Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-18 17:27:33    
AIDS (UKIMWI) 16

cri
    Je, hapa kwetu kuna njia za kuthibitisha kwamba damu inayotolewa kuwapa wagonjwa haina viini vya UKIMWI?

    Ndio. Hospitali chache chini zimeanza kupima damu inayotolewa kuwapa wagonjwa. Haitachukua muda mrefu kutoka sasa kabla hospitali nyingi hazijajipatia vyombo vya madawa yanayotumika kwa kazi hii ya uchunguzi wa awali.

    Yawezekana hapa kwetu kabla ya kufunga ndoa maarusi wakapimwa kwanza ili kuhukikisha kuwa hawana UKIMWI? Gharama itaweza kuwa kiasi gani?

    Hapa kwetu tayari kuna uwezo wa kupima damu kwa kufanya uchunguzi wa awali. Gharama ya uchunguzi huu ni kiasi cha shilingi mia mbili.

    Lakini mara chache huenda uchunguzi huu wa awali ukatatanisha na kuhitaji uthibitisho kwa kufanya uchunguzi wa pili ambao unahitaji vifaa vyenye gharama zaidi na utaalam wa juu zaidi. Hapa kwetu tuna uwezo huo pia. Gharama kwa uchunguzi wa aina hii ya pili inakisiwa kwamba itaweza kuwa shilingi elfu mbili kwa mtu mmoja.

    Hapa kwetu waliowahi kutibiwa UKIMWI na kupona kabisa?

    Hapana. Baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakitibiwa na kupata nafuu, lakini ni kwa kipindi tu.

    Ikiwa hakuna dawa ya UKIMWI kuna haja gani basi kumshauri mtu mgonjwa awahi mapema kutibiwa?

    Kutokana na hali yake duni ya kujikinga na maradhi, yampasa awali mapema kutibiwa kila ugonjwa wa aina yoyote utakaompata hata uwe mdogo kiasi gani, kwani akichelewa kidogo tu ugonjwa huo utaweza kumzidi nguvu. Kwa kumsaidia kuponya angalau kwa muda magonjwa yanayomnyemelea mara kwa mara, mgonjwa ataweza kurefusha muda wake wa kuishi.

    Ikiwa siumwi popote, lakini kutokana na kupimwa damu imegundulika kwamba nina UKIMWI baridi, je, nifanye nini, na niishi maisha ya namna gani?

    Kuna mambo matatu muhimu ya kuzingatia. Jambo la kwanza ni kujitahidi kuzuia UKIMWI yako baridi isilipuke na kuwa UKIMWI vuguvugu au moto. Jambo la pili ni kujitahidi kupambana na magonjwa yatakayojaribu kukunyemelea. Na jambo la tatu ni kujitahidi kuepuka kueneza viini vya UKIMWI kwa wengine.

    Katika kujitahidi kuzuia UKIMWI yako isilipuke na kuwa vuguvugu au moto ujuzi tulio nao bado sio kamili, lakini huendea baadhi ya mambo yafuatayo yakaweza kukusaidia.

    1. Kama utakwepa kuongezea idadi ya viini vya UKIMWI mwili mwako kwa kuacha kuendelea kufanya matembezi, au kupewapewa damu, au kushirikiana sindano na watu wengine n.k.

    2. kama utakwepa magonjwa yanayopunguza nguvu zako?k.m. malaria, utapiamlo n.k.

    3. endapo wewe ni mwanamke, kama utakwepa kubeba mimba.