Mtu anapofikia umri wa miaka 20 hivi, huwa anakabiliwa na shinikizo la masomo. Utafiti uliotangazwa katika mkutano wa mazungumzo ulioandaliwa na wizara ya afya kuhusu afya ya saikolojia (psychology) ya watoto na vijana, unaonesha kuwa 32% ya vijana wana matatizo ya saikolojia. Na matokeo ya uchunguzi uliofanywa kwa baadhi ya wanafunzi katika vyuo vikuu 16, yanaonesha kuwa tatizo la akili, limekuwa sababu muhimu inayowafanya wanafunzi wa vyuo vikuu kupumzika kusoma kwa muda au kucha kabisa masomo yao. Taarifa ya uchunguzi uliofanyika mwaka 2003, inasema kuwa idadi ya wanafunzi walioacha masomo kutokana na ugonjwa uliosababishwa na matatizo ya kisaikolojia ilichukua kiasi cha nusu ya idadi ya wanafunzi walioacha masomo kutokana na sababu mbalimbali.
Habari kutoka kituo cha kutoa maelekezo ya kisaikolojia zinasema kuwa, kati ya watu waliokwenda kwenye kituo hicho kuomba ushauri, wengi ni wanafunzi wanaokabiliwa mitihani ya kuingia sekondari na vyuo vikuu. Kutoka utotoni, watoto wanatunzwa na kuelimishwa na wazazi wao katika hali maalumu, wazazi wanakuwa na matarajio makubwa kwa watoto wao kuwa wasomi. Licha ya hayo, wanafunzi wanakabiliwa na shinikizo la wanafunzi wenzao wanaotarajia kusoma katika vyuo vikuu, hivyo wanasoma kutwa kucha, kujifungia vyumbani wakisoma na kufanya mazoezi ya masomo, kitu ambacho kimekuwa ni kazi ngumu na wala siyo ya furaha. Uchunguzi uliofanyika hivi karibuni mjini Guangzhou, unaonesha kuwa 69.5% ya wanafunzi vijana wanajisikia shinikizo kubwa la masomo.
Mtu anapofikia umri wa miaka 30 hivi, anakuwa na shinikizo la ndoa na kazi. Kutokana na ushindani katika sekta mbalimbali, kupata ajira kumekuwa ni kugumu sana. Hata mtu aliyekwishapata ajira, anakabiliwa na hatari ya kuachishwa kazi kutokana na maendeleo ya jamii na uchumi. Hivyo watu wanaoishi hivi sasa, hususan watu wanaoanza kuingia katika jamii, wanakuwa na shinikizo kubwa la kazi mwaka hadi mwaka.
Mtu anapoingia katika umri wa miaka ya 50, anakabiliwa na shinikizo la kazi na maisha. Mtu anapokuwa wa makamo, licha ya kusikia shinikizo la kazi, anabeba mzigo mkubwa wa familia, hali ambayo inaweza kumsababishia wasiwasi moyoni, hivyo anatakiwa kuchukua hatua ya tahadhari na kujiandaa kwa hali ya namna hiyo.
Mbali na hayo, watu hawana budi kukabiliana na matatizo ya nyumba, mawasiliano finyu na msongamano wa magari, pamoja na kuwatunza wazee na watoto. Kasi na hali ya kubadilika mara kwa mara kwa maisha, vinaingilia utulivu wa ndoa na familia, ambapo mapenzi nayo yanakabiliwa na vikwazo vya aina mbalimbali. Kutokana na migongano ya maslahi ya aina mbalimbali, uhusiano kati ya watu umekuwa na utata, watu wanashidwa kubadilishana mawazo mara kwa mara, hata katika wakati ambapo watu wanakumbwa na matatizo au vikwazo, hawapati mahali pa kujituliza.
Mambo hayo yanatutatiza na kutufuata mara kwa mara. Baada ya kupita muda mrefu, akili yetu inatokewa na hali isiyo ya kawaida, mienendo yetu inaachana na njia ya kawaida na kuwa na hali mbaya ya mwili, hisia na wasiwasi.
Idhaa ya kiswahili 2004-08-31
|