Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-27 21:46:13    
China na nchi za Afrika zahitaji kuimarisha ushirikiano katika sekta ya habari

cri

   

 

 

 

 

Bw.   George Opiyo 

    Pamoja na urafiki mkubwa na wa muda mrefu uliopo kati ya watu wa Afrika na wachina, kutokana na mawasiliano hafifu kati ya watu wa kawaida wa pande hizi mbili, watu wa sehemu hizi mbili wamekuwa na picha zisizosahihi za kila upande. Kutokana na maendeleo ya kasi ya Uchumi wa China watu wengi zaidi wa Afrika wamekuwa na hamu ya kutaka kujionea wenyewe China ilivyo. Ili Kuwawezesha watu wa nchi za Afrika kuifahamu zaidi China na kuimarisha urafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika, ofisi ya habari ya baraza la serikali la China kuanzia tarehe 14 mwezi Agosti iliandaa semina ya kwanza ya habari ya maofisa wa serikali za nchi za Afrika, ambayo itafanyika kwa wiki mbili. Mkurugenzi wa idara ya habari katika wizara ya utalii na habari ya Kenya Bwana George Opiyo ni mmoja kati ya maofisa 18 walioshiriki kwenye semina hiyo. Kabla hajaondoka Beijing na kuelekea sehemu nyingine za China kwa matembezi zaidi, mwandishi wetu wa habari alipata fursa ya kuongea naye ili kupata maoni yake kuhusu jinsi anavyoiona China.           

    Bwana George Opiyo alisema kuwa, hii ni ziara yake ya pili nchini China, na safari hii inaonekana kuwa atakuwepo nchini China kwa wiki mbili. Alisema kuwa Watu wengi wa Afrika hawaifahamu China vizuri. Wengi bado wanadhani kuwa China ni nchi yenye watu wengi na masikini. Pia wanadhani kuwa China ni nchi isiyokuwa na maendeleo isipokuwa siasa ya U-komunisti. Lakini hali halisi ni kwamba China ni nchi kubwa na wananchi wa China wameendelea kuliko watu wengi wa Afrika wanavyofikiri. Kwa mfano mji wa Beining una wakazi milioni 13, idadi hiyo ya watu ni karibu nusu ya wananchi wa Kenya. Majengo yanayoonekana Beijing yanafanana na yale yanayoonekana katika nchi za Ulaya. Mbali na juhudi za wananchi, maendeleo ya China pia yanatokana na sera ya kufungua mlango ili kuvutia vitega uchumi kutoka nje. Bwana Opiyo anaona kusikia sio kuona, watu wengi wa nchi za Afrika wakipata nafasi ya kutembelea China wanaweza kushuhudia wao wenyewe hali ya maendeleo ya China.

   

 

 

 

 

 

Bw.   George Opiyo  na mwandishi wa habari wa CRI Bibi Du

    Bw Opiyo aliisifu sana serikali ya China kuandaa semina hiyo, na kusema kuwa kuna haja kubwa ya kuimarisha uhusiano kati ya vyombo vya habari vya China na Afrika. Pia alisema vyombo vya habari vya nchi za magharibi vinatoa habari kuhusu Afrika kwa kutumia vigezo vyao, lakini baadhi ya habari vinavyotoa hazisaidii maendeleo ya nchi za Afrika na kwa wakati fulani habari hizo huleta athari mbaya.

   

 

 

 

 

 Bw.   George Opiyo  na waadishi wa habari wa CRI Xie na Peng

    Nchi za Afrika na China zinasimama kwenye upande mmoja, na safari hii semina ya maofisa wa habari wa nchi za Afrika zinazoandaliwa na serikali ya China pia zinalenga kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta ya habari ili watu wanaofanya kazi katika sekta hiyo barani Afrika na China waweze kufanya kazi zinazosaidia kusukuma mbele maendeleo ya uchumi na ushirikiano wa kirafiki kati ya sehemu hizo mbili.

Idhaa ya kiswahili 2004-08-27