Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-10-27 18:15:09    
Profesa Wang Zhigong-Mtaalamu wa sayansi ya mwanga na electroniki wa China

cri

    Bw Wang Zhigong na wanafunzi wake

    Bw. Wang Zhigong aliyetoa mchango katika maendeleo ya simu ya mkononi ya China. Hivi sasa nchini China, simu za mkononi imekuwa ni kitu cha lazima katika maisha ya watu wa kawaida. China imekuwa na CMOS CHIP ya simu za mkononi yenye haki ya elimu ya China. Miaka 10 iliyopita, simu za mkononi zilipoingia nchini China, wakati ule, China haikuwa na uwezo wa kutengeneza CMOS CHIP ya simu za mkononi, lakini leo China inaweza kutengeneza simu za mkononi kwa nguvu yake yenyewe. Profesa Wang Zhigong ni mkuu wa kundi la China la kutafiti CMOS CHIP ya simu za mkononi.

    Profesa Wang Zhigong mwenye umri wa miaka 50. alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dongnan cha Nanjing, mkoani Jiangsu. Mwaka 1984, alichaguliwa kuendelea na masomo yake katika Chuo Kikuu cha Ruhr Bochum nchini Ujerumani, alikuwa mwanafunzi wa Profesa Robert Bosch ambaye ni "mwanzilishi wa sayansi ya vifaa vidogo vya umeme wa Ujerumani" na mtaalamu maarufu wa vifaa vidogo vya umeme duniani. Bw. Wang alipofika Ujerumani alishiriki kwenye utafiti na Profesa Bosch, baada ya miezi mitatu tu, mafanikio makubwa yalipatikana katika utafiti wao, Bw. Wang alisifiwa na Profesa Bosch. Yeye ni mwanafunzi wa kwanza wa shahada ya udaktari wa Profesa Bosch, na pia ni mwanafunzi wake pekee kutoka China.

    Katika majira ya joto ya mwaka 1990, Bw. Wang alipata shahada ya udaktari. Chini ya ushauri wa Profesa Bosch, alikuwa anapata mafunzo ya baada ya shahada ya udaktari katika taasisi ya fizikia ya Freiburg, kusini mwa Ujerumani. Baada ya hapo, Bw. Wang alifanya kazi kubwa katika miradi mitano ya serikali ya Ujerumani, CMOS chip alizozipanga zilitumiwa na kampuni kubwa za Marekani, Ujerumani katika maeneo ya mawasiliano na utafiti wa anga ya juu.

    Mwishoni mwa miaka ya 90 ya Karne iliyopita, Bw. Wang aliacha kuishi na kufanya kazi nchini Ujerumani, pia alikataa mwaliko wa kampuni ya Marekani wenye malipo makubwa na kurudi China. Alisema, kurudi China na kuwafundisha wanafunzi wa China ni kazi yake muhimu.

    " sasa ninafanya kazi nchini China, naweza kuwaandaa wanafunzi wengi na wanaweza kutoa mchango zaidi, hii inanifanya nijivune sana."

    Kutokana na maoni hayo, Bw. Wang alirudi katika Chuo Kikuu cha Dongnan mjini Nanjing. Wakati huo kiwango cha njia kubwa za mawasiliano nchini China kilikuwa katika kipindi cha mwanzo, mahitaji ya vifaa vya IC(mfumo muhimu wa mawasiliano) yalifikia bilioni 12, na aina za IC zilizohitajika zilifikia elfu 10, lakini wakati ule China iliweza kutengeneza aina 300 tu. Vifaa vingi vya elektroniki vilipaswa kuagizwa kutoka nchi za nje. Bw. Wang aliona kuwa, kazi ya kutafiti IC yenye haki miliki ya China haiwezi kusubili. Anasema:

    " kutokana na msaada wa serikali na vyuo vikuu, tulinunua vyombo na mitambo mbalimbali, tulianzisha kundi la utafiti, hadi sasa tumekuwa na maabala ya majaribio ya kiwango cha juu nchini China."

Baada ya muda mfupi, kundi la utafiti la Bw. Wang lilifaulu kutengeneza mfumo muhimu wa mawasiliano wenye uwezo mkubwa, wataalamu wa sayansi ya mwanga wa mpango wa maendeleo ya sayansi na teknolojia ya hali ya juu ya China walisema kuwa, matokeo ya utafiti ya Bw. Wang yamefikia kiwango cha juu duniani. Profesa Huang Jiang wa Chuo Kikuu cha Dongnan alisema:

    " utafiti wa Profesa Wang Zhigong uko mbele katika sayansi ya " mfumo wa mawasiliano duniani."

    Lakini, Bw. Wang hakuridhika na matokeo yake, aliona kuwa, matokeo yake makubwa yaliyopatikana baada ya kurudi China ni kuanzisha kikundi cha utafiti. Katika miaka 5 iliyopita, aliandaa wanafunzi 28 wa shahada ya pili na 16 wa shahada ya udaktari.

    Bi Xu Lichao ni mmoja katika kikundi cha utafiti cha Profesa Wang, anafurahi sana kufanya kazi katika taasisi ya Profesa Wang na kupata mafanikio mbalimbali ya utafiti bila kusita, anasema: 

    " chini ya uongozi wa Profesa Wang, taasisi yetu ina watafiti zaidi ya 80, tumeweka msingi mzuri wa kuiwezesha China kushiriki kwenye ushindani wa shughuli za mawasiliano duniani."

    Profesa Wang anaamini kuwa, mwenye CMOS chip nzuri duniani atapata faida kubwa duniani, atakuwa mkuu katika jamii ya mawasiliano ya kisasa. Pia ana matumaini kwamba, baada ya miaka 5 au 10, ataandaa kikundi cha utafiti chenye watu wengi, ili kuiwezesha China kuwa mbele katika shughuli za vifaa vidogo vidogo vya umeme na vifaa vyepesi duniani, hili ni lengo linalomfanya awe na juhudi katika maisha yake.

Idhaa ya kiswahili 2004-10-27