Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-01 18:11:16    
Wajumbe maalum wapatao elfu 1 wanaoshughulikia sayansi na teknolojia

cri

    Habari kutoka idara ya sayansi na teknolojia ya serikali ya mkoa wa Ningxia, China zinasema kuwa, ili kusukuma mbele maendeleo ya uchumi vijijini, kuanzia mwezi Septemba mwaka 2002, mkoa wa Ningxia ulianzisha majaribio ya kuwapeleka wajumbe maalum wanaoshughulikia sayansi na teknolojia kufanya kazi vijijini katika wilaya za Zhongwei, Zhongning, Qingtongxia na Pingluo. Uzoefu wa miaka mitatu umeonesha kuwa, majaribio ya wajumbe hao yaliyofanyika kwa lengo la kuinua kiwango cha uzalishaji wa kilimo, kuongeza mapato ya wakulima na kukuza uchumi wa wilaya hizo pia ni njia nzuri ya kuongeza uwezo wa nguvu ya uzalishaji katika kipindi kipya.

    Hivi sasa, wajumbe maalum wapatao elfu 1 na mashirika 20 ya kisheria ya wajumbe maalum yanafanya kazi kubwa katika vijiji vya Ningxia. Wajumbe hao waliposhiriki kwenye majaribio ya kusukuma mbele maendeleo ya uchumi katika wilaya za huko, walianzisha kazi mbalimbali za ujenzi wa miradi, kuwafundisha wakulima ufundi, kuwapatia habari mbalimbali kuhusu uzalishaji na uuzaji wa mazao; baadhi yao walitoa fedha na ufundi wao kushirikiana na wakulima kufanya shughuli mbalimbali ili kuleta maslahi ya pamoja, na wengine walianzisha mashirika mbalimbali ya kiuchumi ili kuwahudumia wakulima.

    Kutokana na takwimu zilizokusanywa mwishoni mwa mwaka 2003, wajumbe hao wameanzisha miradi 174. Jumla ya gharama za uwekezaji zimefikia yuan za renminbi milioni 390, na pato la uzalishaji kwa mwaka mzima limefikia yuan milioni 465, ambalo limewanufaisha wakulima wengi. Katika vituo, mashirika, na maeneo ya vielelezo ambapo wajumbe hao wanafanya kazi mbalimbali, pato la wastani la kila mkulima limeongezeka kwa yuan za renminbi 50 hadi 60 ikilinganishwa na zamani.

 

    Kazi za wajumbe hao zimeanzisha kielezo cha Ningxia yaani kwenye msingi wa miradi ya sayansi na teknolojia, kuweka mkazo katika kuanzisha shughuli kwa njia ya kisayansi na kiteknolojia; kutekeleza utaratibu mpya na kuzingatia msukumo wa kiuchumi, kushikilia uelekezaji wa soko, na kusukuma mbele kazi za utawala wa serikali, jamii na soko. Uvumbuzi na njia inayotumika ni kuwa, kwanza, kusukuma mbele kazi za utawala wa serikali, jamii na soko kwa wakati mmoja; pili, kuunganisha na uchumi wa vijijini, kuanzisha aina mpya za huduma ya kiuchumi, na kuwagawanya wajumbe maalumu katika ngazi tatu na kuwapa kadi ya dhahabu, fedha na shaba; tatu, kushikilia kuunganisha majaribio ya wilayani na vitendo maalum; nne, kuanzisha utaratibu wa uwekezaji, na kukuza kazi kwa miradi; tano, kubuni sera ya kutoa kipaumbele na kuanzisha kanuni na utaratibu; sita, kuzingatia kutoa mafunzo kwa watu vijijini ili wachangie maendelo ya uchumi vijijini.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-01