Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-03 20:13:01    
Kuziwezesha sehemu za milimani kujiendeleza na kupata utajiri kama zilivyo sehemu za pwani

cri

   

Delta ya Mto Zhu Jiang, mkoani Guang Dong, ambayo iko mstari wa mbele katika mageuzi na ufunguaji mlango, inafanya juhudi kubwa kuzisaidia sehemu za milimani kuendeleza uzalishaji. Miji iliyopo sehemu za milimani zinajitokeza kushiriki katika ushirikiano na mgawanyo wa kazi wa uchumi, na kushiriki kwa hiari katika shughuli zinazoletwa na sehemu zilizoendelea. Toka mwez Januari hadi Juni mwaka huu, ongezeko la mapato ya miji mbalimbali ya sehemu za milimani lilizidi kwa mara ya kwanza wastani wa ongezeko la mkoa.

    Tangu sera ya mageuzi na kuzifungulia mlango nchi za nje ianze kutekelezwa , pengo la mapato kati ya sehemu tajiri ya Delta ya Mto Zhu Jiang na sehemu za milimani za mkoa wa Guangdong limekuwa likongezeka siku hadi siku, hata wastani wa pato la kila mtu wa sehemu tajiri kabisa ni zaidi ya mara 10 ya lile la sehemu maskini kabisa. Maendeleo ya uchumi wa baadhi ya sehemu za milimani mkoani humo hata hayafikii kiwango cha sehemu za ndani na magharibi za China. Hali hiyo inazuia maendeleo ya uchumi wa Mkoa wa Guangdong.

    Kutokana na maelekezo ya wazo kuhusu kujiendeleza kwa njia za kisayansi, serikali ya mkoa wa Guangdong inaona kuwa "Delta ya Mto Zhujiang iliyotajirika inapaswa kuzisaidia sehemu za milimani zenye hali duni", hivyo imeweka mkazo katika kuharakisha maendeleo ya sehemu za milimani, na kuchukua hatua thabiti mbalimbali za kutia nguvu za uhai kwa maendeleo ya uchumi wa sehemu za milimani. Miaka miwili iliyopita, serikali ya mkoa wa Guangdong ilichukua hatua mbalimbali za kusaidia maendeleo ya sehemu za milimani katika sekta mbalimbali, na kuanzisha utaratibu wenye nguvu wa kutoa misaada, kuzisaidia sehemu hizo kuboresha mazingira ya kujiendeleza badala ya kuyasaidia tu maendeleo ya uchumi wa sehemu hizo. Serikali ya mkoa huo imetenga yuani bilioni 37.5 kwa ajili ya ujenzi wa sehemu za milimani. Kutokana na sera hizo, miundo mbinu ya sehemu za milimani imeboreshwa kwa kiasi kikubwa, ujenzi wa mazingira ya kimaumbile umeimarishwa kwa udhahiri na hifadhi ya mazingira na shughuli za elimu na afya za sehemu za milimani zinaendelea kwa kasi.

    Kila mji wa Delta ya Mto Zhu Jiang unasaidia mji au wilaya moja ya sehemu za milimani, kwa jumla msaada huo bila ya malipo wa yuani milioni 5 unahakikishwa kutolewa kwa mwaka, na kuongezeka tena kwa zaidi ya 5% kila mwaka. Misaada hiyo ambayo ni kama "kuwapa damu" ilibadilishwa kuwa "kuwasaidia kuzalisha damu wenyewe", imepata ufanisi halisi, na pande mbili zimenufaishana.

    Sehemu za milimani za mkoa wa Guangdong pia zinajitahidi kujipatia maendeleo makubwa ya uchumi. Ingawa sehemu hizo zilichelewa kupiga hatua ya kujiendeleza, lakini ziliposhirikiana na sehemu iliyoendelea ya Delta ya Mto Zhujiang zilifanya juhudi kubwa za kuendeleza shughuli za kilimo, viwanda na utalii kutokana na mazingira halisi ya kipekee ili kuongeza nguvu ya ushindani. Sasa sehemu hizo za milimani zinaweka mkazo katika shughuli za nguvu kazi nyingi na miradi isiyoleta uchafuzi kwa mazingira badala ya kuanzisha viwanda vya aina mpya vinavyozingatia faida tu.

    Njia nyingine ya kusukuma mbele maendeleo ya uchumi wa sehemu za milimani ni kupanda mboga na maua ili kuziuza katika sehemu za jirani kama vile mikoa ya Hong Kong na Macau na Delta ya Mto Zhujiang. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, ongezeko la uchumi wa mji wa Qingyuan lilifikia 19.8% kutokana na kuzalisha mazao ya kilimo yenye umaalum wa sehemu hiyo, hivi sasa mji huo unafanya juhudi kubwa za kuendeleza kilimo kwa kufuata kigezo duniani ili kuyawezesha mazao ya kilimo kuuzwa kwenye soko la dunia.

    Na sehemu nyingine za milimani mkoani Guangdong zinajitahidi kuendeleza shughuli za utalii kutokana na hali halisi ya sehemu hizo ili kuongeza mapato na kuboresha maisha ya watu wa huko.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-02