Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-10-08 18:07:33    
Umoja wa Mataifa walipa nishani jeshi la ulinzi wa amani la China nchini Libeira.

cri

    Tarehe 14, Septemba, kwenye makazi ya askari wa uhandizi wa China yaliyopo umbali wa kilomita 470 mashariki ya Monrovia, mji mkuu wa Liberia, askari 500 wa ulinzi wa amani wa China walikuwa wakipokea "nishani ya heshima ya amani" iliyotolewa na Umoja wa Mataifa.

    Hiyo ni nishani iliyotolewa na Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Libeira kwa jeshi la ulinzi wa amani la China nchini humo. Kwenye sherehe ya utoaji wa nishani, naibu mwakilishi wa katiub mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni naibu mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa Tume maalum ya Umoja wa Mataifa Bw. Solon Saridarian alitoa hotuba akisifu sana mchango mkubwa uliotolewa na jeshi la China katika ulinzi wa amani ya Liberia.

    China imepeleka askair 558 wa ulnzi wa amani nchini Liberia. Kuanzia tarehe 10, Desemba, mwaka 2003, askari hao walipelekwa nchini humo kwa vikundi vitatu, na kutekeleza kazi ya kulinda amani ya dunia.

    Katika muda usiozidi mwaka mmoja, kutokana na zana za kisasa, nia imara, kiwango cha juu cha ufundi na nidhamu nzuri, jehsi la ulinzi wa amani la China lilipata sifa kutoka kwa serikali ya Liberia, wananchi wake na majeshi mengine ya ulinzi wa amani.

    Katika muda wa miezi kadhaa, kikundi cha askari wa uhandisi kilipata mafanikio makubwa. Kiliifanyia ukarabati barabara mbovu yenye urefu wa kilomita 660, kujenga madaraja matatu ya chuma cha pua, 18 ya mbao, na viwanja vitatu vya helikopta. Kikosi cha uchukuzi cha jeshi hilo kilisafirisha watu 65,580, na tani 12,000 za mizigo. Mbali na hayo, kikosi cha tiba cha jeshi hilo kilitoa huduma za matibabu kwa askari wa ulinzi wa amani na wenyeji wa huko 2000.

    Tarehe 4, Mei, kikosi cha uhandisi cha jehsi la China kilipata amri ya kujenga kambi la kusalimisha silaha. Ingawa kilikabiliana na mazingira yasiyo mazuri, katika muda mfupi, askari hao walifanikiwa kujenga kambi hilo lenye eneo la mita za mraba laki 5.9 katika mazingira safi yenye zana zilizokamilika na ulinzi mkali wa usalama. Mbali nahayo, walijenga barabara zenye urefu wa kilomita 28, viwnaja viwili vya helikopita, na zana za utoaji wa umeme na maji. Kambi hilo linaweza kutoa huduma kwa maisha na elimu ya maelfu ya watu, na kutekeleza kazi ya kusalimisha silaha na kuteketeza risasi.

    Mafanikio ya ujenzi huo wa haraka na wa kiwango cha juu yamemfurahisha sana kamanda mkuu wa Ujumbe maalum wa Umoja wa Mataifa aliyekagua kambi hilo Jenerali Opande, alisema kuwa, kazi nzuri ya askari wa uhandisi wa China katika ujenzi huo umetusaidia kukamilisha vizuri mpango wetu. Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mwenyekiti wa Tume maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia Bw. Klain pia alimwandikia barua mkuu wa kikosi cha askari wa uhandisi cha China kueleza shukurani kwa mchango mkubwa uliotolewa na askari wa uhandisi wa China katika vitendo vya ulinzi wa amani nchini Liberia.

    Kikosi cha uchukuzi cha jeshi la ulinzi wa amani la China kinachoundwa na askari 240 kiliwasili nchini Liberia tarehe 10, Desemba, na tarehe 20, Machi, mwaka 2003, na kuanza kufanya kazi ya uchukuzi nchini humo.

    Kikosi hicho kilionesha uvumilivu mkubwa bila kujali matatizo yoyote, na kuanzisha urafiki mkubwa na majeshi ya ulinzi wa amani ya Pakistan, Bangladesh, Nigeria na Namibia yaliyoko huko.

    Kazi ya kikundi cha uchukuzi cha ulinzi wa amani cha China nchini Liberia ni kutoa huduma z auchukuzi kwa majeshi yote ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa. Mkuu wa kikundi hicho Bw. Shen Gangfeng aliwataka askari wote kueneza mbegu ya amani na urafiki katika njia yake ya kutekeleza kazi ya ulinzi wa usalama.