Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-10-11 21:24:04    
Vivutio vya Wenzhou

cri

   

    Wenzhou ni mji wa kale uliostawi kibiashara tokea miaka 1300 iliyopita, lakini ustawi wake umekuwa mkubwa zaidi katika miaka 20 ilipita kutokana na China kufanya mageuzi. Mji huo unajulikana sana kwa sanaa za mikono na bidhaa zake zilizoenea kote nchini China. Huu ni mmoja kati ya miji inayostawi ya China.

    Ukitembea barabarani na vichochoroni utaona maduka yalijaa yakionesha ustawi wa biashara mjini humo. Kama miji mingine ilivyo, pamoja na uchumi unavyoendelea, sura ya mji pia inabadilika haraka, sasa kuna majumba marefu, barabara pana zinazofika kila mahali, uwanja mkubwa na jumba la makumbusho.

    Licha ya kuona kuwa huu ni mji wa kisasa, utagundua pia utamaduni wake mkubwa wa kale.

    Vinyago na utarizi mjini Wenzhou ni sanaa za mkono zinazojulikana nchini China na zinavutia watalii.

    Vinyago vya Wenzhou vinachongwa kwa mbao ngumu yenye rangi ya manjano. Kutokana na mti wa aina hiyo unakua taratibu sana, mbao zinazofaa kuchonga vinyago vikubwa ni shida kupatikana. Mchonga vinyago Bw. Ye Xiaoquan alisema,

    "Kutokana na shida ya kupata mbao kubwa, vinyago vyetu huwa ni vidogo, kuanzia miaka ya 80 ya karne iliyopita tulianza kuagiza mbao kutoka sehemu nyingine, tulipoanza kuchonga vinyago vikubwa kwa ukubwa wa mbao."

    Madukani kuna mitindo miwili ya vinyago, moja ni mtindo wa kiasili ambao unfalingana na vitu vilivyoigwa. Vinyago vya mtindo huo vinachongwa kwa makini hata pindo za nguo zinaonekana vizuri. Vinyago vya mtindo mwingine vinachongwa kwa kutiwa chumvi, ambavyo vinachongwa kwa kuonesha hisia tu na vitu vilivyoigwa vinatiwa sana chumvi. Fundi mzee Gao Gongbo alisema,

    "Mtindo wa kwanza unafuatilia mfananisho wa vitu halisi, huu ni mtindo wa kijadi. Mtindo wa pili unafuatilia mfananisho wa kijujuu na kutiwa sana chumvi, huu ni mtindo wa kisasa.

    Baada ya kuwafahamisha sanaa za Wenzhou, sasa tunawapeleka katika sehemu nyingine yenye mandhari ya kimaumbile na utamaduni wa kale.

    Katika wilaya ya Yongjia, kiasi cha kilomita 20 nje ya mji, kuna mto wenye maji maangavu, kando mbili za mto huo kuna vijiji zaidi ya 200, nyumba nyingi za wanavijiji ni nyumba zilizojengwa katika enzi za Ming na Qing, kati ya vijiji hivyo kijiji cha Yantou ni kikubwa zaidi.

    Ndani ya kijiji hicho unapita mto mdogo. Ingawa mto huo umekuwa na zaidi ya miaka 500, lakini maji ni mengi na safi. Hiki ni kijiji pekee kilichokuwa na maduka katika siku za kale. Kuna barabara moja nyembamba ambayo ilifunikwa kwa paa ili wateja wasirowe na mvua na kukimbia jua. Hii ni barabara ya kibiashara. Mwanakijiji Jin Kecun alieleza,

    "Kijiji chetu kiliwahi kuwa njia ya wafanyabiashara wanaotoka vijiji vya kusini kwenda mji wa Wenzhou. Kutokana na wafanyabiashara wengi kupita hapa, barabara hii imekuwa ya kibiashara mpaka leo."

    Mandhari nzuri ya vilima na maji, mashamba na maduka ya kale yanavutia watalii. Mtalii kutoka Marekani Bi. Davies alisema,

    "Mandhari ya hapa inanivutia kweli. Ni jambo la maana kuwa wenyeji kuishi kwenye nyumba za kale huku wanazitunza. Hii ni njia nzuri ya kuhifadhi kumbukumbu za kale."

Idhaa ya Kiswahili 2004-10-11