Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-01 16:46:43    
AIDS (UKIMWI) 18

cri
    Nikisikia kwamba mtu ambaye nimewahi kukaribiana naye kimwili amepatikana na AIDS nifanye nini?

    Nenda ukapimwe endapo muda wa miezi miwili au zaidi umeshapita tangu mkaribiane. Kama muda huo haujapita, subiri kwanza mpaka uwadie. Ili kuwa na uhakiak zaidi yafaa urudie kupimwa tena safari moja au mbili baada ya kupita mwaka mmoja au miwili.

    Eti kuna dawa za uzazi wa majira zinazoweza kuua viini vya AIDS?

    Mpaka sasa imegundulika kwamba kuna dawa fulani fulani (k.m. Nonoxynol-9) za uzazi za kiume ambazo zina uwezo wa kufanya viini vya AIDS vishindwe kufanya mashambulizi yake. Hata hivyo wataalamu hawajafanya utafiti wa kutosha kuhusu matumizi yake kwa kusudi hilo la kupambana na AIDS.

    Mambo ya msingi kuhusu AIDS

    Kama umesoma kwa makini maswali yote yaliyoulizwa na wenzako bila shaka umejifunza mengi kutokana na majibu yaliyotolewa. Lakini endapo kuna mambo mengine ambayo yamekutatanisha au ambayo hukuyaelewa vizuri, hapa tungependa kukuorodhesha yale ambayo tunaona ni ya msingi na ambayo kwa vyovyote ni lazima uyakumbuke wakati wote.

    1. kwa kawaida AIDS ni ugonjwa wa waasherati.

    2. mara chache watu wasio waasherati wanaweza kuupata kwa kupewa damu, au kwa kudungwa sindano, au kwa kurithi kutoka kwa mama.

     3. ni ugonjwa unaodumu mwilini mwa mtu maisha yake yote.

    4. hautibiki.

    5. hauna kinga.

    6. huleta kifo.

    7. hauambukizi kwa urahisi kwa kushirikiana na wagonjwa kwa njia nyingine za kawaida-ukiondoa kushirikiana mwili, damu, sindano n.k.

    8. mama mja mzito mwenye ugonjwa huweza kumwambukiza mwanae aliye tumboni.

    9. mwenye hatari kubwa zaidi au nafasi kubwa zaidi ya kuambukiza wengine ugonjwa siye yule anayeonekana ni mgonjwa, bali ni yule anayeonekana na anayejisikia kuwa na afya kamili, kumbe mwilini mwake vimejificha viini vya ugonjwa-huku yeye mwenyewe akiwa pengine hana hata habari.

    10. kuishi kwa uaminifu katika unyumba na mwenzi ambaye hana ugonjwa ndiyo njia iliyo salama kuliko zote. Kama hilo haliwezekani njia iliyo salama kidogo ni angalau kupunguza idadi ya watu wa kukaribiana nao kimwili.

    11. mipira ya kuvaa uumeni inaweza kuwa kinga ya kusaidia wale watakaolazimika kukaribiana kimwili ili wasiambukizane wao kwa wao; na pia ili kukomesha ugonjwa usiendelee kwa vizazi vitakavyofuata.

    12. kupima damu kabla ya kuwapa wagonjwa, na kuchemsha sindano kabla ya kuwadunga watu ni silaha muhimu za kinga.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-01