Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-03 17:06:52    
Kuthibitisha michoro ya kale kwa sayansi na teknolojia

cri
Nchini China, kuthibitisha michoro ya kale siku zote ni utaalam wanaoshika watu wachache. Wataalamu wanaotofautisha michoro halisi ya kale na ya bandia kutokana na uzoefu wa miaka mingi. Ingawa utaalamu wao ni mzuri sana, lakini hawawezi kuthibitisha bila kufanya makosa. Hivyo kutafuta njia mpya ya kisayansi ya kutofautisha michoro ni ndoto ya wapenzi wa kukusanya vitu vya sanaa. Katika miaka ya hivi karibuni, mitambo inayothibitisha michoro ya kale ya kichina ilitengenezwa mjini Beijing, mitambo hiyo imefuatiliwa sana na wapenzi wa kukusanya vitu vya sanaa.

Mitambo hiyo inatoa mwanga juu ya michoro na kupata takwimu za rangi na karatasi, halafu inalinganisha na takwimu za michoro halisi. Kama takwimu za mbili zinafanana, picha hiyo ni halisi, kama takwimu ziko tofauti basi picha hiyo itakuwa ni ya bandia. Mgunduzi wa mitambo hiyo ni Profesa wa chuo kikuu cha elimu cha mji mkuu Bibi Ouyang Qiming, yeye sio mpenzi wa kukusanya vitu vya sanaa, lakini katika kazi yake ya kawaida aliona kwamba, si kama tu mitambo ya upimaji wa kimwanga inafanya kazi katika utafiti wa dawa na ugonjwa, bali pia inaweza kutumiwa katika kuthibitisha michoro ya kale. Anasema:

"Baada ya kutoa mwanga juu ya picha iliyochorwa, chembechembe za picha hiyo zitaoneshwa katika matokeo ya vipimo. Kwa mfano, rangi nyeusi ina chembechembe kadhaa, lakini kati ya picha halisi na picha bandia, chembechembe za rangi nyeusi zinatofautiana sana, tunaweza kutofautisha picha halisi na picha bandia."

Lakini kazi kubwa ya kukamilisha kazi hiyo ni kutatua suala la mwanga kuharibu picha zilizochorwa. Kwa kuwa mahitaji ya picha za kuchorwa za kichina ni mwakubwa, ni rahisi kuathika kwa karatasi ya picha ya kuchorwa ya kichina kutokana na mwanga. Kuhusu hali hiyo, Profesa wa Chuo Kikuu cha Elimu cha mji mkuu Bibi Ouyang Qiming alijulisha kuwa, mabaki ya utamaduni ni athiriwa na mwanga, kwanza ni mwanga wa jua, mwingine ni mwanga wa kamera, lakini sasa mitambo hiyo inaweza kutoa mwanga usioharibu picha zilizochorwa. Mbali na hayo, mitambo hiyo inapaswa kuwa na sehemu ya kuhifadha takwimu za michoro ili kuthibitisha michoro halisi. Hivi sasa chuo kikuu cha elimu cha mji mkuu kinashirikiana na idara husika ya mabaki ya kale ili kupata mifano ya picha mbalimbali za kale zilizochorwa na kuzihifadhi kwenye kompyuta. Bibi Ouyang Qiming alidokeza kuwa

" kwanza tulipata takwmu husika za karatasi ya Enzi ya Song, kama picha zilizochorwa za enzi ya Song zikihitaji kuthibitishwa, tunaweza kufanya kazi ya kulinganisha takwimu hizo, kwa sababu karatasi za enzi mbalimbali zinatofautiana sana.

Habari zinasema kuwa, kituo cha takwimu kilikusanya takwimu za wachoraji wa zama tulizo nazo. Bila shaka katika kituo hicho pia kuna takwimu za wachoraji wa zamani. Kuhusu kutengenezwa kwa mitambo ya kuthibitisha michoro ya kale, mtaalamu wa kuthibitisha mabaki ya kale ambaye pia ni mtafiti wa Jumba la makumbusho la China Bw. Shi Shuqing alisema kuwa, mbinu hiyo ya kuthibitisha michoro ya kale si kama tu imewaondoa wasiwasi wa wapenzi wa kukusanya michoro ya kale bali pia imesaidia sana kazi ya kuthibiisha michoro ya kale. Lakini alisema kuwa, ingawa mbinu hiyo ina ubora wa kisayansi, lakini kutokana na mitindo tofauti mbalimbali ya michoro ya kale, bado ni vigumu sana kuthibitisha michoro kwa pande zote. Alisema kuwa, kama mbinu za kisayansi zitashirikishwa na mbinu za jadi itafanya kazi vizuri. Anasema:

" Hii ni mbinu muhimu ya kusaidia, lakini mbinu ya jadi ya kuthibitisha michoro ya kale kwa macho bado inahitaji kuendelea kuwepo. Hivyo, pande hizi mbili zikishirikiana pamoja zitatoa mchango mkubwa kwa kuthibitisha michora ya kale ya China."

Wapenzi wengi wa kukusanya mabaki ya kale ya utamaduni wanakubali maoni ya Bw. Shuqing. Bibi Renhua anayetoka Beijing alikusanya michoro ya kale ya kichina kwa miaka mingi. Alisema kuwa, kuthibitisha michoro ya kale ya kichina ni tatizo kubwa, uchambuzi wa kikemikali umewasaidia wapenzi wa kukusanya michoro ya kale. Anasema:

" kwa kuwa mbinu ya kuthibitisha michoro ya kale kwa uchambuzi wa kikemikali bado una kikomo. Hivyo kuunganisha njia ya kisayansi na mbinu ya jadi ni mbinu mwafaka ya kuthibitisha michoro ya kale ya China.

Idhaa ya kiswahili 2004-11-03