Mradi wa kupeleka gesi ya asili kutoka sehemu ya magharibi kwenda sehemu ya mashariki ya China ni mradi mkubwa wa ujenzi wa miundo mbinu katika mpango wa kumi wa maendeleo ya miaka mitano kuanzia mwaka 2001 hadi mwaka 2005. Mradi huo wenye urefu wa kilomita 4,000, unapita sehemu mbalimbali zikiwa ni pamoja na mito, maziwa na jangwa. Gesi inayoletwa kutoka sehemu ya magharibi itatumika kuzalisha umeme, katika viwanda vya kemikali, kwa nishati ya viwanda na wakazi wa mijini.
Wataalamu husika wamekadiria kuwa hadi mwaka 2005, mahitaji katika kuzalisha umeme, viwanda vya kemikali na nishati ya viwanda na wakazi yatachukua 47%, 9.8%, 17.4% na 25.8% kwa kufuatana.
Katika sehemu ya delta ya mto Changjiang, gesi ya asili hasa inatumika katika viwanda vya umeme vya Jinshan, Caojing, Zhejiang, Wangting na Zhenhai vya Jiangsu, na kiwanda cha ammonia cha Wujing. Bei ya gesi hiyo ni chini ya Yuan 1.45 kwa mita za ujazo inayotumika hivi sasa mjini Shanghai, ambayo inaletwa kutoka bahari ya mashariki na kuwa chini ya bei ya Yuan 1.6 kwa mita za ujazo inayoletwa kutoka nchi za nje, hivyo itakuwa na soko kubwa katika sehemu ya mashariki ya China.
Sehemu ya delta ya mto Changjiang ni sehemu yenye nguvu kiuchumi na yenye ongezeko kubwa la uchumi hapa nchini. Sehemu hiyo ina upungufu wa rasilimali za nishati, inahitaji nishati kwa wingi, ambazo zinaletwa kutoka sehemu nyingine. Pamoja na uendelezaji wa hifadhi ya mazingira ya asili, sehemu hiyo inahitaji nishati safi isiyo na uchafuzi.
Kwa kuwa mradi huo unapita sehemu zenye mito, maziwa na jangwa, ambazo ni zenye matatizo kwa ujenzi wa mradi, hivyo ubora wake umekuwa ukifuatiliwa na pande mbalimbali.
Kiongozi wa kampuni ya mabomba ya mradi wa kupeleka gesi kutoka sehemu ya magharibi kwenda sehemu ya mashariki, alisema kuwa suala la ubora wa mradi ni suala muhimu la kwanza linalozingatiwa na wajenzi wa mradi huo. Katika suala hilo, kampuni ya mabomba ya China imetumia kigezo kipya cha juu duniani ambacho kina sifa maalumu kama zifuatazo. Ya kwanza, unafuatwa usimamizi wa pamoja wa China na nchi ya nje, kutokana na zabuni iliyotangazwa, kampuni ya Global ya Marekani ilichaguliwa kufanya usimamizi kwa kushirikiana na kampuni ya usimamizi ya nchini. Pili, kufuata utaratibu wa kutoa zabuni katika ujenzi wote wa mradi. Tatu, kufuata utaratibu wa kandarasi, ambao ni njia inayotumika sana nchini kwa kufuata desturi ya duniani, hususan katika mikataba ya kazi, kuna vifungu vinavyohusu kufidia na kufidiwa. Nne, usimamizi wa mtoa zabuni. Mtoa zabuni anazingatia zaidi udhibiti na usawazishaji wa mipango ya ujenzi wa mradi, ambapo kazi nyingine ndogo ndogo zikiwemo uendeshaji wa mchakato zinamalizwa na wakala au wafanyabiashara wa kandarasi.
|