Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-08 16:50:37    
Shule za kiraia zaongezeka haraka mkoani Zhejiang nchini China

cri

                          

    Shule ya Huamei iko kwenye pwani wa Mto Qiantang mjini Hangzhou, mji mkuu wa mkoa wa Zhejiang, shule hiyo ilianzishwa na kampuni ya binafisi ya Zhejiang, na uwekezaji katika shule hiyo ulifikia Yuan milioni 300. shule hiyo yenye eneo la mita elfu 50 za mraba ilianzishwa mwaka 2001mjini Hangzhou. Shule hiyo ina chekechea, shule ya msingi, shule ya sekondari na shule ya sekondari ya juu, sasa ina wanafunzi elfu 2 kutoka Shanghai, Jiangsu, Fujiang wanaosoma katika shule hiyo.

    Ukiingia katika eneo la shule ya Huamei, utaona majengo ya madarasa mbalimbali na watoto wenye furaha wakiwa madarasani. Zhongdi ni mmoja wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo, alisema kuwa, baada ya kujiunga na shule hiyo, lengo lake kubwa ni kupata furaha katika masomo, mbali na hayo, mabadiliko makubwa yalipatikana katika fikra yake. Anasema:

    " baada ya kujiunga na shule hiyo, niliona nilianza kukutana na dunia ya nje, hasa baada ya kujifunza lugha ya Kingereza. Kabla ya hapo, mimi sipendi kuzungumza na watu wengine, lakini baada ya kujifunza lugha ya kingereza, mwalimu aliniambia kwamba, ninapaswa kutokuwa na aibu na kuzungumza lugha ya kingereza mbele ya watu wengine. Alitutaka kuzungumza kingereza kwa sauti kubwa."

    Mwanafunzi wa darasa la 6 wa shule ya msingi Zhang Wei alimwambia mwandishi wa habari kuwa, wazazi wake walishangaa kuona mabadiliko yake baada ya kujiunga na shule hiyo. Anasema:

    " zamani nilikuwa sipendi kukutana na watu wengine, uwezo wangu katika somo la lugha kingereza haukuwa mzuri, na somo la kichina na somo la hisabati ilikuwa ni kawaida tu. Baada ya kujiunga na shule hiyo, maendeleo makubwa yalipatikana katika masomo ya kingereza, na uhusiano kati yangu na wenzangu ni mzuri sana. Walimu wa shule hiyo ni kama marafiki zangu."

    Naibu Mkuu wa Shule ya Huamei Bibi Zhang Meihong alisema kuwa, mabadiliko ya wanafunzi katika shule hiyo yanatokana na mtazamo mpya wa elimu na mfumo mpya wa mafunzo. Zamani shule nyingi za China zilitilia maanani tu matokeo ya mitihani ya wanafunzi, lakini shule ya Huamei ilisisitiza mafundisho ya kufurahisha wanafunzi na elimu ya ubora wa watu. Bibi Zhang alijulisha:

    " katika masomo ya muziki, michezo, uchoraji na kompyuta, tuliacha kutumia vitabu vya masomo vya zamani, katika mitihani wanafunzi wanatazamiwa kuonesha matokeo yao baada ya kujifunza masomo hayo. Kwa mfano, katika somo la piano, katika siku ya mtihani, wazazi wa wanafunzi wataunda kikundi cha kuthibitisha matokeo ya wanafunzi. Wazazi walisifu sana njia hiyo mpya ya mtihani. Katika somo la uchoraji, kila mwanafunzi wa darasa la pili la shule ya msingi anachora vizuri, hasa kila mtoto anaweza kueleza hadithi kwa kutegemea uchoraji wake. Wazazi walishangaa sana."

    Sasa somo la muziki katika shule ya Huamei ni pamoja na Piano, na kuimba, pamoja na muziki hodari za duniani; somo la michezo ni pamoja na michezo ya Wushu, kuogelea, mpira wa kikapu; somo la uchoraji ni pamoja na uchoraji wa kichina, uchoraji wa kuchapisha na uchoraji wa mstari?

    Mbali na hayo, shule ya Huamei pia ilianzisha somo la uboreshaji wa mwili na "thanks giving". Bibi Zhang Meihong anasema:

    " tulianzisha somo la kutoa shukurani, katika mkutano wa darasa, wanafunzi wanasoma maneno ya kutoa shukurani, kwa mfano kuwashukuru wazazi, walimu, maisha, marafiki, mazingira. Sasa watoto wengi hawaoni wajibu kwa jamii na binadamu, wakati fulani, wanaonesha ubinafsi ambapo hawajui kuwashukuru watu wengine."

    Alisema kuwa, shule ya Huamei haikuwahimiza wanafunzi kufanya mashindano katika matokeo ya mitihani. Sifa kubwa ya shule ya Huamei ni " mwana wa Huamei" na "Nyota ya Huamei". Ili kuwasifu wanafunzi waliopata mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali, shule ilianzisha tuza za "nyota ya michezo", na "nyota ya uwimbaji" ili kuwawezesha watoto waweze kuishi na kusoma kwa furaha na kupata maoni ya kushinda."

    Naibu Mkuu wa Shule ya Huamei Bibi Zhang Meihong alimwambia mwandishi wa habari kuwa, kuanzisha shule nzuri nchini China hata duniani, kunatakiwa kuwa na walimu wenye uwezo mkubwa. Hivyo, walimu wa shule ya Huamei wote walifaulu mitihani mingi, wana elimu na uzoefu wa kufundisha. Sasa shule ya Huamei imeanzisha uhusiano mzuri na idara za elimu za Marekani, Canada, Ireland, pamoja na Australia.

    Shule ya Huamei ni moja kati ya shule elfu 10 za kiraia mkoani Zhejiang. Baada ya maendeleo ya miaka 20, shule za kiraia za Zhejiang zimekuwa mbele nchini China.

Idhaa ya kiswahili 2004-09-08