Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-12 21:01:08    
Kampuni ya Viwanda na Biashara ya Chuma na Chuma cha Pua ya China

cri

    Kampuni ya Viwanda na Biashara ya Chuma na Chuma cha Pua ya China ilianzisha shughuli zake barani Afrika katika miaka ya 90 ya karne iliyopita. Wakati huo, China ambayo ilikuwa imefungua mlango wazi ilivutia uwekezaji wa vitega uchumi vingi kutoka nchi za nje, wakati huo huo, China ilikuwa ikijitahidi kutafuta fursa nzuri ya biashara duniani.

    Wakati huo, ingawa China ilikuwa nchi kubwa ya kutengeneza chuma na chuma cha pua, lakini kiwango cha utengenezaji wa chuma cheupe kilikuwa chini sana, kutokana na ukosefu mkubwa wa Kromiamu ambayo ni madini muhimu katika kutengeneza chuma cheupe. Kutokana na hali hiyo, Afrika ya Kusini yenye maliasili makubwa ya Kromiamu, ikawa mwenzi mzuri wa ushirikiano wa China.

    Afrika ya Kusini ina maliasili nyingi ya Kromiamu, na akiba yake inafikia asilimia 72 ya ile ya duniani. Lakini maliasili yake ilikuwa haitumiki hayatumiwa vya kutosha kutokana na masuala mbalimbali. Ili kunufaisha pande zote mbili, China na Afrika ya Kusini zilifanya majadiliano kuhusu ushirikiano katika uchimbaji wa Kromiamu.

    Mwaka 1995, pande hizo mbili zilitia saini mkataba rasmi, na kuanzisha kampuni ya ubia ya ASA Metals (Pty)Ltd, ambayo mpaka sasa bado ni kampuni kubwa zaidi ya ubia kati ya China na Afrika ya Kusini. Afrika ya Kusini inamiliki asilimia 40 ya hisa ya mgodi unaoweza kuzalisha tani laki 4 za Kromiamu, wakati kampuni ya China inamiliki asilimia 60 ya hisa.

    Mradi huo umeonesha hali ya kusaidiana kiuchumi kati ya pande zote za China na Afrika ya Kusini. Kwa upande mmoja, Afrika Kusini ilikuwa imeingiza utaratibu kamili wa biashara na sheria kutoka Ulaya kutokana na hali ya kihistoria, lakini haikufahamu sana utaratibu wa biashara wa kimataifa, na kukosa uzoefu katika biashara na nje. Kwa upande mwingine, China imeonesha nguvu katika nyanja ya biashara na uendelezaji wa masoko, lakini inataka kujifunza utaratibu kamili wa biashara. Hali hiyo ilizifanya pande hizo mbili kushirikiana vizuri.

    Kromiamu ni madini yenye sumu. Katika kuchimba madini hayo, kampuni ya China ilichukua hatua zinazofikia kiwango cha Ulaya cha hifadhi ya mazingira, ili kuhakikisha mazingira ya huko hayachafuliwi.

    Licha ya Kromiamu, Afrika ya Kusini ina maliasili nyingi ya dhahabu, almasi na manganese, na teknolojia ya kisasa za kutengeneza chuma na chuma cha pua, lakini sehemu kubwa ya maliasili yake haijatumiwa kwa mafanikio. Kwa upande mwingine, China ina soko kubwa la madini, lakini inahitaji madini yenye kiwango cha juu. Kutokana na hayo, ushirikiano kati ya pande hizo mbili si kama tu utaiatia Afrika ya Kusini nafasi nyingi za ajira na kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi hiyo, bali pia utatatua tatizo la maliasili la China. Kutokana na hayo, ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili una mustakabali mzuri katika siku za usoni. Hivi sasa, Kampuni ya Viwanda na Biashara ya Chuma na Chuma cha Pua ya China inataka kukuza ushirikiano na Afrika ya Kusini, katika shughuli za kuchimba na kutengeneza madini ya manganese.

    Wakati mwandishi wetu wa habari alipofanya mahojiano hayo, alikutana na mwenyeji wa Afrika ya Kusini Bw. Moeletsi Mbeki ambaye ni ndugu wa rais Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini pia ni mwandishi maarufu wa habari wa nchi hiyo. Bw. Moeletsi Mbeki alisema, "Karne ya 21 ni karne ya Afrika. Binadamu hawatapata maendeleo katika nyanja zote bila ya maendeleo ya Afrika. Anaona kuwa, China inapaswa kushirikiana na Afrika ili kupata maendeleo ya pamoja.

    Bw. Mbeki anaona kuwa Afrika inaweza kujifunza mengi mazuri kutoka kwa China, akisema kuwa, ongezeko la haraka la uchumi wa China linatokana na juhudi za nchi hiyo kuweka mazingira mazuri kwa uwekezaji vitega uchumi kutoka nchi za nje na kukamilisha utaratibu wa sheria. Miji mbalimbali ya China inashindana kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji wa vitega uchumi ili kuvuta vitega uchumi vingi kutoka nje, kwani inafahamu kuwa kampuni za nchi za nje zitaleta faida baada ya kupata faida zao zenyewe, hii inastahiki kuzingatiwa na Afrika ya Kusini.

Idhaa ya Kiswahili 2004-11-12