Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-27 20:57:35    
Mji wa Beiing waanza kushughulikia maombi ya kitambulisho cha ukazi wa kudumu kwa wageni nchini China

cri

    Tarehe 23 mwezi huu, mtaalamu kutoka Marekani Bw. Han Chun ambaye amekaa nchini China kwa miaka 50, alikwenda kwenye ofisi ya idara ya uhamiaji katika idara ya usalama wa raia ya Beijing, na kujaza fomu ya maombi ya kubadilisha au kupata kitambulisho cha kudumu cha ukazi kwa wageni nchini China.

    Hayo ni maombi ya kwanza yanayoshughulikiwa tangu idara ya usalama wa raia ya Beijing kutangaza kuteleleza kanuni za usimamizi wa haki ya ukazi wa kudumu kwa wageni nchini China tarehe 15 mwezi huu. Ndani ya mwezi mmoja, idara hiyo itampatia kitambulisho kipya Bw. Han Chun ambaye ameshapata hadhi ya ukazi wa kudumu nchini China.

     Bw. Han Chun mwenye umri wa miaka 80, pamoja na Bw. Kyoko Nakamura ambaye amekaa nchini China kwa miaka 59, walikuja China na kushiriki katika mapinduzi ya China wakati wa vita vya kupinga wavamizi wa Japan. Wao wanafurahi sana kupata kitambulisho hicho, na kusema kuwa kitarahisisha zaidi maisha yao nchini China.

    Hadhi ya ukazi wa kudumu ni hadhi ambayo matolewa na serikali ya nchi fulani kwa wageni wanaotimiza masharti ya kuwa na hadhi ya ukazi wa kudumu nchini humo kutokana na sheria. Kitambulisho cha ukazi wa kudumu kwa wageni nchini China ni kitambulisho halali cha wageni wanaotimiza masharti ya kisheria kukaa nchini China. Kitamblisho hicho kinaweza kutumika peke yake nchini China, na kutumika pamoja ya pasipoti wakati wa kuingia na kutoka nchini China. Wageni wanaopata kitambulisho hicho hawana haja tena kuomba visa wakati wa kuingia na kutoka nchini China. Kama wageni hao wakikaa kwa muda mrefu nchini China, hawana haja ya kuchunguzwa kitambulisho kila mwaka, na wakati makazi yao ya kudumu na mahali wanapofanya kazi pakibadilika, pia hawana haja tena ya kuomba idhini. Kitambulisho hicho kina pande mbili, upande mmoja una nembo ya taifa, na upande wa pili ni taarifa binafsi zinazoandikwa kwa Kichina na Kiingereza. Kitambulisho hicho kimetengenezwa kwa kutumia teknolojia nyingi za kuzuia kugushi, na kuwa na aina mbili za muda wa matumizi wa miaka 5 na wa miaka 10.

    Hivi sasa, wageni 156 kutoka nchi 20 ambao wamepata hadhi ya ukazi wa kudumu nchini China wanaoishi na kufanya kazi mjini Beijing. Idara ya usalama wa raia itawapatia kitambulisho cha ukazi wa kudumu nchini China ndani ya mwezi mmoja.

    Kutokana na kanuni, wageni ambao wamepata hadhi ya ukazi wa kudumu nchini China wakitaka kubadilisha kitambulisho cha ukazi wa kudumu nchini China, wanatakiwa tu kujaza fomu ya maombi ya kubadilisha au kupata tena kitambulisho cha ukazi wa kudumu, kutoa picha zao na kuonesha kitambulisho cha ukazi walichokuwa nacho, hawana haja ya kushughulikia tena uidhinishaji.

    Raia wa kigeni watakaotimiza masharti yafuatayo wanaweza kuomba hadhi ya ukazi wa kudumu nchini China: wataalamu wa ngazi ya juu wenye madaraka kwenye makampuni au sekta zinazotoa mchango mkubwa katika kusukuma mbele maendeleo ya uchumi, sayansi na teknolojia na jamii nchini China, au wawekezaji wa nje wenye vitega uchumi vya moja kwa moja vyenye thamani kubwa, wageni wanaohitajika sana wenye mchango mkubwa au umuhimu wa pekee kwa China pamoja na familia yao, pia wakiwa ni pamoja na waume au wake wanaokuja China kuambatana na wake au waume zao na kuishi pamoja, watoto wanaokuja kutegemea wazazi wao na wazee wanaokuja kutegemea ndugu zao wa damu.