Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-22 20:13:35    
Michezo ya nyimbo na ngoma ya China (3)

cri
    Mwishoni mwa miaka ya 50, michezo ya nyimbo ya China iliendelezwa katika kipindi chake kizuri, ambapo michezo mingi zaidi ilitungwa, na sifa yao ya kisanaa pia ni ya juu sana. Michezo ya nyimbo ya "Dada Liu San" na "Dada Jiang" ndiyo iliyotokea katika kipindi hiki, na mchezo wa "Jeshi jekundu la ulinzi wa Ziwa Honghu" ni

    Mmojawapo wa michezo hiyo, ambao ulieleza jinsi wananchi walivyopambana kishupavu na tabaka la utawala wa kupinga maendeleo, ambao ulikuwa mchezo ulioenea zaidi, ulioonekana uhai mkubwa zaidi na uliopendwa zaidi na umma baada ya Mchezo wa "Msichana mwenye nywele nyeupe".

    Kwa kulinganishwa na opera za Italia, Ufaransa na nchi nyinginezo, katika michezo ya nyimbo ya China, uelezaji wa kimaneno kama ulivyofanywa katika mchezo wa kuigiza ulichukuliwa badala ya uimbaji wa usimulizi wa kiulaya, lakini ulipokewa na watazamaji wa China kutokana na desturi yao, vile vile umekuwa alama ya michezo ya nyimbo ya kitaifa ya China.

    Hivi leo uelekeo wa kurudi katika opera ya kiulaya umeonekana katika utungaji wa michezo ya nyimbo ya kichina, hali hii inatokana na juhudi kubwa za wasanii wa China katika kutafuta aina mwafaka ya kitaifa ya michezo ya nyimbo ya China. Wasanii hao wanaona kwamba, kwa kiwango cha manedeleo ya opera, michezo ya nyimbo ya Ujerumani, Ufaransa na Russia iliyotokana na opera ya Italia, yote imeshapevuka baada ya kipindi cha mwanzo, na sasa michezo ya opera ya nchi hizo inaweza kulingana kisanaa na opera ya Italia. Na michezo ya nyimbo ya China ikitakiwa kupevuka na kupata mafanikio yenye kung'ara, kwanza lazima kuifanya michezo hiyo iwe na ukamilifu wake wa kimuziki. Katika miaka kadha iliyopita, michezo ya "Malisho yenye majani kibichi" na "Mbuga" iliyovutia sana watu ilionyeshwa kwenye jukwaa la michezo ya nyimbo ya China, michezo hiyo ilipodumisha desturi ya uburudishaji wa watazamaji wa China ilifanikiwa katika utungaji wa muziki wa kimfululizo na wa ukamilifu, na siyo kusema tema maneno kwa kueleza hadithi halafu kuimba, ama kuimba aya moja moja kwa njia rahisi.

    Katika chuo kikuu cha muziki cha China, chuo kikuu cha ngoma cha Beijing na vyuo vingine vya usanii, wako wanafunzi watokao mikoa mbalimbali ya China yenye mila zinazotofautiana, wote wanajifunza kwa makini michezo ya ngoma na nyimbo na sanaa na utamaduni wa nchi za nje. Wasanii kadha wa kadha ambao ingawa wamezidi umri wa miaka 60, lakini wangali bado wanajitahidi kuwaandalia wasanii wa kizazi kipya wa michezo ya nyimbo ya China. Juhudi zao zimeifanya michezo ya nyimbo ya China iendelezwe siku hadi siku, ambapo michezo mingi mizuri imewashangaza watazamaji na kupokelewa na watu wengi zaidi kuliko hapo awali, hali hii imeonyesha kwamba sanaa ya nyimbo na ngoma ya China inasitawishwa katika hali motomoto.

    Hakuna mtu anayeweza kutarajia kwamba, michezo ya ngoma na nyimbo iliyotoka nchi za nje miaka 70 au 80 illiyopita ingeweza kuendelezwa namna hii nchini China. Kwa wachina, michezo ya nyimbo na ngoma haiwi tena na maana ya opera ya kiulaya, michezo hiyo imekuwa sanaa moja ya China yenye tabia ya kitaifa iliyooana na sanaa ya nchi za nje ambayo inaonekana sura yake mpya.