Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-03 18:59:51    
Urafiki kati ya China na Zambia wazidi kuimarishwa

cri
    Wachina wanazifahamu Zambia na Tanzania kutokana na reli ya TAZARA iliyojengwa miaka 30 iliyopita. Hivi karibuni, waandishi wetu wa habari walipata fursa ya kuitembelea reli hiyo, na kampuni nyingine maarufu za ubia za China na Zamiba nchini Zambia. Urafiki kati ya nchi hizo mbili ulianzishwa miaka 40 iliyopita. Hivi sasa, hali mbalimbali za nchi ya Zambia zinafanya waandishi wetu wa habari kuhisi kuwa, urafiki huo unazidi kukuzwa na kuimarishwa.

    Wakati ofisa wa ubalozi wa China nchini Zambia Bw. Zhao Zhanbin alipowaambia waandishi kuwa, reli ya TAZARA inaendelea kufanya kazi, wote walifurahi sana. Baada ya kusafiri kwa kwa gari kwa umbali wa kilomita 200, walifika kwenye kituo cha mwanzo cha reli hiyo cha Sinka, mnamo saa tisa alasiri. Garimoshi lilikuwapo tayari kuanza safari, abiria walikuwa wakipanda kwenye garimoshi kwa utaratibu. Baadhi ya abiria wa waafrika walipoona waandishi wa habari waliotoka China waliwasalimia kwa furaha.

    Reli ya TAZARA ina umbali wa kilomita 1860. Tangu ujenzi huo uanze mwaka 1970, mafundi elfu 50 wa China walishiriki kwenye ujenzi huo, kati yao zaidi ya 60 walipoteza maisha yao. Ujenzi wa Reli ya TAZARA ulimalizika mwaka 1975 na kuanza kufanya kazi mwaka uliofuata. Mpaka sasa imefanya kazi kwa miaka 29, na kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya uchumi wa Tanzania, Zambia na nchi jirani zao. Katika miaka mitatu iliyopita, reli hiyo ilisafirisha tani laki 6. 3 za mizigo, na abiria milioni 1.5 kila mwaka.

    "Katika miaka 29 iliyopita, serikali ya China ilipeleka vikundi 11 vya wataalamu, na kutenga fedha RMB milioni 90. Jumla ya wataalamu 3000 walishiriki kwenye usimamizi wa reli hiyo, na kutoa mwongozo wa teknolojia." Mkuu wa kikundi cha wataalamu wa China wa Reli ya TAZARA nchini Zambia Bw. Sun Wenhua alisema.

    Mbali na reli ya TAZARA, China inashirikiana na Zambia katika nyanja nyingine mbalimbali, na ushirikiano kati yao ni pamoja na kiwanda cha nguo, kilimo, ujenzi na uchimbaji wa madini. Kampuni ya madini ya China ilianzisha kampuni ya madini ya ubia nchini Zambia mwezi Machi, mwaka 1998, na ilianza kukabidhiwa shughuli za usimamizi wa mgodi wa shaba wa Zambezi mwezi Septemba, mwaka huo. Madini ya shaba yalichimbiliwa kwanza tarehe 10, Novemba, mwaka 2003. Mbali na hayo, eneo la kazi linazidi kupanuka.

    Waandishi wetu wa habari walitembelea kampuni ya nguo ya Mulungushi. Waliona kuwa, miradi mingi iliyoanzishwa kwa misaada ya China inatia uhai mpya kwa maendeleo ya uchumi wa Zambia baada ya kufanya mageuzi.

    Kiwanda cha nguo cha Mulungushi kiko katika mji wa Kabwe. Kiwanda hicho kilianzishwa mwaka 1966. Mwaka 1996, kampuni kuu ya nguo ya Qing Dao ikishirikiana na wizara ya ulinzi ya Zambia zilianzisha kampuni ya ubia, na Zambia inamiliki asilimia 34 ya hisa. Kutokana na mbinu mpya za usimamizi, na matokeo ya kunufaishana pande zote, pande hizo mbili zinaonesha juhudi kubwa zaidi na hali ya kuendesha ya kampuni hiyo imeboreshwa kwa kiasi kikubwa.

    Meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Yan Yong alisema kuwa, baada ya juhudi za miaka kadhaa, kampuni hiyo ya ubia inashughulikia kazi nyingi zaidi, badala ya kazi ya utiaji rangi na utengenezaji wa nguo tu, na imebadilika kuwa kampuni kubwa inayoshughulikia upandaji na uchambuaji wa pamba, utengenezaji wa mafuta ya pamba, uendeshaji wa maduka yenye matawi mbalimbali, na kuingiza uwekezaji vitega uchumi wa biashara ya kimataifa. Mwaka 2002, kampuni hiyo ya nguo ilifanikiwa kupata maendeleo makubwa katika mapato, kwa kuuza bidhaa nje na kupata faida kubwa zaidi. Baada ya hapo, ilipata ongezeko kubwa zaidi mwaka 2003.

    Maendeleo ya kampuni hiyo ya ubia yanatoa mchango mkubwa katika nyanja mbalimbali za Zambia. Takwimu zinaonesha kuwa, kampuni hiyo imelipa kodi za dola za kimarekani milioni 5, na kutoa mchango wa fedha kwa sehemu hiyo. Hali ya wazi ni kwamba, idadi ya watu wanaoajiriwa kwenye sehemu hiyo wanaongezeka kwa kiasi kikubwa. Hivi sasa, kampuni hiyo imewaajiri wenyeji wa huko zaidi ya 2000, wakati wakulima wanaopanda pamba wanazidi elfu 30. Wafanyakazi wote walisema kuwa: "Tunaona fahari tukiwa wafanyakazi wa kampuni ya China."

    Mwakilishi wa Zambia ambaye pia ni naibu meneja mkuu wa kampuni ya ubia Bw. Zidafe aliwaambia waandishi wetu habarikuwa, kampuni ya ubia inatoa mchango mkubwa kwa uchumi wa Kabwe, na tunatumai kuwa itakuwa mfano mzuri kwa kampuni za Zambia.

    Shamba la urafiki kati ya China na Zambia lenye historia ndefu limebadilisha njia yake ya zamani ya uendeshaji. Mkuu wa shamba hilo Bw. Dong Fafu aliwaongoza waandishi wetu wa habari kutembelea shamba hilo lenye hekta 667, na alieleza kuwa, "Shamba hilo limeajiri wenyeji 165, idadi hiyo itafikia 800 ikiwa ni pamoja na jamaa zao."

    Kutokana na hali nzuri ya uendeshaji na usimamizi, shamba hilo lilipata faida kubwa, na wafanyakazi wanafurahi kufanya kazi katika shamba hilo. Wakati huo huo, shamba hilo linafanya utafiti kuhusu mbinu mpya za kilimo. Wizara ya kilimo na Idara kuu ya takwimu za Zambia zitaeneza uzoefu wake mzuri nchini kote Zambia.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-03