Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-20 17:52:52    
Nakshi za Shanxi

cri

 

 

 

 

 

    Nakshi za Jimbo la Shanxi zina historia ndefu. Nakshi za namna hiyo hutiwa kwenye mavazi, sadaka na vitu vya kuzikwa hasa katika vijiji vya jimbo hilo.

    Sehemu nyingine za jimbo hilo hulima mifurosadi na katani, hivyo wanawake hujifunza namna ya kusokota nyuzi, kufuma vitambaa na kutia nakshi tangu utotoni. Nao huanza kujifunza ufundi huo kwa mama zao na shemeji zao wakati wanapotia nakshi kwenye mavazi ya arusi. Katika siku ya arusi, wanawake wote wa upande wa bi-arusi na bwana arusi hutoka nje kuangalia mavazi ya arusi. kutokana na nakshi za kwenye mavazi wanapima kiwango cha wepesi wa akili cha bi-arusi. na baada ya ndoa, pia huhakiki hekima ya bi-arusi kutokana na mfuko wa kiunoni, mkoba wa fedha, mfuko wa tumbaku na vitu vingine ambavyo bi-arusi alimshonea mumewe.

    Vitu hivyo vilivyotiwa nakshi vingi vyao vinatumiwa nao wenyewe isipokuwa kimoja tu ni kwa ajili ya umma. Hiki ni kitambaa cha kufunika fataki. Katika siku za kale, wanavijiji walikuwa wakifanya sherehe ya kumkaribisha Mungu wa Majiko kwa kufyatua fataki. Fataki hiyo huzingirizwa kitambaa kabla ya saa za jioni ambao ni wakati wa kufyatua fataki. Kitambaa hicho nacho ni matokeo ya kuunganishwa kwa vipande vidogo vidogo vilivyotiwa nakshi na wanawake wa kijijini na ambavyo vilichaguliwa kutoka wanawake wote. Hivyo bi-arusi naye hujitahidi kutia nakshi ili kazi yake ichaguliwe na yeye mwenyewe asifiwe.

    Michoro kwenye nakshi huwa ni wachezaji wa opera, kwa sababu Jimbo la Shanxi lina husudu sana opera. Wasanii hutumia rangi nyeusi, buluu, nyekundu na kahawia nzito, hii inatokana na mila yao na mazingira ya jiografia ya sehemu hiyo. Wenyeji huwa weusi kidogo na shemu hiyo huwa na baridi, upepo wa mchanga na ardhi huwa kame.

Idhaa ya Kiswahili 2004-08-20