Mtaa wa Zhong Guan Cun mjini Beijing ni kituo cha Wanafunzi wa China waliosoma ng'ambo kuvumbua miradi ya sayansi na teknolojia ya juu. Katika miaka ya karibuni, wanafunzi wa China waliosoma ng'ambo wamevumbua miradi mingi yenye ushindani mkubwa duniani.
Katika miaka zaidi ya 20 iliyopita Wachina karibu laki nne walitoka nchini na kwenda kusoma ng'ambo, kutokana na jinsi uchumi unavyoendelea nchini China watu hao wengi wanarudi kwa ajili ya kuvumbua miradi nchini.
Kutokana na takwimu, hadi sasa wanafunzi wa China waliosoma ng'ambo wapatao 5000 wamewahi kuvumbua miradi ya sayansi na teknolojia ya juu katika mtaa Zhong Guan Cun. Mashirika yaliyoanzishwa na watu hao yanachukua karibu 20 ya mashirika yote nchini China, na bidhaa mpya walizovumbua za sayansi na teknolojia ya juu kwa wastani zinafikia mia kadhaa kila mwaka.
Ili kuhamasisha watu kufanya kazi za uvumbuzi, mkutano wa kutangaza ufanisi wa utafiti wa bidhaa unafanyika kila baada ya muda fulani na kuwajulisha mawakala na wawekezaji. Katika mkutano uliofanyika siku chache zilizopita bidhaa za aina kumi kadhaa zilizovumbuliwa na wanafunzi waliosoma ng'ambo zilitangazwa. Bidhaa hizo zinahusika na tetemeko la ardhi, vifaa vya matibabu, dawa, utafutaji wa madini na hifadhi ya mazingira.
Kati ya bidhaa hizo, moja ni kifaa cha utabiri wa tetemeko la ardhi, ambacho kinaonesha dalili isiyo ya kawaida ya hali ya maumbile na shughuli za viumbe, mvumbuzi wa kifaa hicho Bi. Sun Xiaoming alisema kuwa kifaa hicho kimefanikiwa mara kadhaa kutoa dalili kabla ya tetemeko la ardhi kutokea, alieleza,
"Sasa, tumeweka kifaa hicho katika sehemu nne: Beijing, mkoani Liaoning (kaskazini mwa China) na San Francisco. Kifaa hicho kilitoa dalili kabla ya tetemeko la ardhi kutokea kisiwani Taiwan, mkoani Qinghai na Tibet."
Utabiri wa tetemeko la ardhi ni tatizo gumu ambalo mpaka sasa halijatatuliwa duniani. Wataalamu wanaona kuwa kifaa hicho cha akina Sun Xiaoming kitasaidia sana utatuzi wa tatizo hilo.
Mafanikio mengine ni "maji-nguvu" (powerwater). Maji hayo yana nguvu kuondoa uchafu, sumu, kuua bacteria, na baada ya kutumika yanaweza kurudishwa kuwa sawa na maji ya kawaida kama hapo awali, kwa hiyo hayaleti uchafuzi wowote. "Maji-nguvu" yanaweza kunywewa na biandamu baada ya kuzimuliwa, na yanasaidia kuondoa sumu na bacteria mwilini. Teknolojia hiyo ya kugeuza maji ya kawaida kuwa ya "maji-nguvu" ni mpya kabisa duniani.
Kwenye mkutano wa kutangaza mafanikio ya utafiti, teknolojia hiyo iliwavutia sana mawakala na wawekezaji wengi. Mtafiti wa teknolojia hiyo Liu Junqing alisema,
" 'Maji-nguvu' yanafaa kutumika katika idara za huduma kama hospitali kwa ajili ya kuua vijidudu. Sasa mashirika manane yamekuwa na hamu kubwa ya kupata nafasi za kuyauza"
Katika mtaa wa Zhong Guan Cun, bidhaa zenye hali ya juu ya kisayansi na kiteknolojia zilizovumbuliwa na kutengenezwa na watu waliorudi nyumbani China baada ya kusoma katika nchi za nje. Bidhaa hizo zinafuatiliwa sana na mashirika ya nje ya uwekezaji vitega uchumi na kupata mitaji mingi. Kila siku mashirika kadhaa ya nchini na nje ya uwekezaji vitega uchumi huja kutembelea mtaa wa Zhong Guan Cun, kufanya ukaguzi na kuwa na hamu kubwa za kuwekeza vitega uchumi katika mtaa huo.
Kundi la Kimataifa la Tarakimu la Marekani (IDG) wakati wote linafuatilia uvumbuzi wa mtaa Zhong Guan Cun, na limewekeza katika miradi mingi. Meneja mkuu wa kundi hilo Bw. Li Jianguang alisema,
"Tumewekeza mashirika jumla 30 mjini Beijing na kati ya mashirika hayo kila moja lilianzishwa kutokana na mafanikio ya utafiti mtaani humo na kila shirika linapata faida. Kwa hiyo mtaa huo unatuvutia sana sisi wawekezaji." Aliongeza kuwa tovuti ya internet ya Sohu iliwekezwa na kundi hilo, faida zake zimekuwa zikiongezeka haraka katika miaka ya karibuni.
Kuhusu sifa za Wanafunzi waliosoma ng'ambo, afisa wa mtaa huo Bi. Zhang Xioying alisema,
"Watu hao ni hodari wa uvumbuzi, wamevumba bidhaa nyingi zilizokosekana na zinazohitajika katika soko la China."
Bi. Zhang alieleza kuwa mtaa huo wa syansi na teknolojia uko karibu na vyuo vikuu maarufu vya Beijing, Qinghua na vingine kumi kadhaa. Vyuo vikuu hivyo ni chimbuko la watu hodari, wakiwa ni pamoja na wanafunzi waliosoma ng'ambo ambao wanafahamu hali ya sayansi na teknolojia ya kisasa ilivyo duniani, mtaa huo umejaa uchangamfu na kuwa wa maendeleo.
Wasikilizaji wapendwa, mlikuwa mkisikiliza maelezo kuhusu Mtaa Zhong Guan Cun Mjini Beijing, Kituo cha Wanafunzi wa China Waliosoma Ng'ambo Kuvumbua Miradi ya Sayansi na Tenkonojia ya Juu, hadi hapo ndio kwa leo tumekamilisha kipindi hiki cha elimu na afya, ni mtangazaji wenu Pomboo, asanteni kwa kutusikiliza.
Idhaa ya Kiswahili 2004-10-13
|