Ili kuadhimisha miaka 40 ya waziri mkuu wa zamani wa China marehemu Zhou Enlai kufanya matembezi barani Afrika, shirikisho la urafiki kwa nje la watu wa China na kituo cha televisheni cha Beijing hivi karibuni vimetengeneza kwa pamoja filamu ya televisheni yenye sehemu 10 iitwayo "Safari ya Urafiki". Filamu hiyo imeonesha tena historia ya ziara aliyofanya waziri mkuu wa zamani wa China marehemu Zhou Enlai katika nchi 10 za Afrika kabla ya miaka 40 iliyopita, kukumbusha mchakato wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na nchi za Afrika katika miaka 40 iliyopita.
Ndugu wasikilizaji, mnayosikia sasa hivi ni kipande cha muziki mkuu wa filamu "Safari ya Urafiki". Tarehe 23 mwezi Agosti, tamasha la urafiki kati ya China na Afrika yaani mkutano na waandishi wa habari kuhusu filamu "Safari ya Urafiki" ulifanyika mjini Beijing, ambapo wajumbe zaidi ya 150 wakiwemo wanadiplomasia na mabibi zao kutoka nchi zaidi ya 30 za Afrika nchini China zikiwemo Misri, Cameroon na Algeria, na mabalozi wa zamani wa China katika nchi za Afrika walihudhuria mkutano huo, wakizungumza kwa furaha urafiki kati ya China na nchi za Afrika.
Mkurugenzi wa shirikisho la urafiki wa watu wa China na nje
Mkuu wa shirikisho la urafiki kwa nje la watu wa China Bw. Chen Haosu alipohutubia tamasha hilo alisema kuwa, mwaka huu ni mwaka wa urafiki kati ya China na Afrika, shirikisho la urafiki kwa nje la watu wa China litafanya shughuli za aina mbalimbali kuhusu urafiki wa China na Afrika, kutengeneza filamu "Safari ya Urafiki" ni moja ya shughuli hizo.
Mkuu wa kituo cha televisheni BTV
Kutoka mwezi Desemba mwaka 1963 hadi mwezi Februari mwaka 1964, aliyekuwa waziri mkuu Zhou Enlai na naibu waziri mkuu, ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje Chen Yi waliongoza ujumbe wa serikali ya China kukanyaga kwa mara ya kwanza barani Afrika, wakifanya ziara ya kirafiki kwa nchi 10 za Afrika, ambazo ni Misri, Algeria, Comoro, Tunisia, Ghana, Guinea, Mali, Sudan, Ethiopia na Somalia. Ziara hii si kama tu ilikuwa imeanzisha enzi mpya ya kihistoria ya uhusaino kati ya China na nchi za Afrika, bali pia imeweka jiwe imara ya msingi kwa China kurudishwa kiti halali kwenye Umoja wa Mataifa mwaka 1971.
Katika matembezi yao, waziri mkuu marehemu Zhou Enlai alitoa kanuni tano za China kushughulikia uhusiano kati yake na nchi za kiarabu, na kanuni 8 za China kutoa misaada kwa nchi za nje. Alikuwa amewafahamisha binadamu udhati wa serikali ya China katika kufanya ushirikiano, maendeleo ya pamoja, kulinda amani, kutafuta maoni ya aina moja na kuwepo kwa maoni tofauti na nchi nyingine. Wakati huo huo, mienendo yake ya kidiplomasia yenye unyumbufu na busara ilikuwa imewapa watu wa Afrika picha nzuri sana, ambayo imeleta athari kubwa kwa kuendeleza urafiki wa kijadi kati ya watu wa China na watu wa Afrika.
Mkuu wa kundi la mabalozi wa Afrika
Mkuu wa kituo cha televisheni cha Beijing Bwana Liu Ming alijulisha hali ya utengenezaji wa filamu "Safari ya Urafiki" akisema:
"Kikundi cha wanafilamu cha 'Safari ya Urafiki' kilifunga safari mwezi March mwaka huu kwenda barani Afrika, walipiga filamu na kufanya mahojiano wakifuatana na nyayo za marehamu Zhou Enali alivyotembelea." Kikundi cha wapigaji filamu kimetembea kwa kilomita zaidi ya elfu 40, walikuwa wamewahoji viongozi zaidi ya kumi wa nchi za Afrika akiwemo rais wa Ghana, na walioshuhudia ziara ya marehemu Zhou Enali, miongoni mwao ni msichana wa Misri aliyempa hayati Zhou Enlai shada la maua, mtangazaji wa kituo cha radio cha Ghana, mwandishi habari wa Guinea na kadhalika. Kikundi cha wapigaji filamu pia walipiga picha kwenye mtaa wa Beijing nchini Algeria, bandari la Port Said la Misri waziri mkuu Zhou aliwahi kutembeela, kiwanda cha kutengeneza mafuta cha Sudan, kiwanda cha nguo cha Mali na miradi mingine ambayo ni mifano ya kuigwa katika ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika.
Ndugu wasikilizaji, kabla ya miaka 40 iliyopita, ziara ya marehemu Zhou barani Afrika imeweka jiwe imara la msingi kwa urafiki kati ya China na nchi za Afrika. Baada ya miaka 40, urafiki na ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika umepata maendeleo makubwa chini ya hali mpya, na kupewa mambo mapya ya kisiasa na kiuchumi. Kama mkuu wa ujumbe wa mabalozi ya Afrika nchini China, ambaye pia ni balozi wa Cameroon nchini China Bwana Eleih Elle Etian alivyosema kuwa, viongozi wa China siku zote wanatia maanani uhusiano wa kirafiki na ushrikiano kati yake na nchi za Afrika, kwa upande mwingine, nchi za Afrika pia zinazingatia sana kukuza uhusiano na China. Alisema:
"Katika eneo la siasa, chama cha kikomunisti cha China kinadumisha uhusiano wa aina mbalimbali na vyama 50 vya kisiasa vya nchi 40 za Afrika. China na nchi za Afrika zinasaidiana na kuungana kwenye jukwaa la kimataifa. Tangu kufanyika mkutano wa pili wa mawaziri wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika umeingia katika kipindi kipya. Uhusiano kati ya China na Afrika una matumaini makubwa na mustakabali mzuri."
Idhaa ya Kiswahili 2004-09-24
|