Nitawatambuaje wenye MAHABUSI (AIDS) ili nijiepushe nao?
Si rahisi kumtambua mtu mwenye MAHABUSI kwa sababu dalili za ugonjwa zinahitilafiana kufuatana na ugonjwa uliomnyemelea baada ya kuburugika kwa baadhi ya silaha zake za kujihami. Kwa mfano mtu mwenye MAHABUSI Baridi hataonyesha dalili zozote; na mtu mwenye MAHABUSI Moto ambaye amenyemelewa na viini vya ugonjwa wa kifua ataonyesha dalili za magonjwa ya kifua kama vile kichomi, kukohoa, kutokwa na jasho usiku n.k.
Lakini kuna dalili fulanifulani ambazo mara kwa mara huonekana kwa wale wenye MAHABUSI Moto au Vuguvugu. Baadhi ya dalili hizo ni:
1. Unyong'onyevu na uchovu usio na sababu maalum
2. Kuvimba tezi shingoni, kwapani na kinenani
3. Kukonda
4. Homa ya muda mrefu
5. Kuendesha endesha kwa muda mrefu
6. Utando mweupe kinywani, vidonda mdomoni, na vidonda kooni vyenye kusababisha maumivu wakati wa kumeza.
7. Ukurutu katika ngozi
8. Kuburugika akili
9. Kupungukiwa na damu.
Baadhi ya dalili kama hizo zinapoonekana kwa mtu ambaye haonyeshi kisa halisi cha ugonjwa unaozisababisha, basi anza kuwa mwangalifu zaidi kuhusu ushirikiano wa karibu sana naye ambao utaruhusu kugusana na vitu vitakavyokuwa vinamtoka?zaidi sana endapo mtu mwenye dalili hizo atakuwa ni yule aliye kwenye kundi la watu mashuhuri kwa ugonjwa huu.
Idhaa ya Kiswahili 2004-08-04
|