Han Zengqi ni msanii maarufu wa kufinyanga sanamu za udongo mjini Beijing. Nyumba yake ni ndogo, lakini ndani kunakaliwa na "maelfu ya askari na farasi", juu ya kitanda na meza kumejaa "wapanda farasi" waliokwishafinyangwa na kwenye ua sanamu za udongo za watu na farasi zimepangwa mstari baada ya mstari juu ya vipande vya mbao kusudi zikaushwe kwa upepo.
"Wapanda farasi" ni sifa ya sanamu za udongo alizofinyanga Han Zengqi, kwa sababu karibu sanamu zote za udongo alizofinyanga ni za wapanda farasi. Watu wa ukoo wa Han walikwishafinyanga sanamu za wapanda farasi kwa miaka zaidi ya mia moja. Watu wa ukoo wa Han ni watu wa Kabila la Wamongolia. "Mukedenga, babu yangu, alifika Beijing wakati askari wa Enzi ya Qing walipovamia sehemu za kusini ya Ukuta Mkuu na baadaye alianza kufinyanga sanamu za udongo ili kupata riziki ya kila siku. Baba yangu Han Mingshun alikuwa na ustadi wa hali ya juu wa kufinyanga sanamu za watu za udongo. Mimi ni kikazi cha tatu cha kufinyanga sanamu katika ukoo wetu, nimekwishafinyanga sanamu za udongo kwa maisha sitaki kuacha kufinyanga." Han Zengqi alisema.
Udongo mwekundu wa mfinyanzi unapatikana tu kwenye sehemu ya kina cha mita zaidi ya kumi chini ya ardhi. Zamani Beijing walikuwepo watu waliokuwa wakitembeza udongo wa aina hiyo mitaani; hivi sasa ni shida kupata udongo huo, isipokuwa watoto wanaupata kutoka mahali pa ujenzi au mahali panapochimbwa mitaro. Kabla ya kufinyanga sanamu, kwanza Han Zengqi huutosa udongo mwekundu wa mfinyanzi kwenye maji na kuchuja mchanga uliomo ndani ya udongo. Akisha kuutoa udongo huo kutoka majini, huupigapiga, halafu huanza kufinyanga sanamu, huzichoma kwa moto mpaka zinapata rangi. Han huanza kufinyanga farasi asubuhi; mpaka farasi anapokauka kiasi, ndipo anapoendelea kufinyanga mpandaji. Asipofuata utaratibu huu, mpandaji ataharibu farasi kutokana na uzito wake.
Msanii Han ana kipaji cha ubunifu na ni hodari wa kufinyanga. Anapoanza kufinyanga sanamu hana taswira, mfano, wala kalibu; mikono yake myepesi inafinyanga sanamau kama mawazo yanavyomjia. Kwa muda mgfupi tu, udongo ulioko kwenye meza unageuzwa kuwa sanamu za farasi wenye meza unageuzwa kuwa sanamu za farasi wenye maumbo mbalimbali. Han anaweza kufinyanga sanamu za aina mbalimbali k.v. wahusika wa opera, watu walioko kwenye sherehe za arusi au shughuli za mazishi, wachezaji wa milonjo na hata magari.
Miaka ya karibuni, kwa mujibu wa hadithi ya "Historia ya Madola Matatu", Msanii Han alifinyanga seti ya sanamu za "Vikosi vya Madola Matatu" ambayo ina wahusika zaidi ya 370. Seti hiyo ya sanamu imeonyesha vizuri hali ya ukakamavu wa vikosi vya madola ya Wei, Shu ma Wu. Seti hiyo ilipelekwa katika Maonyesho ya Sanaa Jadiia wakati wa Tamasha la Kwanza la Sanaa ya China mnamo mwaka1987, na vilevile ilionyeshwa mara mbili huko Japani na ilipendwa sana na watazamaji wa Japani.
Katika kazi yake makini na ya uangalifu, Han alifinyanga sanamu za wahusika wenye tabia tofauti na dhahiri (k.v. Zhang Fei anayechukia maovu, Zhuge Liang mwenye hekima nyingi, Cao Cao anyeonekana ni mtu mkubwa na Zhou Yu hodari mwenye ukakamavu) ambazo zinawapa watazamaji kumbukumbu imara.
Han Baocai, mwana wa Han Zengqi, pia amekuwa shabiki wa kufinyanga sanamu za wapanda farasi na amekuwa kikazi cha nne cha sanaa ya ufinyanzi katika ukoo wa Han.
Idhaa ya Kiswahili 2004-10-08
|