"Upinde wa mvua hutokea kimyakimya, na kutoweka kimyakimya. Lakini uzuri wake wa muda hutuachia kumbukumbu daima?.."
Siku moja ya mwezi Aprili mwaka huu, katika mji wa Dengfeng, mkoani Henan, katikati ya China, wakazi zaidi ya laki mbili walijitokeza mitaani kwa hiari wakishika maua au kunyanyua mabango kumuaga mkuu wa kike wa polisi ya Dengfeng Bi. Ren Changxia aliyefariki dunia wakati alipokuwa kazini. Watu pia walitunga wimbo uitwao "upinde wa kudumu wa mvua" kwa ajili ya kumkumbuka afisa huyo mwanamke wa polisi.
Katika mji wa Dengfeng, mkoani Henan ambako Ren Changxia alikuwa akifanya kazi kabla kufariki dunia, hadi leo watu wengi wakitaja jina la Ren Changxia huwa hawawezi kujizuia kutokwa na machozi.
Mioyoni mwa wakazi wa kawaida wa mji wa Dengfeng, Bi. Ren Changxia ni polisi hodari, alikuwa amefanikiwa kushughulikia kesi nyingi zilizokuwa zimerundikana kwa miaka mingi na kuwachukulia hatua za kisheria wahalifu wengi.
Ren Changxia alizaliwa miaka 40 iliyopita kwenye kando ya mto Manjano, tokea utotoni mwake alipenda kujiunga na kikosi cha polisi, akiona kuwa, kazi ya polisi ni kazi nzuri sana, hivyo alijiunga na shule ya polisi baada ya kuhitimu masomo ya sekondari.
Bi. Ren Changxia aliteuliwa kuwa mkuu wa idara ya polisi ya mji wa Dengfeng mwezi Aprili mwaka 2001 baada ya kufanya kazi kwa zaidi ya miaka 10 katika idara ya polisi ya Zhenzhou, mji mkuu wa Henan, alitumwa mjini Dengfeng kutokana na uhodari na umakini wake wa kazi. Mji wa Dengfeng uko kati kati ya mkoa wa Henan, hekalu la Shaolinshi linalojulikana duniani liko huko, kila mwaka watu karibu milioni mia moja wanatembelea mji huo, hivyo hali yake ya usalama ni ya utata. Baada ya kushika wadhifa, Bi. Ren Changxia alianza mara moja kurekebisha nidhamu ya kikosi cha polisi, kuchunguza na kutatua kesi kubwa na zile zilizokuwa zimerundikana kwa miaka mingi, na kuboresha hali ya usalama wa Dengfeng. Kwa mfano alifanikiwa kutatua kesi kubwa ya kundi la Wangsong. Wang Song alikuwa meneja wa kampuni fulani, aliwaongoza watu wa familia yake na walioachiwa kutoka gerezani kuwakandamiza na kuwadhuru wakazi hata kuwaua baadhi ya watu. Bi. Ren Changxia aliwaongoza polisi kuwakamata watu wote wapatao zaidi ya 60 wa kundi la Wang Song wakienda mikoa 9 nchini China. Habari hiyo iliwafurahisha sana wakazi wa Dengfeng.
Katika miaka 3 iliyopita, si kama tu Ren Changxia alikuwa ameshughulikia kesi nyingi kubwa, bali pia amewafukuza polisi kadhaa wasio na nidhamu, na kuboresha hali ya kikosi cha polisi cha Dengfeng.
Ili kufanya uchunguzi kuhusu kesi, Bi. Ren Changxia aliwahi kujifanya mwanakijiji, mchuuzi na mtumishi. Pia alianzisha chumba cha kusikiliza mwenyewe malalamiko ya wakazi kila Jumamosi. Katika miaka 3 iliyopita, kwa jumla alikuwa amewapokea watu zaidi ya 3000, na kushughlikia kesi zaidi ya 100.
Japokuwa mji wa Dengfeng hauko mbali na maskani yake huko Zhengzhou, lakini katika miaka 3 iliyopita, Bi. Ren Changxia hakuwahi kurudi nyumbani hata mara moja wakati wa siku kuu, alikuwa anatumia wakati wake wote kazini. Mume wake Bwana Wei Xiaochun alisema kuwa, ilikuwa ni vigumu kupata nafasi kwa Ren Changxia kurudi nyumbani. Akisema :
"Kila nilipomwona alionekana amedhoofika kutokana na kazi ngumu, hasa katika mwaka wa pili na wa tatu. Nilimwambia anaonekana kama amezeeka, akanijibu kuwa ana kazi nyingi za kufanya. Mara ya mwisho kuzungumza naye ilikuwa ni siku tatu kabla yeye kufariki dunia. "
Usiku wa tarehe 14 Aprili, akiwa njiani kurudi kazini kutoka mkutanoni, Bi. Ren Changxia alikumbwa na ajali ya gari barabarani na kufa papo hapo. Habari hiyo iliwahuzunisha sana wakazi wa Dengfeng na watu wa familia yake. Siku tatu tangu yeye kufariki dunia, wakazi zaidi ya laki mbili walimiminikia mitaani. Msichana Liu Chuanyu ni mmoja kati yao. Mwaka 2001, msichana Liu mwenye umri wa miaka 10 alifiwa wazazi wake kutokana na mlipuko wa mgodi wa makaa ya mawe. Bi. Ren Changxia alimtunza msichana huyo kama binti yake, aligharimia masomo yake na maisha yake, na kumtembelea mara kwa mara. Habari ya Ren Changxia kufariki ghafla ilimhuzunisha sana, alimwomboleza mama yake kwa siku tatu. Alisema:
"Mama, sitaki uondoke namna hii, mimi nilitarajia furaha ya kukutana na wewe tena, lakini umeondoka ghafla ?"
Katika miaka 21 ya maisha yake ya kuwa polisi, Bi. Ren Changxia aliwahi kupata nishani mara tano , na kutunukiwa tuzo za sifa nyingi za heshima. Alikuwa amefuata imani ya polisi wa China ya kutekeleza kanuni za kisheria ili kuwalinda wananchi kwa vitendo.
Idhaa ya Kiswahili 2004-09-16
|