Mchezo wa kivuli pia unaitwa "mchezo wa kovuli cha taa". Mchezo huu unachezwa hivi: msanii anamulika mwangaza wa taa kwenye ngozi za wanyama zilizokatwa katika maumbo ya binadamu, wanyama au vitu vingine, na kuonyesha vivuli vya maumbo hayo kwenye pazia. Ngozi hizo ni nyembamba na hutiwa rangi mabalimbali za kupendeza. Msanii anachezesha ngozi huku akifauta muziki au mazungumzo ya wahusika. Ngozi za maumbo huchezeshwa kwa mfululizo, kwa hivyo kwenye pazia zinaweza visa mbalimbali.
Jimbo la Shaanxi ni chimbuko la sanaa ya mchezo wa kivuli. Kwa mujibu wa kitabu cha historia, mchezo huo ulianza mapema karne ya 11 K.K., na kustawi sana katika Enzi ya Sui (581-618) na Enzi ya Tang (618-907). Sanaa ya mchezo wa kuivuli inagawanyika katiak madhehebu ya mashariki na magharibi.
Mrithi wa sanaa ya madhehebu ya magharibi ni Bwna Chen Xiuwen, ambaye alizaliwa mwaka 1958 katika ukoo wa mkulima wa Wilaya ya Longxian, Shaanxi. Ukoo wake umeshughulikia sanaa hiyo kwa vizazi vitatu. Babu mkuu wake alikuwa hodari wa kukata ngozi za maumbo na kuonyesha mchezo wakivuli. Alikuwa tajiri wa kikundi cha mchezo.
Baba yake, Chen Zhaoxian alikuwa mwakilishi wa wasanii wa madhehebu ya magharibi. Katika kipindi cha miaka 40, alikata ngozi 3,000 zenye maumbo ya aina kemkem, ambazo zilionekana kuwa na ubingwa mkubwa na hali ya juu. Mwaka 1956, ngozi zake zilipewa tuzo katika Mashindano ya Kwanza ya Vikaragosi na Mchezo wa Kivuli ya Shaanxi. Mwaka 1987, ngozi zake 150 zilichukuliwa na kuhifadhiwa katiak Jumba la Sanaa la China, mwaka 1989 aliorodheshwa katiak kitabu "Wasanii Mashuhuri wa Kienyeji wa China".
Bw. Chen Xiuwen alianza kujifunza ukataji wa ngozi za maumbo kutoka kwa babaye tangu utotoni mwake. Ustadi wake umekomaa baada ya yeye kuwa mkubwa, sasa ni gwiji wa sanaa ya mchezo wa kivuli. Ana uhodari wa kutumia rangi, kusanifu maumbo ya wahusika, kurembesha nakshi, kutumia visu kwa makini na kwa mistari myepesi na kupiga chuku.
Kwa miaka 20 sasa, ngozi za maumbo alizokata zimevuka 600, ziliuzwa Japani, Ufaransa na marekani, pia zimehifadhiwa katika taasisi na majumba ya sanaa ya manispaa na majimbo ya nchini.
Idhaa ya Kiswahili 2004-09-24
|