wakitazama mbele au wakiwaza pindo za mavazi zinapepea kwa jinsi ya madaha ya kuvutia macho. Baada ya kukuzwa ukubwa, mchongo huo si tu ulibakia na sifa ya awali, bali pia uliongezwa usanifu wa hali ya juu.

    Bwana Zhang Yiming, Mkurugenzi wa taasisi ana mpango wa kujenga mji au bustani ya michongo ya mawe, ambayo itaonyesha michoro maarufu ya kale na maandiko ya riwaya nne mashuhuri za kale. Maadiko hayo yataambatanishwa na mamia ya picha za wahusika wa riwaya hizo. Anataka kuviachia vizazi vijavyo urithi wa utamaduni.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-30