Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-16 16:50:57    
Jumuiya ovu "Falungong"

cri
    Wasikilizaji wapendwa, kutokana na maombi ya wasikilizaji kadhaa leo tunafahamisha kuhusu jumuia ovu ya "Falungong".

    "Falungong" ni jumuiya ovu iliyotokea nchini China katika miaka ya 90 ya karne iliyopita. Kiongozi wa jumuiya hiyo Li Hongzhi alizua nadharia potovu na kuwadhibiti kifikra wafuasi wake na kufanya shughuli nyingi za kukiuka sheria nchini China.

   Uhalifu mkubwa wa "Falungong" ni kukiuka haki za binadamu na kufanya dhuluma kwa maisha ya binadamu. Kutokana kutawaliwa kiroho na Li Hongzhi, familia mamia kwa maelfu za wafuasi zilivunjika, na wakereketwa wagonjwa 1000 walikufa kutokana na kukataa matibabu na dawa, na mia kadhaa walijilemaza au kujiua, na zaidi ya raia wema 30 waliuawa na wafuasi wa jumuiya hiyo. Kwa mfano: tarehe 4 Septemba mwaka 1998, mfuasi wa "Falungong" Ma Jianmin wa mkoa wa Shandong alijipasua tumbo na kufa papo hapo kwa ajili ya kuona "Falun"( ati "gurudumu la ushirikina") lililotiwa na Li Hongzhi ndani ya tumbo lake. Mwingine ni Zhang Zhiqin aliyekuwa na ugonjwa wa kisukari. Mfuasi huyo tokea alipoanza kuwa mfuasi wa jumuiya hiyo ovu aliacha kabisa kutumia dawa akitegemea wafuasi wenzake kumsomea kitabu cha Li Hongzhi na kusikiliza kanda ya mahubiri ya Li Hongzhi, na matokeo yake alizidiwa na ugonjwa na kufa. Tarehe 23, Januari mwaka 2001, wafuasi saba wakiwa wanafuata matakwa ya Li Hongzhi ya "kuacha uhai" na "kukimbilia ukamilifu" walijichoma moto katika uwanja wa Tian An Men, matokeo yake wawili walikufa na watatu walijeruhiwa vibaya na wakapata ulemavu wa kudumu. Katika muda wa mwezi mmoja tu tokea tarehe 25 Mei hadi 26 Juni mwaka 2003 mfuasi wa "Falungong" Chen Fuyao mkoani Zhejiang aliwaua ombaomba 15 na mwumini mmoja wa dini ya Buddha kwa kuwalisha sumu kwa nyakati tofauti kwa ajili ya eti "kuwafikisha peponi".

    Uhalifu mwingine mkubwa uliofanywa na "Falungong" ni kudhuru jamii na kukiuka haki za biandamu. Ya kwanza katika maovu hayo ni kuvuruga upashanaji habari wa setilaiti. Kutokana na takwimu zisizokamilika, tokea 23 Juni mwaka 2002 jumuyia ya "Falungong" kisiwani Taiwan ilivuruga upashanaji habari wa setilaiti mara 128 kwa muda wa saa 70. Maovu ya pili ni kuharibu zana za huduma kwa umma, na kuingiza tangazo lake katika matangazo ya televisheni. Tokea mwaka 2002, matukio kama hayo yalikuwa 76 katika China bara. Kwenye tovuti yake ya mtandao wa internet kuna makala chungu nzima za kuchochea wafuasi kutangaza makala katika televisheni. Uhalifu wa tatu ni kusumbua na kutishia watu kwa simu na kutuma barua pepe chafu kupitia tovuti yake ya mtandao wa internet. Ili kufanikisha shughuli hizo za uhalifu, "Falungong" iliunda "kikundi maalumu cha kupiga simu" ambacho tovuti yake imetangaza kuwa jumla kilipiga simu mara milioni 10 kwa China bara. Katika miezi miwili tu ya Januari na Februari mwaka huu simu hizo zilikuwa zaidi milioni 8. Kwa mujibu wa takwimu, barua pepe chafu kutoka kwenye tovuti yake ya internet ya nchi za nje zilizidi milioni 30 kwa mwezi. Yote hayo yamekiuka vibaya haki za binadamu.

    "Falungong" pia ilishambulia kwa nia ovu mtu yeyote au shirika lolote lenye maoni tofauti nayo. Watu wengi wa idara za habari, sayansi na dini nchini China waliofichua shughuli za kukiuka sheria za jumuiya ovu ya "Falungong", "Falungong" iliwaogopa sana. Hivyo wafuasi wake waliwatukana, kuwazingira na kuwasumbua watu wenye maoni tofauti nao. Katika miaka kadhaa kabla ya kupigwa marufuku kwa jumuiya hiyo, watu wa jumuiya hiyo waliwahi kuvamia mara kumi kadhaa vyombo vya habari vya sehemu mbalimbali nchini. Walipovamia Gazeti la Chongqing, Jumuiya ya "Falungong" ilifika hadi kutoa "onyo" ikisema: Kama gazeti hilo halitaomba radhi, watu wa "Falungong" watafanya juhudi kwa pamoja, wataingiza mafuriko kuzika shirika hilo la gazeti, na kuifanya dunia iteketee kabla ya wakati. Hivi sasa kwenye tovuti ya mtandao wa internet ya "Falungong", kuna "orodha ya watu waovu", orodha ya "watu wanaosakwa" wakiwemo watu wengi mashuhuri kwenye jamii, kama vile Zhuang Fenggan, Pan Jiazheng na wanasayansi wengine, pamoja na Fu Tieshan, Sheng Hui na wanadini wengine maarufu. Wote hao wamewahi kuunga mkono serikali kuipiga marufuku jumuiya ya "Falungong", hivyo walisumbuliwa na kutishiwa na jumuiya hiyo, na hata usalama wao umetishiwa vibaya.

    Maneno ya uwongo na nadharia potofu ya Li Hongzhi ni mbinu muhimu ya kudhibiti roho ya watu waliofanya mazoezi ya "Falungong", vilevile ni chanzo cha madhara na uhalifu halisi mbalimbali uliofanywa na "Falungong. Kwa mfano, alisema binadamu waliwahi kutoweka mara 81, dunia itaharibiwa hivi karibuni, hivyo itamtegemea yeye kuzuia mlipuko wa dunia; alisema dunia ni kituo cha takataka za anga ya juu, na Marekani ni kiwanja kikubwa kabisa cha takataka duniani, ni "Falungong" tu ndiyo itakayoweza kukimbia; Li Hongzhi hawaruhusu watu wa "Falungong" waamini dini, alisema kuwa dini inaweza kuleta madhara kwa watu, na kila kitu duniani kinapangwa naye, hata Hitler kuwaua wayahudi yalikuwa matokeo ya mabadiliko ya mbinguni; alisema magonjwa hayawezi kuleta maradhi kwa mtu, mgonjwa asiende hospitali kukutana na madaktari, kutotumia dawa; alisema mtu akifanya mazoezi ya "Falungong" anapaswa kuacha kila kitu, "akiweza kuweka kando maisha au kifo ndiye mungu "Falungong" ni shetani, na "shetani mkubwa miongoni mwao anapaswa kuuawa, lakini watu wanaoamini "Falungong" anaweza kuwadhuru jamaa zake, na siku za baadaye wanaweza kuwalipia jamaa waliodhuriwa nao; anajidai kuwa "nadharia ya Falun" ni ya juu kuliko yoyote duniani, pamoja na sheria duniani. Anawatisha watu wote wanaofanya mazoezi ya "Falungong" wapaswa kukumbuka barabara nadharia yake hiyo, na kufuata maneno aliyoyasema katika shughuli zao.

   Umati wa watu wa China hasa jamaa waliodhuriwa pamoja na waumini wa dini walitoa ombi mara kwa mara serikali ya China kupiga marufuku "Falungong" kwa mujibu wa sheria. Ili kulinda haki za binadamu na uhuru wa kimsingi wa wananchi wengi, serikali ya China ilipiga marufuku jumuiya ovu ya "Falungong", hatua hiyo iliungwa mkono na jamii nzima. Serikali ya China inaona kuwa, watu wengi kabisa wanafanya mazoezi ya "Falungong" walidanganywa, wao pia ni watu waliodhuriwa, hivyo ilishikilia kutekeleza sera ya kuwashirikisha, kuwaelimisha na kuwaokoa watu wengi waliofanya mazoezi ya "Falungong". Jamii nzima ilifanya kazi nyingi kwa makini, kuwasaidia watu waliofanya mazoezi ya "Falungong" kujitoa kutoka kwenye minyororo ya kiroho ya jumuiya hiyo ovu. Hivi sasa watu wengi waliofanya mazoezi ya "Falungong" wametambua undani wa jumuiya ovu ya "Falungong", wamejitoa kutoka udhibiti wa kiroho wa Li Hongzhi, na kurudi kwenye jamii ya kawaida na kuishi maisha ya watu wa kawaida. Wale wachache walimotii "Falungong" na kufanya uhalifu waliadhibiwa kisheria, kwani walikiuka sheria na kufanya shughuli mbalimbali za uhalifu.

    Hivi sasa watiifu wachache wa "Falungong" wanaoongozwa na Li Hongzhi wanazusha uvumi nchini Marekani na sehemu nyingine za nje, walisema uwongo kuwa serikali ya China iliwakandamiza watu walioshiriki "Falungong", wanajipamba kuwa ni watu wanaotafuta "ukweli, udhati na uvumilivu" na "utamaduni wa jadi wa China, ili kuficha umaalum wa jumuiya ovu ya "Falungong". Lakini bila kujali wanajitetea nini, maneno aliyoyasema Li Hongzhi mbele ya watu waliofanya mazoezi ya "Falungong" wapatao zaidi ya milioni 2, na vitendo vingi halisi vya uhalifu vilivyofanywa na "Falungong" nchini China haviwezi kukanushwa. Mwaka 2003, mkoa wa Shanxi wa China uliwahi kufanya uchunguzi wa maoni ya watu, matokeo ya uchunguzi ni kuwa, asilimia 99.39 ya watu waliohojiwa waliona kuwa "Falungong" ni jumuiya ovu, asilimia 98.75 ya watu waliohojiwa waliunga mkono kupigwa marufuku kwa "Falungong". Hii ni nia ya raia. Hali halisi ni kuwa, katika dunia hii mbali na watu wachache wanaokusudia kutumia "Falungong", nchi nyingi kabisa na watu wanaotetea haki wanaona kuwa "Falungong" ni jumuiya ovu, na wote wanaunga mkono hatua mwafaka ya serikali ya China kupiga marufuku "Falungong".

Idhaa ya kiswahili 2004-11-16