Vyombo vya vanishi ni sanaa ya jadi ya pekee ya China. Kwenye tabaka la utamaduni la tatu huko Hemudu, Wilaya la Yuyao, Jimbo la Zhejiang, kuligunduliwa bakuli kubwa la vanishi nyekundu lenye umri wa miaka 7,000. Ndani ya kaburi la Enzi ya Chu huko Zenhouyi, Wilaya ya Suixian, Jimbo la Hubei na kaburi la Enzi ya Han huko Mawangdui, Mji wa Changsha, Jimbo la Hunan, mligunduliwa idadi kubwa ya vyombo vya vanishi.
Vyombo hivi vinadhihirisha kuwa muda wa mamia ya miaka tangu Madola Yaliyopigana (475K.K.?221K.K.) hadi Enzi ya Han (206K.K.?220B.K.) ni kipindi cha ustawi kabisa cha vyombo vya vanishi. Majumba ya makumbusho ya kila taifa yanafanya bidii ya kutafuta na kuhifadhi vyombo vya vanishi vya China. Vyombo vilivyotengenezwa katika Enzi ya Yuan, Ming na Qing (1279?1911) vinatia for a kabisa.
Vanishi ni utomvu uliogemwa kutoka mipira. Kwa kuwa ina sifa ya kujikinga na unyevu, uozaji na ukwaruzwaji, hupakwa nje ya vyombo kusudi kuvilinda. Kwa upande mwingine, rangi ya vanishi inapendeza na kung'ara, kwa hivyo hutumiwa kwa kurembesha vyombo. Mafundi wa kila enzi walichemsha ubongo wao, walivumbua mtindo mmoja baada ua mwingine. Hadi zama ya leo, vyombo vya vanishi vinarithi jadi za kikalem vilevile vina ubingwa wa kisasa wa pekee.
"Samaki wa Dhahabu", sahani ya vanishi ilisanifiwa na Bwana Shen Fuwen, ambaye alivuma tangu miaka ya 1930. Kwenye karatasi nyeupe, msanii anachora samaki tu bila maji. Kwa kipaji chake, Bw. Shen pia lichora samaki bila maji kwenye sahani nyeusi. Vanishi halisi ina sifa ya kupenyeza mwanga n akuvumilia kukwaruzwa. Juu ya nakshi ya samaki mwekundum msanii alipaka vanishi halisi. Baada ya kukauka, msanii alipiga polishi kwa msasa na makaa.
Kwa vile nguvu ya kupiga polishi hutofautiana, kwa hivyo mwangaza ulionekana kwenye martabaka, na samaki anaonekana kama anazama na kuibuka.
Baada ya kutiwa rangi mbalimali, vanishi ikawa yenye rangi mbalimbali. Rangi nyekundu ni ya pili kwa umuhimu kufuatia rangi nyeusi. Wasanii wa kale walipenda sana kuitumia vanishi nyekundu katika vyombo vya vanishi. Bakuli la vanishi nyekundu ni kiwakilishi cha vyombo hivi. Bakuli hili lilitengenezwa kutokana na mti. Wakati wa kuchonga, mti hubaki milia iliyokwenda ndani na kutokea juu. Msanii hakujali milia hiyo, alipaka juu yake vanishi nyeusi kwanza, kasha nyekundu, mwisho alipiga polishi. Kazi zote zilipokamilika, milia myeusi iliyo katika huonekana juu ya vanishi nyekundu,. Mtu anahisi yzuri wa rangi na milia ni kama wa maumbile bila ya kutiwa urembo na binadamu.
Vanishi pia ina sifa ya kuganda. Wasanii hutumia vanishi kugandisha nyenzo za maumbile kwenye vyombo vya vanishi. Nyenzo hizo ni kama zifuatazo: magome ya wanyama wa baharini, maganda ya mayai, dhahabu, fedha na mawe ya thamani. Kasha la duara "Kamba Mweusi" ndilo lililotengenezwa kwa ufundi huu. Kwanza kabisa, msanii alichagua magome ya konokono, ambayo yanafanana na yale ya kamba kwa rangi na sifa nyinginezo. Aliyakata magome hayo katika vipande vipande, na kiuvigandisha katika umbo la kamba kwenye kasha.
Sanamu ya vanishi "Chui Anayetelemka kutoka Mlimani" ilisanifiwa kwa maganda ya mayai. Msanii anajali sana rangi na milia ya maganda hayo. Alivunja maganda hayo, akachagua vipande vinavyofanana na ngozi ya chui, akavigandisha juu ya gimba la chui. Chui huyu anaonekana kama yu hai.
Ufundi wa kusanifu sanaa ya vanishi bila ya gimba unatatanisha sana. Kwanza msanii anatengeneza gimba kwa jasi, udongo au mti, kasha anagandisha matabaka kadhaa ya vitambaa juu ya gimba. Baada ya vitambaa kukauka na kuwa vigumu, msanii hubandua vitambaa kutoka kwenye gimba na vitambaa hivi huchukua umbo la gimba. Wakati huu, msanii anaweza kupaka vanishi ya rangi na kunakshi juu yake.
Kasha la vanishi "Watoto Watano", nayo pia ilisanifiwa bila ya gimba. Juu ya vanishi nyekundu, msanii alinakshi kwa unga wa vanishi na kugandisha maganda ya mayai. Watoto watano wanaoungana miili, wanakaa mmoja juu ya mwingine. Kutokana na upangaji wa busara, watoto watano wanaonekana kama kumi.
"Chombo cha kuwekea kalamu" ni cha vanishi kilichongwa. Msanii anapaka matabaka ya vanishi juu ya gimba, idadi ya matabaka kwa uchache ni zaidi ya kumi, kwa wingi huwa ni mamia. Wakati idadi ya matabaka ilipotimia ile iliyotakiwa, msanii huanza kuchonga nakshi juu ya vanishi.
Vyombo vya vanishi na sanaa za vanishi vinapendwa sana siyo na Wachina tu, bali pia na wageni wa ng'ambo. Vinatumiwa kama vyombo katika maisha ya kila siku, vilevile vinarembesha vyumba au kuzawadiwa kwa marafiki.
Idhaa ya Kiswahili 2004-09-17
|