Tarehe 11 Juni, gesi inayotoka Tarim, mkoani Xinjiang, magharibi mwa China ilifika Jingbian mkoani Shan'xi. Hii ina maana kuwa mradi wa kupeleka gesi asilia kwa mabomba kutoka magharibi hadi mashariki mwa China umekamilika, yaani gesi kutoka chanzo cha Tarim mkoani Xinjiang na gesi kutoka Changqing, kaskazini mwa mkoa wa Shan'xi zimekutana kwenye kituo cha kuongeza nguvu ya kusukuma cha Jingbian mkoani Shan'xi. Kukutana kwa gesi hiyo inayotoa kutoka kwenye vyanzo viwili kumeweka msingi wa kupeleka gesi hiyo kwa pamoja kwenye eneo la mashariki tarehe mosi Oktoba.
Tarehe 11saa 6 za mchana mkurugenzi wa ofisi ya shughuli za gesi mkoani Shan'xi, Bw. Zhang Liwei, baada ya kuthibitisha alitangaza kuwa gesi kutoka Tarim, mkoani Xinjiang imefika kwenye kituo cha kuongeza nguvu cha Jingbian.
Naibu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Mabomba ya Kupeleka Gesi Kutoka Magharibi hadi Mashariki Bw. Huang Zejun alieleza kuwa tokea tarehe mosi Septemba upande wa magharibi walipoanza kusafirisha gesi kutoka Tarim, hali ilikuwa nzuri, jumla walisafirisha gesi yenye mita za ujazo milioni 8.2 na gesi hiyo ilipofika kwenye kituo cha kuongeza nguvu cha Jingbian iliongezeka hadi ujazo wa mita 140,000 kutoka 60,000 kwa saa, tokea hapo shinikizo litaongezwa, na kwa makadirio hadi tarehe mosi Oktoba nguvu ya kusukuma gesi kati ya upande wa magharibi na upande wa mashariki zitakuwa sawa, wakati huo ndipo gesi kutoka kwenye vyanzo vyote viwili itapelekwa pamoja kwenye eneo la mashariki mwa China, mjini Shanghai.
Kituo cha kuongeza nguvu cha Jingbian kiko kilomita 10 kaskazini ya mji mkuu wa wilaya ya Jingbian. Tangu tarehe mosi Oktoba mwaka jana kituo hicho kilipoanza kupeleka gesi hadi mashariki mjini Shanghai kituo hicho kilikuwa kinabeba kazi ya kusafirisha gesi kutoka Changqing kaskazini mwa Mkoa wa Shan'xi. Baada ya gesi inayotoka kutoka vyanzo viwili kukutana, kituo hicho kitakuwa kituo cha katikati cha "kupokea gesi kutoka vyanzo viwili na kupeleka mashariki kwa pamoja". Kutokana na mpango, hadi tarehe mosi Desemba, gesi itakayokuwa inapelekwa mashariki itakuwa ya Tarim tu na gesi kutoka chanzo cha Changqing itakuwa ya nyongeza.
Mabomba ya kupeleka gesi kutoka magharibi mpaka mashariki mwa China yanayoanzia Lunnan, mkoani Xinjiang, sehemu ya magharibi ya China hadi mashariki kwenye kijiji cha Baihe mjini Shanghai, yana urefu wa kilomita 4,000 na gesi ya inayopelekwa huko Shanghai ni ujazo wa mita milioni 1.2 kwa mwaka.
Idhaa ya Kiswahili 2004-09-16
|