Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-10 21:00:35    
Matukio makubwa ya mashambulizi ya kigaidi duniani yaliyotokea tangu "9.11"(Sehemu B)

cri
Tarehe 20 mwezi Novemba, milipuko miwili katika magari ilitokea kwa nyakati tofauti kwenye mlango wa tawi la benki ya HSBC ya Uingereza mjini Istanbul na wa ofisi ya balozi mdogo, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 30 na wengine zaidi ya 450 kujeruhiwa.

Tarehe 5 mwezi Mei, garimoshi moja la abiria lililipuka huko jimbo la Stavropol na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 44 na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa.

Mwaka 2004

Tarehe 6 mwezi Februari, subway ya huko Moscow, Russia, ililipuka na kusababisha vifo vya watu karibu 50 na wengine zaidi ya 130 kujeruhiwa.

Tarehe 2 mwezi Machi, milipuko ya mfululizo ilitokea katika misikiti miwili ya madhehebu ya shia iliyopo Baghdad na Karbala, na kusababisha vifo vya watu 271 na wengine 500 hivi kujeruhiwa.

Tarehe 11 mwezi Machi, magarimoshi matatu yalilipuka kwa mfululizo huko Madrid, mji mkuu wa Hispania?watu wasiopungua 198 waliuawa na watu wapatao 1800 kujeruhiwa katika milipuko hiyo.

Tarehe 9 mwezi Mei, mlipuko ulitokea katika uwanja mmoja wa michezo huko Grozzy, mji mkuu wa Jamhuri ya Chechnya, watu 7 akiwemo rais Kadrov wa Jamhuri ya Chechnya waliuawa na wengine 53 kujeruhiwa katika mlipuko huo.

Kuanzia tarehe 21 mwezi Juni usiku hadi tarehe 22 asubuhi, vikundi haramu vya watu wenye silaha walishambulia idara kadhaa za usimamizi wa sheria huko Nazran, na miji mingine nchini Jamhuri ya Ingushetiya, na kusababisha vifo vya watu 90 pamoja na kaimu wa wizara mbadala wa mambo ya ndani na naibu wake wa nchi hiyo.

Tarehe 24 mwezi Agosti, ndege mbili za abiria zilizotoka kiwanja cha ndege cha Domodedovo mjini Moscow zilianguka karibu kwa wakati mmoja katika jimbo la Tura na Rostov, na watu 89 wakiwa ni pamoja na abiria na wafanyakazi wa ndege wote walikufa.

Tarehe 31 mwezi Agosti, mlipuko wa kigaidi ulitokea karibu na kituo kimoja cha subway mjini Moscow, na ilisababisha vifo vya watu 10 na wengine 51 kujeruhiwa.

Tarehe 1 mwezi Septemba, kundi moja la magaidi lilivamia shule ya sekondari No.1 katika mji wa Beslan, nchini Jamhuri ya North Ossetia, na kuwateka nyara watu zaidi ya 1000 wakiwa ni pamoja na walimu, wanafunzi na wazazi wao, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 300, miongoni mwao, karibu nusu yao ni watoto.

Tarehe 9 mwezi Septemba, mlipuko wa mabomu ulitokea kwenye sehemu iliyo karibu na ubalozi wa Australia nchini Indonesia, na kusababisha vifo vya watu 9 na mejeruhi 182.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-10