Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-15 16:43:34    
Binadamu amekuwa na hisia kuhusu uzuri tangu alipozaliwa

cri

    Hisia ya binadamu kuhusu uzuri inatoka wapi? Pengine hili ni swali gumu linalowatatiza watu wengi. Utafiti uliofanywa hivi karibuni na wanasayansi wa Uingereza umeonesha kuwa, hisia hiyo ya binadamu inakuwepo tangu anapokuwa tumboni mwa mama, hata mtoto mchanga aliyezaliwa tu, anaweza kupambanua uzuri na ubaya.

    Wataalamu wa saikolojia ya ukuaji (up growth psychology) katika miaka mingi iliyopita walithibitisha kuwa watoto wachanga wanapenda baadhi ya vitu maalumu, kwa mfano kuhusu viumbe virefu na vyenye kupindika, wanapenda kuona vile vinavyotembea, wala siyo vile vilivyotulia. Ingawa watu wametafakari sana, lakini bado hawajafahamu ni Kwanini watoto wanapenda vitu vya namna hiyo. Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa chuo kikuu cha Ecsait umethibitisha maoni ya watu wengi, yaani binadamu anapozaliwa hawi kama "karatasi nyeupe", bali anakuwa tayari na mfumo kamili wa hisia kuhusu uzuri.

    Vyombo vya habari nchini Uingereza tarehe 6 vilitoa habari zikisema kuwa wanasayansi wa chuo kikuu hicho katika utafiti wao walitumia picha nyingi za nyuso za wanawake. Kwanza, walitaka baadhi ya watu wazima watoe pointi kuanzia 1 hadi 5 kwa kufuata uzuri wa sura za nyuso za wanawake katika picha hizo. Kisha, wanasayansi walitoa picha za wanawake hao kutoka za pointi 1 hadi 5, na walichagua picha zile ambazo mwangaza wa nyuso za wanawake unaolingana.

    Baada ya hapo, waliwaonesha picha hizo watoto wachanga waliozaliwa ndani ya siku 7. Mtafiti mmoja alimpakata mtoto mchanga na kusimama kwenye futi moja kutoka kwa picha hizo, na mtafiti mwingine alikuwa anaangalia macho ya mtoto mchanga yataangalia picha ipi. Matokeo ya utafiti yalionesha kuwa watoto waliangalia zaidi picha yenye sura nzuri ya mwanamke.

    Kiongozi aliyesimamia utafiti huo alipohojiwa na mwandishi wa habari alisema kuwa sababu ya kukadiria kuwa watoto wachanga walikuwa na hisia kuhusu uzuri toka wanapozaliwa ni kuwa, mtu mwenye sura nzuri ni mtu mwenye sura yenye uzuri ya kiwango cha kupendwa na watu. Binadamu anapozaliwa, amekuwa na habari kamili kichwani mwake kuhusu sura ya binadamu yenye uzuri wa kiwango kinachopendwa na watu, hivyo ni rahisi kwake kupambanua sura za aina hiyo.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-15