Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-13 20:17:17    
China yajenga ukanda wa misitu kwenye barabara ndefu zaidi ya jangwa duniani

cri

    Miongoni mwa vilima vya mchanga vinavyohamahama barabara moja inanyooka bila kupinda, misitu ya kuzuia upepo na uhamiaji wa mchanga iliyopandwa pembeni mwa barabara hiyo imestawi vizuri, inaonekana kama utepe wa majani unaopeperuka kwenye jangwa kubwa la Taklamagan.

    Jangwa la Taklamagan huitwa "bahari ya kifo". Barabara inayopita katika "bahari hiyo ya kifo" inaitwa barabara ya jangwa la Talimu, ilijengwa miaka 10 iliyopita. Barabara hiyo kwa upande wa kaskazini inaanzia wilaya ya Luntai, mkoani Xinjiang, na imefika katika wilaya ya Minfong mkoani humo, urefu wake ni kilomita 446, ambayo ni barabar ndefu kabisa duniani inayopita mahali penye mchanga unaohamahama.

    Kama kutengeneza barabara jangwani ni kitendo cha kishujaa, basi kupanda misitu kwenye "bahari" ya mchanga kumekuwa ni muujiza la Talimu, mwandishi wa habari aliona kuwa, miti ya aina mbalimbali inayofaa kuzuia upepo na kupeperushwa kwa mchanga pembezoni mwa barabara inakua vizuri.

    Katika majira ya mpukutiko ya mwaka 2003, kikundi cha uchimbaji wa mafuta wa Talimu kilianza kupanda misitu pembeni mwa barabara jangwani Talimu. Kwa mujibu wa mpango, mradi huo una kilomita 436, upana wake wa wastani ni mita 70 na zaidi, jumla ya gharama ni yuan za Renminbi milioni 220, na utakamilika baada ya miaka mitatu. Awamu ya kwanza ya mradi huo kilomita 200 imeshakamilika, awamu ya pili iko mbioni.

    Tatizo kubwa kabisa la kupanda misitu jangwani ni jinsi ya kuzuia mchanga unaopeperuka na kumwagilia misitu. Naibu mkuu wa idara ya misitu ya tarafa inayojitawala ya Bayinguole Bw. Zhou Jiang alijulisha kuwa, wafanyakazi kwanza wanajaribu kuzuia kupeperuka kwa mchanga kwa kutumia njia ya kupandikiza mabua katika miraba, baada ya kupanda miti mchanga, huchimbwa mpaka kupata maji ya ardhini pembeni mwa barabara, na kumwagilia miti kwa matone ya maji ili kuhakikisha mahitaji ya maji wakati miti inapokua.

   Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na idara ya usimamizi wa mradi wa misitu ya kuzuia upepo na kuhama kwa mchanga wa barabara ya jangwa la Talimu, inakadiriwa kuwa, ifikapo mwaka 2005, jumla ya eneo la misitu pembeni mwa barabara hiyo itakuwa hekta 3128, zenye miche zaidi ya milioni 20. wakati huo, barabara ndefu ya kijani duniani itaonekana jangwani Taklamagan.

Idhaa ya Kiswahili 2004-08-13