Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-03 13:47:32    
Wanaviwanda binafsi wanatarajia kupata mafanikio makubwa

cri
Mkoa wa Zhejinag, ambao uko katika pwani ya mashariki ya China, ni moja ya mikoa tajiri nchini China. Tangu kutekelezwa sera za mageuzi, uchumi wa mkoa huo ulikuwa na ongezeko la kasi, hususan viwanda binafsi vya mkoa huo vimepata maendeleo makubwa. Lakini kadiri soko la China linavyozidi kufunguliwa kwa nje, viwanda hivyo binafsi vimekabiliwa na shinikizo kubwa la ushindani. Ili kubadilisha hali ya namna hiyo, hivi sasa wanaviwanda binafsi wa mkoa wa Zhejiang wanajitahidi kuboresha mfumo wa usimamizi wa viwanda ili kuongeza nguvu zake za ushindani na kupata mafanikio mapya.

Tukitupia macho historia za baadhi ya wanaviwanda wa Zhejiang, tutaona kuwa kabla yao kufanikiwa, walikuwa watu wa kawaida tu, kama wakulima, wafanyakazi wa kawaida na mafundi. Wakati ule walipungukiwa mitaji, kukosa uzoefu wa usimamizi ila tu kujitegemea na kupiga hatua kutoka mwanzo. Lakini hali ya unyonge haikuathiri ari yao ya kuinuka kutoka tabaka la "mizizi ya majani" na kuelekea kwenye mafanikio. Katika miaka ya karibuni, kulikuwako wataalamu na wasomi wengi ambao walijitahidi kuchunguza "siri" ya kutajirika kwa wanaviwanda binafsi. Baadhi ya watu wanaona kuwa wakazi wa Zhejiang wana tabia nzuri ya kujinyima kwa matumizi mengi yasiyo ya lazima, bidii za kazi na kipaji cha biashara. Sifa zao hizo zimewawezesha kupata mafanikio katika uwanja wa biashara.

Wanaviwanda wa Zhejiang hupenda kusema kuwa mafaniko wanayoyapata, yanatokana na sera za mageuzi na ufunguaji mlango zilizoanza kutekelezwa nchini China toka mwishoni mwa miaka ya 70. Sera hizo zilibuniwa kwa kusudi la kukuanzisha uchumi wa soko huria na kuongeza pato la wananchi. Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya lifti ya Xizi, mjini Hangzhou, mkoani humo Bw. Wang Yongfu alisema kuwa sera za mageuzi ziliwapatia fursa ya kutajirika.

"Mwanzoni, hatukuwa na tarajio kubwa, kwani wakati ule tungefurahi sana kama tungeweza kuacha kazi za shambani na kwenda nje kujishughulisha kwa kazi za viwanda. Mchakato wa maendeleo pia ni fursa, sisi tumewahi, endapo mageuzi yalifanyika mapema zaidi, tusingeweza kukamata fursa hiyo, kwa kuwa tungali kuwa watoto; endapo yangecheleza zaidi, sisi tungezeeka. Hii ni fursa nzuri ambayo tumeipata kwa bahari nzuri, sisi tumekamata fursa hiyo."

Bwana Wang ana hoja nyingi za kuthibitisha maoni yake. Katika mwisho wa miaka ya 70 ya karne iliyopita, Bw. Wang alianzisha kiwanda cha mitambo ya kilimo katika kitongoji cha mji wa Hangchou, mji mkuu wa mkoa wa Zhejiang na kuzalisha vipuri vya trakta. Haraka aliona kuwa lifti zitahitajiwa kwa wingi, hivyo alijenga kiwanda cha lifti akishirikiana na wafanya biashara wengine. Hivi sasa, thamani ya uzalishaji mali wa kiwanda hicho imezidi Yuan bilioni 2.

Kusema kweli, uwanja wa biashara ni kama uwanja wa vita, ukitaka kupata ushindi, huna budi kuwa na moyo wa ujasili na uvumbuzi. Hiyo ni sababu muhimu ya kufanikiwa kwa wafanya biashara wa Zhejiang. Mkurugenzi wa kampuni ya Aokang iliyoko katika mji wa Wenzhou, mkoani Zhejiang ni mfanya biashara mwenye moyo wa ujasiri, ambaye alianzisha kiwanda cha viatu zaidi ya miaka 20 iliyopita, hivi sasa kiwanda chake kinachukua nafasi ya tatu katika sekta ya uzaliishaji wa viatu nchini China. Lakini, hakuridhika na hali bora aliyokuwa nayo, katika miaka michache iliyopita, alitenga fedha nyingi kwa kuanzisha duka la viatu vya kampuni yake

"Sasa imetimiza miaka miwili tangu nilipofungua duka la viatu katika nchi za nje. Mwaka 2001, nilichagua Paris kufungua duka, miji niliyochagua yote ni mikubwa ma maarufu duniani, kama vile, Milan, Romme, Naples, New York ya Marekani na Baselona ya Hispania, hadi hivi sasa nimefungua maduka katika zaidi ya nchi kumi.. mwaka huu, ninanuia kufungua maduka katika Marekani ya kaskazini. Lengo langu ni kufanya bidhaa maarufu za China kuuzwa katika nchi mbalimbali duniani."

Hadi mwishoni mwa mwezi Juni mwaka 2003, uchumi binafsi mkoani Zhejiang umechukua 53% ya pato la mkoa huo mzima. Kati ya viwanda zaidi ya laki 3.5 vya mkoa Zhejiang, kiasi cha 80% ni viwanda visivyo vya kiserikali au vya utaratibu wa hisa. Hata hivyo, viwanda binafsi vya mkoa Zhejiang bado viko mbali na viwanda vikuwa vya China na vya nchi za nje, kwa kuwa viwanda hivyo bado ni vidogo na vya ukoo, na bado kuna upungufu katika maandalizi ya mafundi, teknolojia na utaratibu. Hivi sasa, wanaviwanda wa Zhejiang wanafanya ujasiri mkubwa katika kuboresha utaratibu wa viwanda. Katika kipindi kilichoita, viwanda 9 maarufu binafsi vilianzisha kampuni moja kubwa ya utaratibu wa hisa, ambayo mitaji inayoweza kutumika imezidi Yuan bilioni 10.

Haibu mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Wang Zhentao ni kiongozi wa kiwanda kikubwa cha viatu. Alipohijiwa na mwandishi wetu wa habari alisema kuwa kuanzisha kampuni hiyo ya utaratibu wa hisa ni kukabili ushindaji wa soko huria katika siku za mbele.

"Kwa kukabili ushindani wa nchini na duniani baada ya China kujiunga na WTO, viwanda vyetu vinafi vinatakiwa kuungana na kuanzisha kampuni moja kubwa, huu ni mwelekeo wa maendeleo ya viwanda vinafsi katika siku za baadaye."

Habari zinasema kuwa licha ya kuungana pamoja, viwanda vingi vinafsi vya mkoa Zhejiang vinajitahidi kushirikiana na viwanda vikubwa vya kimataifa na kuingiza uzimamizi na teknolojia ya kimaendeleo ya nchi za nje.

Idhaa ya kiswahili 2004-08-03